CCM Waangukia pua uchaguzi mdogo jimbo la Mtambwe Pemba, na kukubali ushindi ACT Wazalendo

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
28 October 2023
Pemba, Zanzibar

MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA MTAMBWE PEMBA, ACT-WAZALENDO WAIBUKA KIDEDEA
1698515392758.png
Picha: Dr. Mohamed Ali Suleiman wa ACT-Wazalendo akizungumza wakati wa kampeni.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mtambwe Pemba Zanzibar , leo tarehe 28 oktoba 2023 amtangaza Dr. Mohamed Ali Suleiman mgombea wa ACT Wazalendo yaliyevuna kura 2449 kuwa mshindi huku mgombea Hamad Khamis wa CCM akiambulia kura 1531.


TOKA MAKTABA : MOTO WA UCHAGUZI

Historia ya jimbo la Mtambwe ambalo linatambulika ni jimbo mama waanzilishi wa siasa za uchaguzi wa vyama vingine, na ushindi utapeleka ujumbe Tanzania nzima na kote ulimwengu kuhusu ukubwa wa Mtambwe katika siasa za Zanzibar


View: https://m.youtube.com/watch?v=hkc5D3Q6XKY

11 October 2023​

Habari za figisu na Matukio ya majaribio ya kumuengua mgombea wa ACT Wazalendo asiwe mgombea uchaguzi mdogo.​

TUME YAKUBALI RUFAA YA UTENGUZI ACT WAZALENDO
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetengua uamuzi wa kumtengua Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo kwa nafasi ya Uwakilishi kwa Chama hicho ndugu. Mohammed Ali Suleiman katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe.

MKURUGENZI_4.jpg


Akitoa taarifa ya maamuzi ya rufaa kwa Vyombo vya Habari katika Afisi ndogo ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliyopo Chakechake kusini Pemba tarehe 10 Oktoba 2023, baada ya Chama cha ACT Wazalendo kukata rufaa kwa Tume hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndugu. Thabit Idarous Faina amesema,

“katika hatua za Uteuzi wa Wagombea Uchaguzi wa Jimbo la Mtambwe, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mtambwe alipokea pingamizi mbili (2) zilizowekwa na Wagombeawa CCM na ACT Wazalendo Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi katika pingamizi hizo ulikuwa kama ifuatavyo,alimteuwa Mgombea wa CCM kwa kuamini kuwa ana sifa zote za kuteuliwa kisheria kuwa Mgombea na hakumteua mgombea wa ACT Wazalendo baada ya kujiridhisha kwamba hakutimiza sifa za kuteuliwa kwa mujibu masharti ya kifungu cha 51 (1) Sheria ya Uchaguzi Namba 4 ya mwaka 2018, Kufuatia uamuzi huo Mgombea wa ACT Wazalendo Ndg. Mohammed Ali Suleiman amekata Rufaa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kufuata masharti ya kifungu Nam 52 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Nam 4 ya mwaka 2018”

Akielezea uamuzi wa rufaa hiyo baada ya kuzijadili hoja za utenguzi kwa pande zote mbili Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Zanzibar alisema

“Kuhusu Rufaa ya kupinga Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kumtengua Mgombea wa CCM Ndg Hamad Khamis Hamad kuwa Mgombea kwa sababu ya kutokukamilisha Fomu ya Uteuzi katika Kiambatanisho cha Fomu ya wadhamini ambayo ilijenga hoja ya kuwa taarifa zake haziwezi kumtambua Mgombea chini ya kifungu cha 51 (1) (a) Tume imeamua kwamba Msimamiziwa Uchaguzi alishindwa kuzingatia Kanuni ya 13 (8) ya kanuni za Uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo inamtaka msimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha kwamba Fomu anayopokea iwe imejazwa kwa ukamilifu kwa kuwa Msimamizi alishindwa kuzingatia matakwa ya Kanuni hiyo, halikuwa kosa la Mgombea kwa hivyo Tume ya Uchaguzi imetupilia mbali Rufaa hiyo na kuthibitisha kuwa Ndg Hamad Khamis Hamad anazo sifa za kugombea katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe”

