DOKEZO RC na RPC Dodoma, Polisi Jamii Kata ya Nala anatunyanyasa sana, tafadhali muondoeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mwanadodoma

Member
Mar 12, 2024
29
49
Naandika kwa uchungu mkubwa baada ya Mke wangu kufanyiwa udhalilishaji na huyu kijana mhuni anayeitwa MALIMA ambaye ni Polisi Jamii hapa Kata ya Nala.

Ni kijana ambaye anajiona yeye ni zaidi ya Polisi wa kawaida. Yeye ndie Polisi,yeye ndie Mwanasheria,yeye ndie Hakimu,yeye ndie Magereza. Kazi yake ni kukamata watu na kuwalazimisha wampe pesa akidai ili asiwafikishe Kituo cha Polisi.

Nimesikia Dodoma ameletwa RPC mpya ambaye ni Mwanamama hivyo RPC na RC wote ni wakinamama.

Tafadhali njooni Kata ya Nala itisheni kikao cha wananchi ili tuwaambie malalamiko yetu dhidi ya huyu Polisi Jamii anayeitwa MALIMA.

Ni mnyanyasaji sana kwa Wananchi wanyonge hasa wanawake kwa kuwa hawajui Sheria na Haki zao za msingi.

Haiwezekani mtu mmoja mhuni tu kwa kofia ya upolisi jamii awasumbue wake zetu kwa kumwaga vyakula vyao vya biashara akisema wamechafua mazingira kwa kumwaga maji yenye ukoko wakati ukweli ni kwamba aliwatongoza wakamkataa, na sasa anawakomesha kwa kuwakamata na kutaka wampe pesa akitishia kuwafunga jela.

Diwani anazo taarifa za unyanyasaji unaofanywa na huyu kijana lakini amekaa kimya. Tafadhali RC na RPC mpya Dodoma njooni Nala, itisheni Kikao ili msikie malalamiko yetu dhidi ya huyu mhuni polisi jamii anayeitwa Malima, tafadhali tusaidieni tumechoka na manyanyaso na uonezi wake.

Pia soma - Malima aliyetajwa na JamiiForums kuwa Polisi Jamii awekwa kikaangoni mbele ya mkutano wa hadhara
 
Poleni kwa changamoto mkuu

Huyo muhini anapatikana Nala sehemu gani? Siunaelewa Nala ni kubwa mkuu?
 
Watanzania uzezeta umezidi, ukondoo wa kipuuzi sana huu,Kenya huwezu sikia malalamiko kama haya, hao Police jamii ingekuwa ni kenya wangekuwa futi 6 chini ya aridhi. Ukondooo umewazidi
 
Naandika kwa uchungu mkubwa baada ya Mke wangu kufanyiwa udhalilishaji na huyu kijana mhuni anayeitwa MALIMA ambaye ni Polisi Jamii hapa Kata ya Nala.
Ni kijana ambaye anajiona yeye ni zaidi ya Polisi wa kawaida. Yeye ndie Polisi,yeye ndie Mwanasheria,yeye ndie Hakimu,yeye ndie Magereza. Kazi yake ni kukamata watu na kuwalazimisha wampe pesa akidai ili asiwafikishe Kituo cha Polisi. Nimesikia Dodoma ameletwa RPC mpya ambaye ni Mwanamama hivyo RPC na RC wote ni wakinamama. Tafadhali njooni Kata ya Nala itisheni kikao cha wananchi ili tuwaambie malalamiko yetu dhidi ya huyu Polisi Jamii anayeitwa MALIMA. Ni mnyanyasaji sana kwa Wananchi wanyonge hasa wanawake kwa kuwa hawajui Sheria na Haki zao za msingi. Haiwezekani mtu mmoja mhuni tu kwa kofia ya upolisi jamii awasumbue wake zetu kwa kumwaga vyakula vyao vya biashara akisema wamechafua mazingira kwa kumwaga maji yenye ukoko wakati ukweli ni kwamba aliwatongoza wakamkataa,na sasa anawakomesha kwa kuwakamata na kutaka wampe pesa akitishia kuwafunga jela. Diwani anazo taarifa za unyanyasaji unaofanywa na huyu kijana lakini amekaa kimya. Tafadhali RC na RPC mpya Dodoma njooni Nala,itisheni Kikao ili msikie malalamiko yetu dhidi ya huyu mhuni polisi jamii anayeitwa Malima, tafadhali tusaidieni tumechoka na manyanyaso na uonezi wake.
Punguzeni ukondoo, utawacost
 
