Boko haram ni zao la marekani Africa hata kwetu watakuja tu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Wakati wa utawala wa Bush, ndani ya Nigeria kulianzishwa kile kilicho fahamika kama ACRI, yaani Africa Response Initiative, lakini taasisi hii ilikuwa kama msimamizi wa taasisi nyingine inayofahamika kama ECOWAS au zaidi ilifahamika kama ECOMOG, kutokana na shughuli yake iliyofanyika Liberia ya kutuliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Nigeria ndani ya ECOMOG mchango wake ulionekana waziwazi, Nigeria iliweza kulimaliza sakata lile la Liberia bila msaada wowote kutoka kwenye taasisi za kimataifa na mataifa ya kimagharibi wala Washington. Taarifa za kijasusi kwenye mataifa ya Magharibi zinasema, mataifa hayo yalihofia endapo Nigeria itaendelea kuyamaliza matatizo yake na nchi jirani kwa kutumia ECOMOG, tafasiri yake ni kwamba, Nigeria itapata heshima kubwa ndani ya Afrika kiasi kwamba umuhimu wa mataifa ya kikoloni eneo hilo kama vile Uingereza na Ufaransa ukatoweka kabisa. Hivyo ushawishi wa mataifa hayo ya kimagharibi ukawa si chochote si lolote kwenye eneo hilo la Afrika Magharibi.
Sababu Liberia ilikuwa ni matokeo ya kazi chafu za Marekani, ingekuwa ni hatari sana kwa Liberia kuangukia kwenye mikono ya Nigeria kwa kutumia ECOMOG ambayo ilionesha mafanikio makubwa ya kutatua mizozo ya eneo hilo. Hivyo Marekani nayo haikuwa na budi ila kuingilia kati kuona uchafu wake bado unaendelea kuwepo kwa faida yake. Kwa maneno mengine ushawishi wa Marekani ndani ya Liberia nao ungefutwa na Nigeria, na maslahi ya mataifa ya magharibi katika eneo la Afrika magharibi yangebakia kwa watu hao wenyewe, kitu ambacho hakikubaliki katika sera zozote, kwenye zama zozote za mataifa ya Magharibi.
Suluhisho ikaonekana ni lazima Marekani na washirika wake, wahakikishe kuwa hali hiyo wanaibadilisha.
Ushawishi wa Nigeria kwenye mataifa ya Afrika lazima uzikwe na ECOMOG lazima ibaki kama mbwa asiyekuwa na meno. Lakini bila kuwashtua walio lala na kutengeneza mazingira ya chuki baina ya Marekani, washirika wake na nchi za Afrika Magharibi ambapo ushawishi wa Nigeria ni mkubwa, mpango huu ukaonekana utakuwa na tija zaidi kwa kutumia njia za kidiplomasia.
Ndipo Marekani walipokujwa na kile kilicho kuja kufahamika kama Africa Response Initiative (ACRI), lakini wakachagua nchi mahususi za kuwauzia ACRI na Nigeria ikawekwa kushoto, sababu ACRI ilikuja kufanya kazi ambayo tayari ilishamalizwa na ECOMOG, hivyo kwa Nigeria isingeuzika.
Hivyo wakatafuta washirika muhimu ndani ya ECOMOG na kuwauzia ACRI lengo ikiwa ni kuzitoa nchi hizo kwenye ushirika wa ECOMOG na hivyo kuibakiza Nigeria peke yake. Hivyo Nigeria ikaachwa na zikatafutwa nchi zilizo na ushawishi mkubwa ndani ya ECOMOG na kuuziwa ACRI ambayo iliahidi kuleta msaada ya kijeshi na kibinaadam.
Wakati Marekani na washirika wake, ambao ni Uingereza na Ufaransa wakiwauzia baadhi ya Waafrika ACRI, wakati huohuo walikuwa wakiziambia nchi hizo kuna haja ya ECOMOG kutizamwa upya na kupatiwa mwelekeo mwingine.
Mwisho wa yote ECOMOG ikawekwa pembeni kwenye mgogoro wa Liberia, na Marekani wakatengeneza AFRICOM kama kiranja wa mgogoro wa Liberia.
Kinyume na ilivyokuwa ACRI ambayo ilijaribu kila lililowezekana kuficha maslahi ya Marekani ndani ya mpango huo, kiasi cha kuzishirikisha nchi za Latin Amerika na Asia na mpaka UN, ilimradi tu, mapango uonekane ni kwa ajili ya Waafrika wenyewe na maendeleo yao. AFRICOM ilikuwa ni tofauti kabisa.
