Brazil: Msitu wa Amazon unaendelea kuwaka moto

Brazil: Msitu wa Amazon unaendelea kuwaka moto

manchoso

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
1,605
Reaction score
2,058
Kwa wiki ya tatu sasa msitu wa Amazon unaendelea kuwaka moto.Moto kuwaka huwa kawaida katika msitu huo mkubwa zaidi duniani lakini huu wa sasa unaonekana haudhibitiki.

index.jpg

Chanzo cha moto haijulikani lakini mashirika yasio ya kiserikali na Serikali ya nchini Brazil kila mmoja anamtuhumu mwenzake kuhusika na moto huo

images (2).jpeg

Msitu wa amazon ni muhimu sana kwa ustawi sio tu kwa brazil bali kwa dunia yetu kiujumla pamoja na vizazi vyetu vijavyo


#prayforamazon
Amazon.PNG


indesx.jpg

---------------
MSITU WA AMAZON UNAUNGUA MOTO

Msitu wa Amazon katika nchi ya Ecuador.
Msitu wa Amazon ni msitu mkubwa uliopo katika bonde la tropiki la Mto Amazon.

Una eneo la takribani kilomita za mraba milioni saba, ambazo kati yake tano na nusu zimefunikwa na msitu wa mvua.

Msitu huo unajumuisha mataifa tisa: uko ndani ya Brazil kwa asilimia 60, ikifuatiwa na Peru asilimia 13, na Colombia asilimia 10, halafu Venezuela, Ecuador, Bolivia, Guyana, Suriname na Guyana ya Kifaransa kwa kiasi kidogo.

Kwa Taarifa nilizo ziona katika Website mbalimbali ikiwemo CNN zinasema kwamba msitu mkubwa Duniani wa #Amazon unaungua Moto kwa kasi kubwa na kwa eneo kubwa sana na kwa uvumi wa taarifa ambazo hazijathitishwa inasemekana moto huo ulianza takribani wiki 3 zilizopita na Rais wa Brazil analaumiwa kwa kutowajibika.

Chanzo cha moto kwenye msitu huu kutokana na historia yake huwa unasababishwa na Mgandamizo wa hewa haswa kipindi cha kiangazi cha Joto kali lakini kwa Taarifa za moto huu wa Sasa shirika la tafiti za Anga NASA wamesema kwamba moto huu umesababishwa na Shughuli za Kibinaadamu ikiwemo na uandaaji mashamba,lakini Rais wa Brazil anasema wanaharakati ndo wanaochochea zaidi ili aaribikiwe kisiasa.

Msitu huu wenye maili za mita za mraba Milioni 2.1 sawa na Kilometa za mraba Milioni 5.5 ukiwa na makadirio ya Miti mikubwa takribani Bilioni 390 ni Msitu muhimu sana kwa Dunia nzima.

Msitu huu unafahamika zaidi kuwa na viumbe wa ajabu na wakubwa ikiwemo aina ya nyoka wakubwa sana Dunia wanaofahamika zaidi kwa jina la Anaconda.

Hivi unajuwa kwamba Asilimia 20% ya Oxygen tunayotumia Dunia nzima inatengenezwa na Msitu huu?

Hivi unajuwa kiasi kikubwa cha Carbon dioxide inayoharibu Ozon layer yetu msitu huu unashiriki kwa kiasi kikubwa sana kufyonza Gesi hiyo?

Kama msitu huu utaungua kwa kiasi kikubwa basi Dunia nzima tutakuwa hatarini kimaisha na kwenye nyanja tofauti tofauti.

Mamlaka mbalimbali na vitengo maalumu vinavyohusika na masuala yote ya kijografia zipo zinalitizima jambo hili na taratibu za kuuzima moto zinaendelea japo umeshika eneo kubwa sana.

Tuombee Amazoni bado tunahitaji kuona nyoka wa Anaconda, bado nahitaji kuona miti yake mikubwa ambayo mvua ikinyesha hufika kwenye ardhi baada ya dakika 10.

Zaidi ya aina 3,000 za samaki zinapatikana ktk mto huu,250 za wanyama kama nyani,mamba,10,000 za miti mikubwa,70,000 za mimea mbalimbali na aina 1,800 za ndege uishi na kupatikana ktk misitu ya Amazon.
Amazon ni msaada kwa dunia nzima.

#Prayforamazon
#Prayforamazonia
#Prayforamazonrainforest
#amazonforest
#amazonrainforest.
 
Tukianza kupumua kwa shida usishangae mkuu asilimia 20 ya hewa tunayovuta inatokana na msitu wa amazon
#prayforamazon
Kweli mkuu Ila wale mabeberu wanaweza kusaidia ku recover chap wakiamua kupanda miti mingine miundo mbinu ya msitu irudi kama kawaida.
 
Aaah aahaa aisee hatari afu naona wakubwa wa dunia wako kimya hili ni janga ilitakiwa waungane waangalie wanawasaidia vipi kabla hali haijawa tete zaid
Mrusi analipukiwa na manyuklia yake kwenye majaribio hana hamu kabiaaaa!!

China vita ya kiuchumi inamtoa kamasi! Hajui aiokoeje Huawei!

Uingereza BREXIT inawapasua kichwa balaa!!

France anaangalia namna ya kumpiga hela Iran kwa kudalalia usuluhishi!

Germany hofu imetanda ya recession!

Trump anawaza Uchaguzi.

Canada amemaindi wachina kususia minofu ya Nguruwe wake!!

India yuko kashmiiirrr!

Pakistan yuko kortin anapambania kashmir.

South Africa wameduwazwa na scandal ya Ramaphosa!!

Labda tutegemee muujiza wa WAFILISTI.
 
Back
Top Bottom