BoT Saga Unfolding: Ilikuwa Balali auwawe kwa sumu- Fununu !

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
WanaJF,

Nianze kwanza kwa kuwakumbusha jinsi ambavyo JF ilifanikiwa sana kwa kuwekwa barua ya Balali ya kujiuzulu hapa JF na story hiyo ikaenea kwenye vyombo vya habari Tanzania kiasi cha kufikia kina Saliva na wenzake kuchanganyikiwa na kuanza kukana hizo taarifa, habari nyingine zinazofikia vyanzo vya habari vya JF ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Balali akafanya interview na kipindi maarufu cha uchunguzi marekani cha 60 minutes.

Ikumbukwe pia kuwa mimi binafsi nimekuwa anti-Balali mkuu katika jamvi hili na mara kwa mara nimekuwa namuombea hadharani aende hell maana ndiko wezi na mafisadi wanastahili. Pamoja na haya yote, ujio wa afisa usalama mkuu wa serikali ya Kikwete RO hapa marekani kumjulia hali Balali na yale aliyosema baada ya kuonana naye vilinifanya nibadili uamuzi wangu kwa muda na kucheza the same game inayochezwa Tanzania.

Nilijiuliza sana maswali kuwa kwa nini RO asifurahie kuendelea vyema kwa Balali na aonekane kushangaa kumuona akipata nafuu kwa haraka? Kwa nini serikali ya Kikwete ilikataa kujiuzulu kwa Balali na baada ya muda mfupi Kikwete akatangaza kwa misifa mingi kuwa amemfuta kazi Balali? Haya yote yalipelekea nimtafute Balali ili nijue kulikoni.

Kwa vile kwa sasa hairuhusiwi kusema kama Balali anaendeleaje kiafya na yuko wapi hapa US, naomba usiniulize maswali kuwa nilikutana naye wapi maana sitakujibu. Yafuatayo ni maneno ya Balali mwenyewe kuhusu ugonjwa wake na kwa nini alikimbilia hapa Marekani:

1. Balali anadai kuwa aliitwa Dodoma bila sababu maalumu
2. Anashangaa kuwa aliyoulizwa Dodoma angeulizwa hata Dar
3. Anashangaa kwa nini alisindikizwa na mkubwa toka Dodoma
4. Alishangaa sana usiri uliondelea alipokuwa Dodoma
5. Anakumbuka kuwa alikunywa na kula Dodoma na kwenye ndege
6. Anadai kuwa matatizo yake yalianza haraka baada ya Dodoma
7. Mengine ni mambo ya kitabibu......

Binafsi simuonei huruma sana Balali lakini ningefurahi kuona akitoa story yake kwenye 60 minutes. Alichokifanya Balali ni kibaya na kinastahili adhabu kubwa lakini sio ya kujaribu kutoa maisha yake ili asitoe siri ya wizi mkubwa uliofanywa wakati wa uchaguzi wa ccm na baadaye taifa mwaka 2005.

Balali anastory kubwa sana ya kutoa na ninafanya juhudi zote kwa ushirikiano na baadhi ya watu ili story yake isikiwe na watanzania woooote.

Swali kubwa ni kuwa, kwa nini kuna watu wangependa sana kumuona Balali akiwa kwenye jeneza? Nani anafaidika sana na kifo cha mtu huyu (nitamwita fisadi akipona vizuri) ?
 
Bado hujamalizia story M.Kike Tumefungua masikio, macho na mdomo.
 
Balali asife kabla ya kutueleza ukweli kuhusu dili hili chafu. Atutajie mafisadi wenzake wote then akifa sisi kwetu poa tu, kwani yeye na kundi lake walikuwa na nia ya kuua watanzania masikini kama sisi.
 
Bado hujamalizia story M.Kike Tumefungua masikio, macho na mdomo.

Endelea kufuatilia hii thread na JF kwa ujumla. Mambo yanaanza kutoka sasa. Jamaa wanataka sana Balali afe ili kila mtu atupe lawamwa kwake. Kumbuka Kikwete alikataa barua yake ya kujiuzulu. Kumbuka alivyoanza Meghji na wenzake jana. Kuna mengi sana yatasemwa na serikali kuwa ni Balali alifanya.

Angalia vile Kikwete ameamua kuongelea EPA peke yake, na pia amechagua makampuni 22 tu na kuacha makampuni kibao kama .. Green nakadhalika kwenye ile habari yake ya kumfuta kazi. Kuna mchezo mkubwa sana umechezwa hapo BOT na vigogo wakubwa kabisa wa serikali ya Tanzania wanahusika na wangependa sana kuona mtu mmoja akibeba lawama zote badala yao.

Kinawaumiza sana wakisikia kuwa Balali bado yuko hai maana hawana uhakika atasema nini!
 