Sambamba na hilo ameongeza kuwa kuhusu Rufaa ya kutoteuliwa kuwa Mgombea wa ACT Wazalendo Mohammed Ali Suleiman, kwa kutoa taarifa za uongo katika Fomu ya Uteuzi chini ya kifungu cha 51 (1) (b), Tume imebaini kuwa ushahidi uliowasilishwa kujenga hoja hiyo haukujitosheleza na hivyo imetengua uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi na kumteua Mohammed Ali Suleiman wa Chama cha ACT Wazalendo kuwa Mgombea wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe kupitia Chama hicho

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mtambwe unatarajia kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu ambapo vyama vinne vya Siasa ambavyo ni ACT Wazalendo, Chama cha Wananchi CUF, Chama cha Mapinduzi (CCM) na CHAUMMA vimeteuliwa kushiriki katika Uchaguzi huo. Source : https://www.zec.go.tz/index.php/habari/matukio/135-wasimamizi-wasaidizi-watakiwa-kusimamia-maadili
 
28 October 2023
Pemba, Zanzibar
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mtambwe Pemba Zanzibar , amtangaza Dr. Mohamed Ali Suleiman mgombea wa ACT Wazalendo yaliyevuna kura 2449 kuwa mshindi huku mgombea Hamad Khamis wa CCM akiambulia kura 1531
Vipi Jecha yuko wapi?
 
28 October 2023
Pemba, Zanzibar
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mtambwe Pemba Zanzibar , amtangaza Dr. Mohamed Ali Suleiman mgombea wa ACT Wazalendo yaliyevuna kura 2449 kuwa mshindi huku mgombea Hamad Khamis wa CCM akiambulia kura 1531
Huko walikuwa wanafanya uchaguzi au maigizo ya uchaguzi?

Halafu inakuwaje mshindi wa jimbo anapata kura 2500 na kuwa mbunge wakati Tanganyika hizo ni kura za mshindi wa mwenyekiti wa kijii au mtaa?

Kweli hii nchi huliwa na wajanja huku wajinga wakilalamika badala ya kuchukua hatua.
 
Huko walikuwa wanafanya uchaguzi au maigizo ya uchaguzi?

Halafu inakuwaje mshindi wa jimbo anapata kura 2500 na kuwa mbunge wakati Tanganyika hizo ni kura za mshindi wa mwenyekiti wa kijii au mtaa?

Kweli hii nchi huliwa na wajanja huku wajinga wakilalamika badala ya kuchukua hatua.
Mkuu wew ulitaka apate kura ngapi ?
 
Huko walikuwa wanafanya uchaguzi au maigizo ya uchaguzi?

Halafu inakuwaje mshindi wa jimbo anapata kura 2500 na kuwa mbunge wakati Tanganyika hizo ni kura za mshindi wa mwenyekiti wa kijii au mtaa?

Kweli hii nchi huliwa na wajanja huku wajinga wakilalamika badala ya kuchukua hatua.
Ni mambo ya hovyo sn
 
28 October 2023

LIVE🔴MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA MTAMBWE

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mtambwe akitangaza matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Mtambwe Pemba, Zanzibar


View: https://m.youtube.com/watch?v=a65XpI4F2iA

Kutoka maktaba :

More info : SABABU ZA UCHAGUZI MDOGO
Hii ni Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo la mtambwe Habibu Ali Mohamed, tume ya uchaguzi Zanzibar imeamua kufanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi hiyo iliopo wazi na wadau wote wa uchaguzi wanatakiwa kushiriki kukamilisha uchaguzi huo kama ilivyokusudiwa.

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kupitia Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph Kazi iliwaomba wananchi, wapiga kura wa jimbo la Mtambwe, vyama vya siasa, wenye nia ya kugombea, na wadau wengine wa uchaguzi kujitayarisha na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo huru na wa haki unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu 2023.

Kufuatakifo cha aliyekua Mwakilishi wa Jimbo hilo Habibu Ali Mohamed kilichotokea Machi 3 mwaka huu 2023., mwenyekiti wa ZEC Mh. jaji George Joseph Kazi amesema , kifungu cha 40 (2) (3) cha sheria ya uchaguzi namba nne ya mwaka 2018 kinajukumu la kuendesha uchaguzi mdogo si chini ya miezi minne na si zaidi ya miezi 12.

