BoT Saga Unfolding: Ilikuwa Balali auwawe kwa sumu- Fununu !

Kulingana na raia mwema, Ballali alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na kutibiwa hata huko SA. Sasa hii sumu ilianza lini? Report ya raia mwema ni kama hapa chini:

"Serikali kwa kawaida haiwezi kuzungumzia ugonjwa wa mtu bila ridhaa kwanza ya familia, na familia ndiyo inayoweza kutoa taarifa ama kuiomba Serikali itoe taarifa kwa kushirikiana nayo, na hili la Ballali ni katika mantiki hiyo," alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali.

Ofisa huyo alisema Ballali amekuwa akiumwa kwa muda mrefu sasa japo amekuwa akipata matibabu ndani na nje ya nchi na kwamba kabla ya kwenda Marekani aliwahi kutibiwa nchini Afrika Kusini.
 
Kaazi kweli kweli.Polinium 210 au walisaga betri wakamkorogea kwenye chakula?
 
Kuna habari ya kuvunjika vunjika sina hakika nayo iko mwananchi....inasema hivi:
Dr Daudi Ballali amefutiwa visa ya Marekani, anadaiwa ametorokea Visiwa vya Malta
 
Kulingana na raia mwema, Ballali alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na kutibiwa hata huko SA. Sasa hii sumu ilianza lini? Report ya raia mwema ni kama hapa chini:

“Serikali kwa kawaida haiwezi kuzungumzia ugonjwa wa mtu bila ridhaa kwanza ya familia, na familia ndiyo inayoweza kutoa taarifa ama kuiomba Serikali itoe taarifa kwa kushirikiana nayo, na hili la Ballali ni katika mantiki hiyo,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali.

Ofisa huyo alisema Ballali amekuwa akiumwa kwa muda mrefu sasa japo amekuwa akipata matibabu ndani na nje ya nchi na kwamba kabla ya kwenda Marekani aliwahi kutibiwa nchini Afrika Kusini.

Mtanzania,

Kumbuka pia kuwa Raia mwema wamesema kuwa "Balali amekuwa anasumbuliwa kwa muda mrefu na kupata matibabu huko Afrika kusini". Balali amesemwa kuwa na magonjwa mengine kwa muda sasa lakini hayo hayahusiani sana na huu ugonjwa wake wa juzi uliopelekea afanyiwe upasuaji na kusafishwa tumbo.

Balali anastahili kupata adhabu kubwa sana kwa aliyofanya lakini hili la kutaka kumuona akifa mapema linatia wasiwasi wa nini kinapelekea kufichwa!
 
Mtanzania:
Hii habari ya sumuni tete, na hata jinsi ilivyoingizwa humu JF ni kwa njia za kutatanisha. Kwanza alianza Nshomile kuwa na 'contacts' za ndugu aliyepewa mtaji wa kufanyia biashara; na hadi hii eo Nshomile hajarejea tena kutueleza chochote. Huu unawez kuwa upandikizi wa habari. Halafu, mara tu baada ya habari ya Nshomile, kukajitokeza habari za Arsenic, sumu ambayo pengine tulitakiwa tuichukulie kuwa ndio iliyotumika kufanya kazi hiyo ya kumwondoa Balalli. Kwa ujumla bado kabisa hapajawa na taarifa inayoonyesha kwa ushahidi mkubwa kuwa kweli Balali alilishwa sumu; ingawaje kuna habari zinazosema alikula chakula pamoja na mstaafu mmoja, siku moja kabla ya kuanza matatizo ya kutapika na kuumwa tumbo. Huu sio ushahidi tosheleza, kwani la kushangaza ni kuwa mtu anayeshuku kulishwa sumu, na hapo hapo usubiri kufunga safari hai Marekani ndipo upate matibabu; haielekei kuwa habari ya maana sana.