Yaleyale ya Kolimba!... The System.
Sikujua kama JK ni miongoni mwao. Eeeh Mungu wee JK mwogope Mungu wako na mkumbuke rafikio Mwaikambo aliyeondoka ukalia kama mtoto....
 
Naam,stori nzima itatoka tu, hilo halina ubishi. Hawa mafisadi wanadhani binaadam tutaendela kuwaabudu wao hadi lini?

Balali akitoka 60 minutes litakuwa jambo makini; lakini tutataka pia ha 60 minutes wamtafute Msanii Mkuu pia, tusikie atakavyojitetea.

Haya yetu masikio tu saa.
 
Mkuu Kalamu,

kumbuka pia kuwa 60 minutes wanachukua muda mrefu sana kabla hawajarusha story. Kinachotakiwa sasa hivi ni the guy kuwa kwenye record na kama jamaa wakichukua miezi 3 au 6 kurusha story basi wengine kwetu iwe subira tu.
 
iwapo balali alipewa sumu kweli kama inavyodaiwa, basi angefaa kuomba ulinzi wa kimtaifa ili aje tanzania kutaja wahalifu wenziwe
 
Yaleyale ya Kolimba!... The System.
Sikujua kama JK ni miongoni mwao. Eeeh Mungu wee JK mwogope Mungu wako na mkumbuke rafikio Mwaikambo aliyeondoka ukalia kama mtoto....

Mkandara:

Naona aibu kuongea na wewe kaka. Maana nilimshabikia sana Mkapa lakini uvundo alioacha unatia aibu.
 
Mtega hutegwa! Siku moja kabla ya kuanza kutapika kwa nguvu Bw. Balali inadaiwa alienda kupata msosi wa nguvu na mmoja wa viongozi wastaafu katika hali ya "kucatch up" na mambo yanayoendelea.

Ilikuwa ni baada ya kutoka huko ndiyo maumivu ya tumbo yalipoanza na kuanza kutapika. Kwa vile, ujanja ni kuwahi siyo kupata, Balali alijumlisha moja na moja na jibu likaja kuwa ni mbili, akachukua tiketi yake akaruka na kuwahi hospitali!

Kwanini hakutaka kwenda hospitali ya Taifa au yoyote nchini? Balali alihisi chochote kilichomsumbua kilitokana na chakula...Ukichanganya na madhaifu mengine aliyokuwa nayo... ilikuwa arudishe namba kiulaini kabisa! Lakini wakati mwingine dua la kuku halimpati mwewe! Jamaa amesavaivu, so far.

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kutokea.

a. Balali kudai ukimbizi ambao anatengenezewa na serikali ya Tanzania, kwa jinsi wanavyomtengeneza vibaya na hivyo akasema "fear of persecution" ambayo ni ground for political asylum.

b. Balali kutoweka ki namna. Katika ulimwengu wa plastic surgeries na Identity protection, Balali anaweza kubadilishwa sura na wajihi wake kiasi kwamba itakuwa vigumu kumfahamu ukiondoa kichwa chake ambacho jinsi kilivyoumba sidhani kama kuna Daktari anaweza kukibadilisha.

c. Kwa vile hakuna mkataba wa extradition kati ya marekani na Tanzania (sidhani kama upo?) Balali hatalazimishwa kurudishwa Tanzania isipokuwa kwa makubaliano maalum.

d. Balali anajiandaa kujibu mashambulizi na kurusha nyavu yake pana ya ushahidi na kusema nani alifanya nini. Kama kuna watu wanadhania Balali alifanya yote hayo bila kucover his behind, washtuke. Balali, anajua nani na nini kilifanyika kwani SITOSHANGAA kuna nakala za vimemo kadhaa toka kwa watu mashuhuri na baadhi ya mafaili yao yaliyokuwa BoT aliyahamisha na kuyaweka mahali fulani akijua kuwa siku moja anaweza kupata kibano.
 
M.wa kike, tunakuaminia lete data!!!

Umuhimu wa yeye kuendelea na uzima haupingiki.

Ila ifahamike kuwa, pesa walizoiba zingeweza kuokoa maisha ya maelfu ya watanzania wanaokufa kwa magonjwa yanayoweza kutibika kwa kisingizio cha nchi maskini.

Haiwezekani watu wachache waiibie nchi maskini kama Tanzania (japo haistaili kuitwa masikini kwa raslimali tulizonazo) kiasi chote hicho cha pesa.

Ndugu watanzania wenzangu naomba ifahamike kwamba, hiyo ni sehemu ndogo tu (asilimia 0.00000000000000000000000000000000001) ya pesa zote zinazoibiwa.
 
Yaleyale ya Kolimba!... The System.
Sikujua kama JK ni miongoni mwao. Eeeh Mungu wee JK mwogope Mungu wako na mkumbuke rafikio Mwaikambo aliyeondoka ukalia kama mtoto....