Source : https://www.zec.go.tz/index.php/habari/matukio/135-wasimamizi-wasaidizi-watakiwa-kusimamia-maadili
 
Mmh huo ushindi sijui kwa nini nina mashaka nao

Isijekuwa ni tego kwa baadae ACT nao wasijelalamika maana ccm kukubali tu bila purukushani yo yote si kawaida?
 
SIASA ZA TANZANIA

Uchaguzi mdogo Zanzibar unaakisi ushindani wa kisiasa?​

27.10.202327 Oktoba 2023
Ushindani wa kisiasa umeibuka tena kufuatia uchaguzi mdogo, jimbo la Mtambwe kisiwani Pemba iliko ngome ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Maalim Seif Sharif Hamad.


Mpiga kura akitumbukiza karatasi kwenye sanduku la kura

Mpiga kura akitumbukiza karatasi kwenye sanduku la kuraPicha: Emmanuel Herman/REUTERS
1698517920783.gif


Vyama vinne vinashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa kumtafuta mwakilishi wa jimbo hilo baada ya kufariki aliyekuwa mwakilishi wake, Habib Mohammed Ali, mapema mwaku huu, lakini mchuano wa wazi ni baina ya chama CCM na washindani wao na washirika wenzao kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa, ACT Wazalendo.

Kampeni zilitawaliwa na mtizamo wa hali za maisha ambapo wakati CCM kinaomba kuungwa mkono na wapiga kura kutokana kile inachodai "kuendelea kuleta maendeleo."
Huku chama cha ACT kikisema CCM haifai kupigiwa kura kwa sababu imeshindwa kuzuia kupanda kwa gharama za maisha.

Akifunga kampeni za chama chake cha ACT Wazalendo, makamu mwenyekiti wa chama hicho na makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, aliwataka wapigakura kukipa ushindi chama hicho.

Kwa upande wake, Chama cha Mapinduzi, CCM, kupitia makamo wa pili wa rais, Hemed Suleiman Abdulla, kimeomba wapiga kura kuunga mkono chama hicho ili kumpa nguvu zaidi Rais Mwinyi kuwatumikia.

Chaguzi ndogo kipimo cha demokrasia?

Uchaguzi huu mdogo wa Mtwambwe unafanyika baada ya chaguzi nyengine mbili ndogo kisiwani Pemba, iliko ngome ya muda mrefu ya upinzani.
Mpiga akiwekea alama ya wino baada ya kupiga kura

Mpiga akiwekea alama ya wino baada ya kupiga kuraPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Wa kwanza ulikuwa wa jimbo la Pandani ambapo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), iliitangaza ACT kwa ushindi kwa kura chache zaidi kuliko inavyokuwa kwenye chaguzi za kisiwani humo.

Mwengine ulikuwa uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Konde, ambao ulilazimika kurejewa tena baada ya awali, Tume ya Uchaguzi, ZEC, kumtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi.


Uchaguzi mdogo wa 28 October 2023 pia una umuhimu mkubwa kwa Rais Hussein Mwinyi kuona ni kwa kiasi gani anaungwa mkono katika jitihada zake za kuleta maendeleo.

Na vile vile ni kipimo kwa viongozi wapya wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ambayo sasa ina wajumbe wawili kutoka ACT Wazalendo, chini ya uwenyekiti wa Jaji George Kazi, ambaye ametowa wito kwawapiga kura kuzingatia sheria na kuweka mbele suala la amani.