Pamoja na yote haya, ilijulikana tokea huko nyuma kwamba huyu bwana afya yake ilikuwa sio nzuri siku nyingi. Kwa hiyo kuwa kwake huko hospitalini, tena akilipiwa na serikali, inatuonyesha pia kuwa huenda alikuwa akitibiwa maradhi yake ya kawaida ya siku nyingi
 
Mwafrika wa kike,

Kwa kweli kwangu mimi fisadi ni fisadi tu. Awe mgonjwa, buheri wa afya, mfu au hai. Mimi huwa nahuzunika mtu akitutoka dunia hii, lakini naelewa kuwa sote tutafikwa na mauti siku moja. Kwa mtaji huu, binafsi nisingefurahia kumwona Ballali ndani ya jeneza.

Kitu ambacho ningependa kuona ni Ballali akirudi akiwa hai. Suala la ufisadi ni kubwa na yeye ni mhusika mkubwa. Ningependa kuona anaweka mambo bayana; nani alihusika, kwa jinsi gani, kwa nafasi gani...badala ya kupeleka hizo siri kaburini.

Kama hizi tuhuma za sumu ni kweli, basi vijana wa JK (au ni BWM) ni sawa na KGB walivyomtenda Alexander Litvinenko. Huu ni unyama na ubinafsi wa wahusika kutaka kulinda matumbo yao na kumtoa mhanga Ballali.

Mimi naamini mfumo wa mtu huwa "innocent until proven guilty". Kwa Ballali, amekuwa guilty kwa mismanagement na criminal charges are pending. Hii ni nafasi yake kueleza msimamo wake na kujitetea kwani anayo kila haki ya kujitetea.
 
Ufisadi BoT: Baada ya kufukuzwa kazi, Marekani yamfutia viza Dk Ballali
* Ubalozi wasema hastahili kuishi nchini humo
* Wasema hawajui anakotibiwa

* Ndulu asisitiza kuwa bado ni mgonjwa

Dennis Msacky na Ramadhan Semtawa

SERIKALI ya Marekani ikiwa imetangaza kumfutia viza aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daud Ballali, anadaiwa kuwa ametorokea kwenye Visiwa vya Malta.

Kufuatia kufutiwa viza, Ballali sasa haruhusiwi kuishi wala kwenda nchini Marekani.

Katika hatua nyingine kumhusu mtuhumiwa huyo wa ufisadi, Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amedai kuwa baada ya Ballali kufukuzwa kazi wiki iliyopita alitorokea katika Kisiwa cha Malta kwa lengo la kujificha.

Katika mahojiano na Mwananchi, Dk Slaa alidai kuwa amepata habari kuwa wiki iliyopita Ballali aliondoka Marekani kwa ndege ya kukodi kuelekea Kisiwa cha Malta ili asiweze kurejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

"Nimepata taarifa kwamba Ballali wiki iliyopita alikodi ndege kwenda kujificha katika Kisiwa cha Malta ili asirejeshwe nchini, pia nimeambiwa aliondoka na madaktari watatu, baadaye nitatoa majina yao na namba za ndege aliyotumia
," alisema Dk Slaa.

Awali, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jaffery Salaiz, alisema wameamua kumfutia viza baada ya serikali ya Tanzania kuulizia hadhi ya gavana huyo anaposafiri au kuwako nchini mwao.

Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za uhamiaji za nchi hiyo, kuanzia sasa Ballali hawezi kuishi katika nchi hiyo wala kusafiri kwa kuwa viza yake imefutwa.

"Hakuna njia yoyote Ballali anaweza kuishi Marekani kwa kuwa viza yake imefutwa, hata kama ana mali kule," alisema.

Pia Afisa Balozi huyo alipoulizwa kama wana habari kuhusiana na Ballali kuwako katika matibabu nchini Marekani, alisema mpaka sasa hawajui kama kweli yuko nchini mwao, kwani wao wamekuwa wakisoma katika vyombo vya habari vya ndani.