AFRICOM ilionekana kuandaliwa kufanya mipango na stratejia za kijeshi kulinda maslahi ya Marekani kwenye eneo hilo dhidi ya Wachina ambao ushawishi wao kidunia na ndani ya Afrika umefikia kwenye silingi bodi. Ushawishi huo wa Wachina ni changamoto kubwa na kikwazo kwa maslahi ya Marekani na washirika wake kwenye bara hili.
Ilikukabiliana na ukuaji huu wa ushawishi Wachina ndani ya Afrika na upanukaji wa viwanda vya Wachina kwenye bara hili, ni kazi ya AFRICOM kuhakikisha inayakamata maeneo yote ya kistartejia ndani ya Afrika na kuyaweka kwenye milki ya Marekani ilikuweza kumzuia Mchina kuzifikia hizo rasilimali na nishati kwa ajili ya uchumi wake unao kuwa kwa kasi ya ajabu.
Sasa basi ili AFRICOM iweze kufanya kazi yake vyema, inabidi nchi ambazo zimechaguliwa kama ni maeneo ya kistartejia, kwanza zizoroteshwe ndani kwa ndani kiasi kwamba zenyewe zitambue kwamba katu haziwezi kushindana na hali hiyo bila kwanza kupata msaada eidha kiufundi, kivifaa, wataalam kutoka Marekani.
- Kiufundi ni wanajeshi wako kwenda kupatiwa mafunzo ya kijeshi ndani ya Marekani au kwa Washirika wake.
- Kivifaa ni nchi yako kukopeshwa zana mahususi za kijeshi kupambana na janga husika.
- Kiutaalam ni nchi yako kuletewa wataalam kutoka Marekani kama vile FBI na wenzao kuja kukusaidia.
Nchi ambayo itakuwa imechaguliwa na Marekani na washirika wake halafu wakawa wabishi kwamba hawaelewi au wanajua sana na hawahitaji msaada wowote kutoka kwa mabwana wakubwa hao, itaanza kutengwa huku na huko kama Zimbabwe, na kuwekewa vikwazo kadha wa kadha kama Sudan na mwisho watatengenezwa watu wa kujifanya kuwa na mrengo tofauti na serikali na kutengeneza vurugu baina ya serikali na watu hao kiasi cha kupaza kelele kuingiliwa kwa nchi hiyo kijeshi na mataifa ya magharibi wakiongozwa na Marekani kama ilivyo tokea Libya
Tumeona kwa macho yetu hayo yakitoka kwenye nchi za maziwa makuu, ambapo Marekani mara kadhaa imepeleka wanajeshi wake na bado wapo Uganda na Rwanda kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kuzilinda nchi hizo na maharamia ambao wao Marekani wamewatengeneza. Wanajeshi hao utawakuta Somalia, Kenya sasa mlango nao upo wazi kama itakuwa bado hawajaingia kupitia ‘CTU’ ya Kenya.
Sudan tumeona kupitia blangeti la ‘Humantarian Aids’ lililoshonwa kwenye mashine ya Darfur ambapo Al-Bashir alishushiwa lawama zote. Watu wa kawaida wanakuambia ni kwa sababu ya Uislamu wake, au Waarabu hawawataki Wakristo. Sudan ya Kusini kunayo Mwarabu au Mwislamu? Mbona vurugu ndiyo zinashika kasi?
Waafrika tuna nini sisi jamani? Sudan ya Elbashir imetengwa na ulimwengu kutokana na kisanga hicho. Lakini hiyo ilikuwa ni kiboko kwa Elbashir kutokana na kusaini kwake ‘Dili la Mafuta ’ na Wachina na ‘kuzipotezea’ kampuni za Marekani. Hakuna ishu ya Uislamu hapo, wala Shariah, wala Uarabu, ishu ni nani kapata nini, na Mchina hatakiwi Afrika na Obama hiyo ndiyo jukumu lake kubwa alililogewa wakati anaachiwa ofisi na Bush.
Kwa mchezo huohuo tumemuona Gaddafi wa Libya akipotozwa. Ishu ilikuwa na bado inaendelea kuwa ni mafuta hakuna cha udikteta wala utawala bora, mafuta kwanza. Lakini zawadi kubwa kabisa kwa AFRICOM na malengo lake mahususi ni kujenga dola ya Marekani ndani ya Afrika, PAX AMERICANA IN AFRICA.
Libya hayupo, nani kabaki Afrika? Mwenye jeuri kama Libya? Mwenye utajiri na kiburi cha rasilimali na nishati muhimu kama Libya? Hapana shaka ni jina moja tu ndilo litasimama kwenye kinyang’anyiro hicho; NIGERIA. Hapo ndipo umuhimu wa BOKO HARAM ndani ya NIGERIA UNAPO ONEKANA.
WAKATI WEWE UNASHABIKIA KWAMBA NI SAWA HIVYO, ATI WANASIMAMISHA DOLA YA KIISLAM, ATI WANASIMAMISHA SHARIAH, ATI ... ... ... ADUI YAKO MBAYA KULIKO WOTE ANAWATAWALA NYOTE WEWE NA BOKO HARAM.