Mkandara:
Hao wanaolialia au kuchekacheka sana ndio hatari zaidi. Atalia kwa uchungu sana hapo kwenye msiba au kanisani au mskitini, akishatoka hakumbuki tena na kwenda kwenye maovu yale yale ayatendayo. Hawa ni watu wa kuogopwa, hawana msimamo imara.
 
Yaani mngejua ambavyo nimetulia naifuatilia hii habari, acha kabisa. Hapa ni muhimu Balali ananyue mdomo, hii ndio muhimu kuliko kitu kingine chochote sasa. Nina uhakikia kuna watu watabidilisha suruali na skirt sasa hivi maana za zamani zitakuwa zimeshakuwa kubwa mno.

Sasa hivi inabidi tuelekeze kampeni kwenye kumtaka Balali aseme neno; Tumwambie: Balali sema baba sema Taifa lipone. Sema ile hela ilienda wapi sema tu baba.
 
Kitila mimi mwenyewe hii issue inazidi kukoroga akili yangu day in day out. Nilimpinga Balali sana na nilikuwa naomba aongezewe moto mara saba na awekwe kwenye jehanum special. Baada ya kugundua kwa kiasi kinachoendelea na namna jamaa serikalini wanavyotaka this guy apotee haraka sana, nimeanza kuwa na wasiwasi wa kuhusu nini kinafichwa hapa.

The same argument utaiona pia kwenye issue hii ya BOT, watu wote tutakimbilia kutaka Balali na Meghji wasulubiwe huku tukiwaacha Mgonja na Mramba wakizuia list ya wezi wakubwa kabisa na hiyo carbal yao ya deepgreen and the like.

Balali amefanya makosa makubwa sana lakini hayafikii kitendo cha usalama wa taifa kutaka kuona this guy dead as soon as possible. Balali ameanza kugundua hilo na anaweza kwenda chini na alot of people kama karata zikichezwa vizuri.

Swali kuu hapa, ni nani atachezesha hii game kama wahusika wenyewe ni usalama wa taifa na wapambe wa karibu sana wa Kikwete?
 
Kitila mimi mwenyewe hii issue inazidi kukoroga akili yangu day in day out. Nilimpinga Balali sana na nilikuwa naomba aongezewe moto mara saba na awekwe kwenye jehanum special. Baada ya kugundua kwa kiasi kinachoendelea na namna jamaa serikalini wanavyotaka this guy apotee haraka sana, nimeanza kuwa na wasiwasi wa kuhusu nini kinafichwa hapa.

The same argument utaiona pia kwenye issue hii ya BOT, watu wote tutakimbilia kutaka Balali na Meghji wasulubiwe huku tukiwaacha Mgonja na Mramba wakizuia list ya wezi wakubwa kabisa na hiyo carbal yao ya deepgreen and the like.

Balali amefanya makosa makubwa sana lakini hayafikii kitendo cha usalama wa taifa kutaka kuona this guy dead as soon as possible. Balali ameanza kugundua hilo na anaweza kwenda chini na alot of people kama karata zikichezwa vizuri.

Swali kuu hapa, ni nani atachezesha hii game kama wahusika wenyewe ni usalama wa taifa na wapambe wa karibu sana wa Kikwete?[/QUOTE]

Hili ndo soo lenyewe...
No wonder most of African Leaders appoint their best buddies despite their competence to lead the intelligence institutions!
There is only one answer,... To make sure that they cover their butts .. hasa kwenye time kama hizi!

Script hapa imeshaandaliwa.
Enjoy game tu!
 
Kuna uwezekano pia hii script ikabadilishwa kama masnitch wakiongezeka huko TISS!
 
Bin Maryam,
Wala usiwe na noma maanake hata mimi nilikuwa mshabiki mkubwa wa Mkapa awamu ya kwanza, kusema kweli sikumpenda Mwinyi kabisa na sababu unaijua maanake tulisha zungumza huko bcstimes....
 
Hakuna cha sumu wala mtoto wa sumu, jamaa alikimbia kujikoa na kuwaokoa hao anaowalinda.

Hizi stories za sumu ni spinning ya makusudi ya kutaka kuondoa pressure kwa Ballali na kupeleka kwa watu wengine.

Kama aliweza kupenyeza barua yake ya kujiuzulu JF, hashindwi kupenyeza habari nyingine yoyote.

Sasa gloves are off, aache kuendelea kujificha, aseme anachokijua ili angalau huko mbele ya mungu anakoenda awe na sababu ya kusema japo alitubu.

Katika watu ambao hawakuwa na sababu za kuiba, Ballali ni mmoja wapo, lakini kama tunavyojua ufisadi ni kitu kibaya, unachota kila kitu hata kile ambacho hutaki kula.

Eti hata haelewi umuhimu wa kuitwa kwenye kamati ya bunge Dodoma? Hii ni kichekesho, alitaka wamfuate ofisini kwake kumhoji?
 
Back
Top Bottom