"Mpaka sasa hatuna uhakika kwamba Ballali yuko Marekani, habari za kuwako kwake Marekani tumezipata kupitia vyombo vya habari vya ndani, lakini kama ubalozi hatuna taarifa rasmi kwa hilo," alisema.

Alisema Ballali alikuwa na viza ambayo alipewa kwa wadhifa wake wa kuwa Gavana wa BoT, lakini baada ya kufukuzwa kazi kwa madai ya ufisadi, imefutwa.

Hata hivyo, alisema kama Ballali atakuwa nchini Marekani basi itambidi arejee nchini Tanzania kwa kuwa hana kibali cha kuishi nchini humo.

Katika taarifa ya awali ya ubalozi, ilisema hatua hiyo inatokana na Ballali kutokuwa tena gavana wa BoT baada ya kuachishwa kazi.

Ballali ameachishwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kubainika ufisadi wa zaidi ya Sh 133 bilioni ambazo zililipwa chini ya uongozi wake.

Ufisadi huo unahusu Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambayo ukaguzi wa Kampuni ya Ernst&Young, ulithibitisha kufanyika katika kipindi cha mwaka 2005/06.

Marekani ikizungumzia zaidi sakata hilo, ilisema Tanzania iliulizia kuhusu hadhi ya Ballali, baada ya kuachishwa kazi kufuatia kubainika ufisadi huo mkubwa wa fedha za umma katika akaunti moja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali ya Marekani tayari imeitaarifu Serikali ya Tanzania kuwa inabatilisha viza ya Ballali kwa sababu haiwakilishi tena Tanzania.

Marekani ilisema Ballali alipewa viza hiyo kutokana na wadhifa wake kama mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.

"Kwa hiyo, kwa sababu ajira yake sasa imesitishwa, haiwakilishi tena serikali ya Tanzania na hastahili kuwa na viza aliyo nayo sasa hivi ambayo siyo ya kuhamia Marekani (non-immigrant visa status).

"Kuongeza uwazi na kupiga vita ufisadi ni maadili makuu mawili ambayo

Serikali ya Marekani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

vinayathamini sana," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Marekani inaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi kuhusu ubadhirifu uliofanywa kwenye BoT na inaamini kuwa uamuzi huu unadhihirisha azma ya Rais Kikwete kupambana na vitendo vya rushwa.

Katika taarifa hiyo, Marekani ilisema kuwa uchunguzi na ufunguzi wa mashtaka

wa haraka kwa wahusika katika kadhia ya BoT ni muhimu.

"Nchi zetu mbili zinafanya juhudi za dhati kufanya kazi pamoja kwa karibu katika

kung'oa mizizi ya rushwa na kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria, mtu

yeyote atakayepatikana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa," ilisema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alimweleza mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake jana kwamba, haijajulikana lini Ballali atarejea nchini kwa kuwa bado anaendelea na matibabu.

Profesa Ndulu alifafanua kwamba, Ballali kwa sasa anapata matibabu katika hospitali ambayo iko karibu na nyumbani kwake.

"Siwezi kujua atarejea lini nchini kwa sababu bado anaumwa, kuumwa anaumwa kweli," alisema Profesa Ndulu.

Kumekuwa na utata kuhusu Ballali kwamba amekuwa na uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Marekani hivyo kuwepo hofu ya kutorejea nchini.

Hata hivyo, uamuzi huo wa Marekani unaweza kuwa hatua moja mbele katika kushirikiana na serikali ya Tanzania kumrejesha

Inawezekana kweli jamaa huyu alikula hela nyingi sana kama ana uwezo wa kukodi ndege ya binafsi na kulipia gharama za madakari watatu kwa mpigo.
 
Kalamu,
Nikuulize swali moja tu kaka. Hivi kama umewekewa sumu kwenye chakula au kinywaji, utahitaji uthibitisho upi? Na kule Bongo hakuna post mortem kaka.
 
