Brazil: Msitu wa Amazon unaendelea kuwaka moto

Brazil: Msitu wa Amazon unaendelea kuwaka moto

Duu week ya 3 inamaana maelf ya ekari yameungua na maelfu ya viumbe wamekufa na inategemewa asilimia kubwa ya hewa safi duniani inapatikana Amazon....majanga ya dunia
Ubatizo wa moto
 
Kwa wiki ya tatu sasa msitu wa amazon unaendelea kuwaka moto.Moto kuwaka huwa kawaida katika msitu huo mkubwa zaid dunian lakin huu wa sasa unaonekana haudhibitiki.
View attachment 1187939


Chanzo cha moto haijulikani lakini mashirika yasio ya kiserikali na serikali ya nchini Brazil kila mmoja anamtuhumu mwenzake kuhusika na moto huo

View attachment 1187940

Msitu wa amazon ni muhimu sana kwa ustawi sio tu kwa brazil bali kwa dunia yetu kiujumla pamoja na vizazi vyetu vijavyo


#prayforamazon
Ni jambo ambalo haliepukiki... Tunaweza kuwalaumu wawashaji na kutafakari athari pamoja na maelfu ya viumbe hai wanaokufa lakini hii ni njia ya kiroho zaidi kusafisha uoza na uchafu mwingi ndani ya huo msitu... Moto huchoma na kuunguza kabisa usibakishe kitu
Baada ya hapo itatokea Amazon mpya yenye mimea mipya uoto na viumbe hai pia
 
Ni jambo ambalo haliepukiki... Tunaweza kuwalaumu wawashaji na kutafakari athari pamoja na maelfu ya viumbe hai wanaokufa lakini hii ni njia ya kiroho zaidi kusafisha uoza na uchafu mwingi ndani ya huo msitu... Moto huchoma na kuunguza kabisa usibakishe kitu
Baada ya hapo itatokea Amazon mpya yenye mimea mipya uoto na viumbe hai pia
Still bado uoto wa asili ndo unakufa.... Baadhi ya mimea na wanyama ndo wanzidi kupotea kabisa
 
Tukianza kupumua kwa shida usishangae mkuu asilimia 20 ya hewa tunayovuta inatokana na msitu wa amazon
#prayforamazon
Dah! Noma Sana kumbe hewa kutoka misitu ya hapo Drc haitutoshi?
 
MSITU WA AMAZON UNAUNGUA MOTO

Msitu wa Amazon katika nchi ya Ecuador.
Msitu wa Amazon ni msitu mkubwa uliopo katika bonde la tropiki la Mto Amazon.

Una eneo la takribani kilomita za mraba milioni saba, ambazo kati yake tano na nusu zimefunikwa na msitu wa mvua.

Msitu huo unajumuisha mataifa tisa: uko ndani ya Brazil kwa asilimia 60, ikifuatiwa na Peru asilimia 13, na Colombia asilimia 10, halafu Venezuela, Ecuador, Bolivia, Guyana, Suriname na Guyana ya Kifaransa kwa kiasi kidogo.

Kwa Taarifa nilizo ziona katika Website mbalimbali ikiwemo CNN zinasema kwamba msitu mkubwa Duniani wa #Amazon unaungua Moto kwa kasi kubwa na kwa eneo kubwa sana na kwa uvumi wa taarifa ambazo hazijathitishwa inasemekana moto huo ulianza takribani wiki 3 zilizopita na Rais wa Brazil analaumiwa kwa kutowajibika.

Chanzo cha moto kwenye msitu huu kutokana na historia yake huwa unasababishwa na Mgandamizo wa hewa haswa kipindi cha kiangazi cha Joto kali lakini kwa Taarifa za moto huu wa Sasa shirika la tafiti za Anga NASA wamesema kwamba moto huu umesababishwa na Shughuli za Kibinaadamu ikiwemo na uandaaji mashamba,lakini Rais wa Brazil anasema wanaharakati ndo wanaochochea zaidi ili aaribikiwe kisiasa.

Msitu huu wenye maili za mita za mraba Milioni 2.1 sawa na Kilometa za mraba Milioni 5.5 ukiwa na makadirio ya Miti mikubwa takribani Bilioni 390 ni Msitu muhimu sana kwa Dunia nzima.

Msitu huu unafahamika zaidi kuwa na viumbe wa ajabu na wakubwa ikiwemo aina ya nyoka wakubwa sana Dunia wanaofahamika zaidi kwa jina la Anaconda.

Hivi unajuwa kwamba Asilimia 20% ya Oxygen tunayotumia Dunia nzima inatengenezwa na Msitu huu?

Hivi unajuwa kiasi kikubwa cha Carbon dioxide inayoharibu Ozon layer yetu msitu huu unashiriki kwa kiasi kikubwa sana kufyonza Gesi hiyo?

Kama msitu huu utaungua kwa kiasi kikubwa basi Dunia nzima tutakuwa hatarini kimaisha na kwenye nyanja tofauti tofauti.

Mamlaka mbalimbali na vitengo maalumu vinavyohusika na masuala yote ya kijografia zipo zinalitizima jambo hili na taratibu za kuuzima moto zinaendelea japo umeshika eneo kubwa sana.
Tuombee Amazoni bado tunahitaji kuona nyoka wa Anaconda, bado nahitaji kuona miti yake mikubwa ambayo mvua ikinyesha hufika kwenye ardhi baada ya dakika 10.
Zaidi ya aina 3,000 za samaki zinapatikana ktk mto huu,250 za wanyama kama nyani,mamba,10,000 za miti mikubwa,70,000 za mimea mbalimbali na aina 1,800 za ndege uishi na kupatikana ktk misitu ya Amazon.
Amazon ni msaada kwa dunia nzima.

#Prayforamazon
#Prayforamazonia
#Prayforamazonrainforest
#amazonforest
#amazonrainforest.
 

Attachments

  • skynews-amazon-fires_4751293.jpg
    skynews-amazon-fires_4751293.jpg
    12.3 KB · Views: 33
Yaaah nimeiona hii taarifa lkn ajabu ni kwamba watu hawapo attention kabisa na swala hili
 
Waambie waache lana moto utazimika wenyewe.
Laana gani wewe bibi, ule msitu unakaliwa na indigenous people na wanaishi maisha yao ya asili kabisa bila usasa.
.
Wajerumani wana mashamba makubwa makubwa kwenye huo msitu ya kilimo na huwa wanatoa fedha za kuutunza msitu hiyo laana uliwapa wewe kapuku mtu mweusi?
 
Back
Top Bottom