Jumla ya wapiga kura 6,098 wanatarajiwa kupiga kura zao hapo tarehe 28 October 2023 na matarajio ya kutangazwa kabla ya kumalizika mapumziko ya mwisho wa wiki.
Source : DW.com
 
Pemba, Kaskazini

JARIBIO LA CCM LAISHIA, KUNYOOSHA MIKONO JUU NA KUKUBALI IMESHINDIKANA


View: https://m.youtube.com/watch?v=ObZvnB3PVFo
CCM mbele kwa mbele walivyotamani na kuwekeza nguvu kubwa kufanya jaribio kulinyakuwa jimbo la Mtambwe

Safu kubwa ya viongozi na vigogo wa CCM walipiga kambi na kuendesha kampeni isiyo na kikomo kuandika historia Kaskazini Pemba

Tazama video hapo juu na chini zilivyokuwa kampeni za chama dola kongwe walizoziita za kishindo na kali za kimkakati CCM jimbo la Mtambwe, sehemu iliyo ngome kwa Maalim Seif Sharif na ACT Wazalendo

CCM WAFUNGA KAMPENI MTAMBWE PEMBA KWA KISHINDO , MAKAMU WA PILI ASHUSHA NONDO ZA UKWELI


View: https://m.youtube.com/watch?v=6kvuxOZB0I4

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu, Hemed Suleiman Abdulla ameawaataka wananchi wa jimbo la Mtambwe kumchagua mgombea wa Chama Cha mapinduzi katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika 28 oktoba 2023 ili aweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo jimboni humo..

Akimnadi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Hamad Khamis Hamad wakati wa ufungaji wa kampeni za Chama hicho katika Jimbo la Mtambwe Mhe. Hemed amesema ongezeko la idadi ya wanachama wanaojiunga na CCM kutokea vyama pinzani ni dhahiri kuwa sera na utekelezaji wa Ilani ya CCM vimekubalika ndani ya Jimbo la Mtambwe hivyo wananchi wanayo kila sababu ya kumchagua Mgombea wa Chama cha Mapinduzi ili akashirikiane na viongozi wenzake katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mtambwe .

Mhe. Hemed amefahamisha kuwa maendeleo yanayoletwa na Serikali kupitia CCM yanawanufaisha wanachi wote ambapo amewataka wananchi kuondoa tofauti zao za kisiasa na kuungana pamoja katika kumchagua mgombea wa CCM akaendeleze mema na mazuri yanayofanywa na chama cha mapinduzi.

Amewataka wanachama wapya na wale wa zamani kushirikiana katika kumuombea kura mgombea wa CCM na kuhakikisha anashinda katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu ili aweze kuitekeleza vyema ilani ya CCM sambamba na kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Nae mgombea wa Uwakilishi kupitia tiketi ya CCM Jimbo la Mtambwe Ndg. Hamad Khamis Hamad amewaomba wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo kumpa ridhaa aweze kuwa mwakilishi wao katika baraza la wawakilishi ili aweze kuwatatulia changamoto zilizobaki Jimboni humo.

Amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe atahakikiasha anaendelea kuitekeleza vyema ilani ya CCM kwa vitendo na atashirikiana na viongozi na wananchi kuhakikisha analeta usawa katika upatikanaji wa maendeleo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Salum Suleiman Tate amesema Chama cha Mapinduzi kimefanya kampeni za kistaarabu na kisayansi kwa kutangaza sera Imara zinazotekelezeka na wamejipanga kushinda kwa kishindo katika Jimbo la Mtambwe.

Tate amesema CCCM itashinda bila ya kutumia nguvu kwa vile wapinzani wanajiunga na CCM makundi kwa makundi baada ya kujieone newma zinazoletwa na Rais Dkt Mwinyi.

Mapema Katika ufungaji wa kampeni hizo wananchi kadhaa wa jimbo hilo kutoka vyama pinzani wameamua kujiunga na CCM, hivyo kizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake waliojiunga na Chama hicho Ndugu,Salum Abdulla Salum maarufu Daiyadaiya kutoka chama cha ADC amesema ameamua kujiunga na CCM kutokana na kuwa na sera imara, haki na usawa kwa wanachama wote hivyo atahakikisha anashirikiana na uongozi uliopo kwenda kuongeza nguvu katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Amewanasihi wale wote ambao hawajafanya maamuzi ya kuhama upinzani muda bado wanao wa kuzinduka kutoka katika giza totoro na kujiunga na CCM chama ambacho neema zake zimeenea Zanzibar nzima chini ya Rais Makini Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)


 
Back
Top Bottom