Kuwa na akili za ku comment, jamaa kasema anatongoza wake zao wamekataa anamwaga chakula chao.
Sasa RPC na RC wanashirikiana kutongoza hao wanawake?
Hahaha wewe ndio umechemka, jamaa alikuwa anasema kutohusika kwa diwani huenda anashiriana naye na sio RC na RPC
 
Poleni kwa changamoto mkuu

Huyo muhini anapatikana Nala sehemu gani? Siunaelewa Nala ni kubwa mkuu?
Nala ya kwanza mpaka Jamaica ndio maeneo yake,yaani Wake zetu wakimuona anapita hujifungia ndani kwa jinsi alivyo mnyanyasaji,Nchi imekuwa na mambo ya ajabu sana hii. Diwani yupo na anajua,Mtendaji wa Mtaa yupo na anajua lakini wanafumbia macho hali hii
 
Diwani na Mtendaji wa Kata wameshindwa kumaliza issue ndogo hii. Mpaka kumpatia umaarufu wa huyo mhuni wenu kuandikwa jukwa hili.
Wameshindwa maana malalamiko dhidi ya huyo mhuni wanayo mengi sana na bado anaendelea kunyanyasa watu
 
Naandika kwa uchungu mkubwa baada ya Mke wangu kufanyiwa udhalilishaji na huyu kijana mhuni anayeitwa MALIMA ambaye ni Polisi Jamii hapa Kata ya Nala.

Ni kijana ambaye anajiona yeye ni zaidi ya Polisi wa kawaida. Yeye ndie Polisi,yeye ndie Mwanasheria,yeye ndie Hakimu,yeye ndie Magereza. Kazi yake ni kukamata watu na kuwalazimisha wampe pesa akidai ili asiwafikishe Kituo cha Polisi.

Nimesikia Dodoma ameletwa RPC mpya ambaye ni Mwanamama hivyo RPC na RC wote ni wakinamama.

Tafadhali njooni Kata ya Nala itisheni kikao cha wananchi ili tuwaambie malalamiko yetu dhidi ya huyu Polisi Jamii anayeitwa MALIMA.

Ni mnyanyasaji sana kwa Wananchi wanyonge hasa wanawake kwa kuwa hawajui Sheria na Haki zao za msingi.

Haiwezekani mtu mmoja mhuni tu kwa kofia ya upolisi jamii awasumbue wake zetu kwa kumwaga vyakula vyao vya biashara akisema wamechafua mazingira kwa kumwaga maji yenye ukoko wakati ukweli ni kwamba aliwatongoza wakamkataa, na sasa anawakomesha kwa kuwakamata na kutaka wampe pesa akitishia kuwafunga jela.

Diwani anazo taarifa za unyanyasaji unaofanywa na huyu kijana lakini amekaa kimya. Tafadhali RC na RPC mpya Dodoma njooni Nala, itisheni Kikao ili msikie malalamiko yetu dhidi ya huyu mhuni polisi jamii anayeitwa Malima, tafadhali tusaidieni tumechoka na manyanyaso na uonezi wake.
Inashangaza pia Mpo Nala.
Namba ya DC hamuna
Namba ya OCD hamna
Namba ya RC hamna
Namba ya DAS au RAS hamna
Namba ya RPC hamna
Namba ya RCO hamna
Namba ya Mnadhimu wa Polisi pia hamna?
😀

Ni uzembe pia huu
 
Naandika kwa uchungu mkubwa baada ya Mke wangu kufanyiwa udhalilishaji na huyu kijana mhuni anayeitwa MALIMA ambaye ni Polisi Jamii hapa Kata ya Nala.

