FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,819
Anza na usafi wa moyo kwanza then matunda utayaona,
Mimi nimefanya kazi na viongozi wengi wa kiislam nikakuta ni wabinfsi kweli kweli na ndo maana hata taasisi zao ziko hoi sana kimaendeleo but haohao ni swala tano, wansababisha migogoro mingi sana ktk jamii ya kiislam sana!!
Hakuna anaeufuata Uislam asiye msafi wa moyo, ukiona mtu hana usafi wa moyo ujuwe huyo haufati Uislam. Tafadhali usichanganye Uislam na Muislam.
Jisomee:
Qur'an 2:8 - 11
8. Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.
9. Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.
10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo.
11. Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji
12. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.