Kalamu,
Nikuulize swali moja tu kaka. Hivi kama umewekewa sumu kwenye chakula au kinywaji, utahitaji uthibitisho upi? Na kule Bongo hakuna post mortem kaka.

Jasus,

Hakuna kitu rahisi kama kufanya uchunguzi wa kulishwa sumu especially food poisoning. maana ni laboratory check ya matapishi au wastes zinaweza kudetermine sumu uliyopewa.

Ingawa kuna sumu nyingine zinahitaji softicated technology ambazo bado Tanzania kupitia ofisi ya mkemia mkuu zipo machine za kutosha.

Cha kushangaza kama kweli alillishwa sumu alikata ticket saa ngapi, aliwezaje kusafiri ilihaki akiwa na hali mbaya bila kuwa na daktari wa kumsaidia na walau first aid. Na kama alikua anatbiwa SA nadhani kunusuru maisha yake angeanzia SA ili baadae aende US. But nahisi huyu alitoroka kwa kisingizio za kuumwa na hata huko US haumwi anaspinn tu kwamba anaumwa.

Mimi nasema wanted either Dead or Alive. Tutafreeze hata hiyo nyumba yake ya US kulipia fidia ya fedha zetu
 
Kalamu,
Nikuulize swali moja tu kaka. Hivi kama umewekewa sumu kwenye chakula au kinywaji, utahitaji uthibitisho upi? Na kule Bongo hakuna post mortem kaka.

Mkuu Jasusi,

Mimi hili nilisema toka siku ya kwanza kabisa kwamba hapa tunaongopewa. Inaelekea kuna juhudi za wazi tena cordinated na upande wa Ballali kutaka kuendelea kutudanganya Wadanganyika. Kuna spinning kubwa sana hapa.

Kilichonishutua mimi ni kwamba ile barua ya Ballali kuna kila sababu ya kuamini ilivujishwa na upande wake. Hapo ndio machale yalipoanza kunicheza. Kama aliweza kupenyeza barua yake JF, kwanini asiweze kupenyeza ukweli wake?

Nafikiri kuna mambo mengi mno ambayo haya make sense kwenye story yake ndio maana hata ukijaribu kumpa a benefit of doubt bado inagoma kabisa.

Kama JK ameulizia status ya Billali USA, inaelekea yuko serious na hili. Kama Ballali anachosema ni sahihi basi huu ni wakati muafaka. Asije akafa na kuacha conspiracy theories zinaendelea kuzagaa wakati alikuwa na muda wa kuiweka case yake wazi.
 
Mbona habari zinasema FATHER BALALI alikuwa haumwi! Sasa tuamini vipi? Nasikia mshikaji alikuwa amewekwa tuu hospital Bosheni kuwazuga wananchi.
 
Mkuu Jasusi,

Mimi hili nilisema toka siku ya kwanza kabisa kwamba hapa tunaongopewa. Inaelekea kuna juhudi za wazi tena cordinated na upande wa Ballali kutaka kuendelea kutudanganya Wadanganyika. Kuna spinning kubwa sana hapa.

Kilichonishutua mimi ni kwamba ile barua ya Ballali kuna kila sababu ya kuamini ilivujishwa na upande wake. Hapo ndio machale yalipoanza kunicheza. Kama liweza kupenyeza barua yake JF, kwanini asiweze kupenyeza ukweli wake?

Nafikiri kuna mambo mengi mno ambayo haya make sense kwenye story yake ndio maana hata ukijaribu kumpa a benefit of doubt bado inagoma kabisa.

Kama JK ameulizia status ya Billali USA, inaelekea yuko serious na hili. Kama Ballali anachosema ni sahihi basi huu ni wakati muafaka. Asije akafa na kuacha conspiracy theories zinaendelea kuzagaa wakati alikuwa na muda wa kuiweka case yake wazi.

