Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,057
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.
Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.
Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.
Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.
Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.
Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.
Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.
Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.
Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.
Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.
Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.
Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.
Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.
Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.
Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?
Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.
Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.
Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.