Ni kijana ambaye anajiona yeye ni zaidi ya Polisi wa kawaida. Yeye ndie Polisi,yeye ndie Mwanasheria,yeye ndie Hakimu,yeye ndie Magereza. Kazi yake ni kukamata watu na kuwalazimisha wampe pesa akidai ili asiwafikishe Kituo cha Polisi.

Nimesikia Dodoma ameletwa RPC mpya ambaye ni Mwanamama hivyo RPC na RC wote ni wakinamama.

Tafadhali njooni Kata ya Nala itisheni kikao cha wananchi ili tuwaambie malalamiko yetu dhidi ya huyu Polisi Jamii anayeitwa MALIMA.

Ni mnyanyasaji sana kwa Wananchi wanyonge hasa wanawake kwa kuwa hawajui Sheria na Haki zao za msingi.

Haiwezekani mtu mmoja mhuni tu kwa kofia ya upolisi jamii awasumbue wake zetu kwa kumwaga vyakula vyao vya biashara akisema wamechafua mazingira kwa kumwaga maji yenye ukoko wakati ukweli ni kwamba aliwatongoza wakamkataa, na sasa anawakomesha kwa kuwakamata na kutaka wampe pesa akitishia kuwafunga jela.

Diwani anazo taarifa za unyanyasaji unaofanywa na huyu kijana lakini amekaa kimya. Tafadhali RC na RPC mpya Dodoma njooni Nala, itisheni Kikao ili msikie malalamiko yetu dhidi ya huyu mhuni polisi jamii anayeitwa Malima, tafadhali tusaidieni tumechoka na manyanyaso na uonezi wake.
Mbuluzeni mahakamani
 
Wanaume wa dodoma mna taka kua kama wa dar sasa wana ogopa mbwa 10...yani mvuta bangi mmoja mna muandikia uzi
 
Namfahamu huyo anayelalamikiwa Malima. Ni mpuuzi mmoja ambaye hata mimi alishawahi kunikuta napata bia zangu saa 5 Pub akaanza kunihoji eti kwa nini nakunywa Pombe muda wa kazi. Bila kuamuliwa na watu waliokuwa jirani ilikuwa nimng'oe meno. Ni kijamaa kipumbavu kinachoonea sana wananchi wasiojitambua hasa Wanawake. Anachokifanya huwa anachukua mfano TV yake au Subwoofer halafu anampa kijana anayefahamiana nae kisha anamwambia katafute Mteja hasa kwa vijana wenye viduka na vibiashara kule Nala. Kijana anaenda anauza huo mzigo. Kisha baada ya saa 1 huyu Malima anaenda na yule kijana aliyeenda kuuza akiwa amemfunga pingu mpaka pale alipouza. Anaanza kumtisha yule mnunuzi kwamba amenunua kitu cha Wizi na yupo chini ya ulinzi. Mnunuzi unakuta kweli mzigo bado upon palepale dukani kwake hivyo lazima aogope. Hivyo huyu Polisi Jamii anampiga Mnunuzi Mkwara inabidi mnunuzi akubali kuachia alichonunua kwa Malima bila kurudishiwa pesa yake. Malima anabeba mzigo wake anaurudisha kwake,kisha anarudi tena kwa mnunuzi kumtisha atoe pesa ili Kesi ifutwe kituoni. Kwa kuwa mnunuzi ni mshamba na muoga inabidi atoe pesa nyingine na kumpa huyo Malima bila kujua suala lote lilikuwa ni mpango.
Hivyo ni kijamaa kipumbavu sana sana
 
Back
Top Bottom