Mtanzania,

Swali moja limeulizwa hapa. Je Balali asemee wapi haya wewe na mimi tunataka sana ayaseme?

Kumbuka kuwa Kikwete kwa makusudi kabisa ameamua kusensor report ya Ernst and Young na kuacha kutaja makampuni kama DeepGreen and the like kwa makusudi kabisa na badala akataja makampuni yenye majina ya watu wa kawaida tu (au bila majina) na kisha kuamuru Bodi ya BOT "kuchunguza" kwa miezi sita.

Kuna tatizo kubwa sana hapa kwa Balali na kwa watu wengine hapa ya kuwa ni wapi Balali atoe na kusema aliyonayo. Wakubwa serikalini hawataki kabisa kusikia anachotaka kusema Balali na TISS wangependa kumuona amekufa. Nani ashughulikie kupata story ya Balali. Baadhi hapa tumejaribu kurisk all we have kupata hii story ila usiri na security system around this guy inatisha.

Angalia, Kikwete ametoa miezi sita kushughulikia report ya BOT kwa mategemeo kuwa may be by that time jamaa atakuwa kishakufa. Kuna mchezo mkubwa sana hapa unachezwa na kama unaweza, tuwasiliane kwenye PM, uje USA na ujaribu kufuatilia wapi na chochote kuhusu Balali then uone kina nani wanashow up.

CCM na hasa Kikwete wana alot ku-lose hapa. Kikwete anajua kabisa kuwa alitumia hizi pesa za wizi kununulia watu kofia na tisheti ili ashinde urais. DeepGreen inaelekea moja kwa moja TISS na kuna sababu kubwa sana kwa nini kikwete ameiondoa DeepGreen kwenye report.

Mimi namchukia Balali kama fisadi lolote la Tanzania ila hii jitihada ya mafisadi walio hai bongo kutaka kuona Balali amekufa inatisha kiwango cha kawaida cha kufikiri.
 
Balalli alichota hela lakini kiasi kikubwa kilienda kwingine.Kinachoendelea sasa hivi ni kuvuta muda na kupoteza malengo ili watanzania wasahau.
 
Kalamu,
Nikuulize swali moja tu kaka. Hivi kama umewekewa sumu kwenye chakula au kinywaji, utahitaji uthibitisho upi? Na kule Bongo hakuna post mortem kaka.

Jasusi:
Kama mtu umehisi kuwa mtu anataka kukumaliza, tena kwa sumu, unatapika na tumbo ni moto, huwezi kuwa na mawazo hata chembe ndogo tu, ya kufikiria niende hadi Marekani nikatibiwe hii sumu; kwani huna hakika ya kufika huko mzima tena - safari ya masaa mangapi? zaidi ya 18?

Mtu mwenye 'connection' nyingi kama Gavana wa Benki Kuu hawezi kukosa msaada wa madaktari hodari kabisa wa kumpa angalau huduma ya kuondoa sumu mwilini haraka kabla ya kuanza hiyo safari.

Uthibitisho kuwa amelishwa sumu, hilo ni jambo rahisi kufanyika. Ni kiasi tu cha kuchukua 'sample' ya hayo matapishi na kuyafanyia uchunguzi alipokuja huko Marekani. Kama hakuweza kufanya hivyo, katika hayo masaa takribani 30 baada ya kula hiyo sumu, bado uchunguzi wa kina wa sampuli za damu,kinyesi/mkojo, mate, viini vya tumboni/utumbo vingeweza kabisa kugundua hiyo sumu.

