MSITU WA AMAZON UNAUNGUA MOTO
Msitu wa Amazon katika nchi ya Ecuador.
Msitu wa Amazon ni
msitu mkubwa uliopo katika
bonde la
tropiki la
Mto Amazon.
Una
eneo la takribani
kilomita za mraba milioni saba, ambazo kati yake
tano na
nusu zimefunikwa na msitu wa
mvua.
Msitu huo unajumuisha
mataifa tisa: uko ndani ya
Brazil kwa
asilimia 60, ikifuatiwa na
Peru asilimia 13, na
Colombia asilimia 10, halafu
Venezuela,
Ecuador,
Bolivia,
Guyana,
Suriname na
Guyana ya Kifaransa kwa kiasi kidogo.
Kwa Taarifa nilizo ziona katika Website mbalimbali ikiwemo CNN zinasema kwamba msitu mkubwa Duniani wa #Amazon unaungua Moto kwa kasi kubwa na kwa eneo kubwa sana na kwa uvumi wa taarifa ambazo hazijathitishwa inasemekana moto huo ulianza takribani wiki 3 zilizopita na Rais wa Brazil analaumiwa kwa kutowajibika.
Chanzo cha moto kwenye msitu huu kutokana na historia yake huwa unasababishwa na Mgandamizo wa hewa haswa kipindi cha kiangazi cha Joto kali lakini kwa Taarifa za moto huu wa Sasa shirika la tafiti za Anga NASA wamesema kwamba moto huu umesababishwa na Shughuli za Kibinaadamu ikiwemo na uandaaji mashamba,lakini Rais wa Brazil anasema wanaharakati ndo wanaochochea zaidi ili aaribikiwe kisiasa.
Msitu huu wenye maili za mita za mraba Milioni 2.1 sawa na Kilometa za mraba Milioni 5.5 ukiwa na makadirio ya Miti mikubwa takribani Bilioni 390 ni Msitu muhimu sana kwa Dunia nzima.
Msitu huu unafahamika zaidi kuwa na viumbe wa ajabu na wakubwa ikiwemo aina ya nyoka wakubwa sana Dunia wanaofahamika zaidi kwa jina la Anaconda.
Hivi unajuwa kwamba Asilimia 20% ya Oxygen tunayotumia Dunia nzima inatengenezwa na Msitu huu?
Hivi unajuwa kiasi kikubwa cha Carbon dioxide inayoharibu Ozon layer yetu msitu huu unashiriki kwa kiasi kikubwa sana kufyonza Gesi hiyo?
Kama msitu huu utaungua kwa kiasi kikubwa basi Dunia nzima tutakuwa hatarini kimaisha na kwenye nyanja tofauti tofauti.
Mamlaka mbalimbali na vitengo maalumu vinavyohusika na masuala yote ya kijografia zipo zinalitizima jambo hili na taratibu za kuuzima moto zinaendelea japo umeshika eneo kubwa sana.
Tuombee Amazoni bado tunahitaji kuona nyoka wa Anaconda, bado nahitaji kuona miti yake mikubwa ambayo mvua ikinyesha hufika kwenye ardhi baada ya dakika 10.
Zaidi ya aina 3,000 za samaki zinapatikana ktk mto huu,250 za wanyama kama nyani,mamba,10,000 za miti mikubwa,70,000 za mimea mbalimbali na aina 1,800 za ndege uishi na kupatikana ktk misitu ya Amazon.
Amazon ni msaada kwa dunia nzima.
#Prayforamazon
#Prayforamazonia
#Prayforamazonrainforest
#amazonforest
#amazonrainforest.