Hatujui kama ni madhara hayo ya sumu au harakati za upasuaji ndicho kilichomsababishia awe katika 'coma' inayozungumziwa kuwa alikuwa hajitambui. Kama ni upasuaji wa tumboni tu kuondoa utumbo uliokuwa umeathiriwa na sumu, sioni ni kwa vipi awe na hali hiyo ya kutojitambua kwa mda mrefu namna hiyo - labda kutokana na 'complications' zingine ambazo bado hatujaambiwa.
 
jamani ehhh tupunguze kuongea amabako mengine twaanza danganyana kama movies za hollywood sijui..

kama ameweza kutuma barua ya kustaafu,kukodi ndege na kulipia madaktari wa3 to malta kweli angeshindwa hata kutoa barua nyingine yenye ukweli wooote asambaze watu tuusome na tujue zipi mbichi na zipi mbovu???atleast hiyo itampunguzia mzigo wa kutokiri makosa yake duniani...

as nijuavyo mie once akifa..will be the end of the whole story abt wizi wa bot n stuffs kama muanavyo now hata waziri anamruka sembuse bosi wao mkuu na kudiriki kusema jamaa alidanganya wat wil tokea once akishakufaa??si ndo wizi wa ccm wooote utawekwa jina la balali kufunika kesi??
 
Mtanzania,
Heshima mkuu. Upande wa Balali mpaka sasa haujasema lolote. Ile barua iliyovujishwa JF ilitokea Tanzania. Ilivujishwa na Ikulu, ikachapishwa na Majira na sisi hapa JF tukaipata. Mzee Balali mpaka sasa hajasema lolote hapa JF au hata kwa magazeti ya Tanzania. Hata ndugu zake wamekuwa very discreet. Lakini a time will come, the truth will bear. Every drama has and end. Right now waachie jukwaa akina Meghji, Mwuungwana, UWT, lakini scene yao itafika mwisho. There will be a part 2 to the drama before the curtain comes down.
 
Hivi pesa zilizotoka nje ya nchi moja kwa moja kutoka BoT, ziko kwenye ripoti? Nauliza tu.
 
Mtanzania,

Swali moja limeulizwa hapa. Je Balali asemee wapi haya wewe na mimi tunataka sana ayaseme?

Kumbuka kuwa Kikwete kwa makusudi kabisa ameamua kusensor report ya Ernst and Young na kuacha kutaja makampuni kama DeepGreen and the like kwa makusudi kabisa na badala akataja makampuni yenye majina ya watu wa kawaida tu (au bila majina) na kisha kuamuru Bodi ya BOT "kuchunguza" kwa miezi sita.

Kuna tatizo kubwa sana hapa kwa Balali na kwa watu wengine hapa ya kuwa ni wapi Balali atoe na kusema aliyonayo. Wakubwa serikalini hawataki kabisa kusikia anachotaka kusema Balali na TISS wangependa kumuona amekufa. Nani ashughulikie kupata story ya Balali. Baadhi hapa tumejaribu kurisk all we have kupata hii story ila usiri na security system around this guy inatisha.

Angalia, Kikwete ametoa miezi sita kushughulikia report ya BOT kwa mategemeo kuwa may be by that time jamaa atakuwa kishakufa. Kuna mchezo mkubwa sana hapa unachezwa na kama unaweza, tuwasiliane kwenye PM, uje USA na ujaribu kufuatilia wapi na chochote kuhusu Balali then uone kina nani wanashow up.

CCM na hasa Kikwete wana alot ku-lose hapa. Kikwete anajua kabisa kuwa alitumia hizi pesa za wizi kununulia watu kofia na tisheti ili ashinde urais. DeepGreen inaelekea moja kwa moja TISS na kuna sababu kubwa sana kwa nini kikwete ameiondoa DeepGreen kwenye report.

Mimi namchukia Balali kama fisadi lolote la Tanzania ila hii jitihada ya mafisadi walio hai bongo kutaka kuona Balali amekufa inatisha kiwango cha kawaida cha kufikiri.

Mwafrika wa Kike,

Barua yake ya kujiuzulu aliitolea wapi? Kama aliweza kufikisha ujumbe wake wa kujiuzulu kwa Watanzania, nina uhakika anaweza kabisa kufikisha hata mambo mengine.
 
Back
Top Bottom