WANAENDELEA NA MCHEZO HUOHUO KWA KUTUMIA VIKUNDI VYA KIISLAM NA SISI TUNASHABIKIA, LAKINI TUTAKAPO GEUZA NYUSO ZETU NA KUTAZAMANA USO KWA USO NA ADUI YETU ...
KAZI YA BOKO HARAM
Tangu Oktoba 2010 mirindimo ya mabomu imekuwa ikisikika ndani ya Abuja, kutoka kwenye majengo ya serikali, taasisi za elimu, maeneo ya wazi na kwenye mikusanyiko ya watu na kuuwa takribani watu 15,000 na mauaji yupo huru kila akijisikia anatoa vidio yake na kuuambia ulimwengu kile anacho jisikia kuambia.
Serikali ipo, inayo majeshi, vifaa, mbinu na pesa, lakini haijaweza kufanya chochote mpaka Aprili 14 wanafunzi zaidi ya 300 wakatekwa na Boko Haram na kutokomea nao kusiko julikana. Sasa ni kama dunia nzima imeamka, turudishieni, turudishieni, turudishieni mabinti zetu ndiyo habari zinazo pamba vyombo vya habari.
Kama kawaida Boko Haram wakafetua albamu yao inayo sema hawatawarudisha kamwe mpake wapatiwe wenzao waliokamatwa na serikali, albamu hii nayo imeuza sana kutoka kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, kitaifa, magazeti na hata mitandao ya kijamii.
Watu tunajiuliza ni nani hao Boko Haram, wanacho taka nini? Vipi kwa muda wote huo serikali imeshindwa hata kufahamu makazi yao, sura zao? Mohammed Yussuf, kiongozi wa kundi asiye na maarifa na mbinu za kijeshi, kufumba na kufumbua anaikimbiza Nigeria yote na serikali yake mchakamchaka. Mbinu hizi za hali ya juu za kutega mabomu, kuteka watu nyara, kulipua majengo makubwa na kutoweka bila kuacha hata unyayo wake kajifunzia wapi? Ametolea wapi silaha hizo nzito za kivita? Anatolea wapi fedha za kuwalisha wanamgambo wake kiasi wasiweze kumsaliti?
Maswali ni mengi, mazito si ya kudharaulika na wala hayahitaji majibu mepesi.
Tafiti zinatambulisha kuwa, kazi inayo fanywa na Boko Haram kwa sasa ni shughuli kivuli za CIA ambazo zinaratibiwa na ubalozi wa Marekani ndani ya Nigeria.
Kwa kipindi sasa CIA wamekuwa wakiendesha kambi za siri za mafunzo na kuwafunda dhana za wahabisim and new salafisim kwenye vichochoro vya mipaka ya Niger, Chad na Cameroon.
Mwisho wa siku, hakuna Jihad, hakuna Shariah, hakuna dola ya Kiislam wala Uislam. Mwisho wa siku kuna Marekani na maslahi yake, na sisi wengine wote ni wanasesere tu
Kwanini nchi ambayo hapo kabla iliweza kutatua matatizo yake yenyewe, bila ushirika wowote wa kimataifa, na hata kutatua matatizo ya nchi jirani kama Liberia leo imegeuzwa kuwa mwanasesere na kituko kwenye jukwaa la kimataifa?
Je wananchi milioni 160 wa Nigeria watasimama pembeni na kuwaachia Marekani waifanye nchi yao kama walivyo ifanya Libya, Iraq, Afghanistan, Syria, Egypti, Latini Amerika na kwengineko? Ambako kote huko rekodi ya taifa hili jeuri na lenye kiburi imekuwa ni chafu na mbaya kurekodiwa kwenye vitabu huru vya historia.
Huu ni mtihani kwa Wanigeria, na somo kwa Waafrika wote.
 
Ulichoandika ni Sawa kuwa USA na nchi za ulaya zinahusika.

Ila huku Tanzania, wakija tunafuta dini zote maana katiba yetu imeandikwa "serikali ya Tanzania haina dini ila watu wake wana dini" unaelewa maana ya maneno hiyo!?

Tanzania siyo nchi ya kisportsport kama unavyodhania.

Tanzania yetu , ni Sawa na USA au Israel kwa hapo Africa.
 
Ukiona hivyo, basi kwisney!!

Yaani, elewa tayari una vitukuu basi, hapo wewe hao wajukuu na vitukuu wakusomee wewe unasikiliza tu.

Teeeeh teeeh teeeeh Haaaa haaaa teeeeh Haaaa.
uzee hatari kiongozi

Sent From My iDevice using Jamii Forums Auto-reply Mobile App
 
Kwa Tanzania Boko Haram itakuwa shida kuingia kutokana na geographical location yetu...
Wakisema watokee upande wa visiwa vinavyopakana na zenji, hakuna visiwa watakavyokaa tukawaacha salama hata mmoja (zenji ni Tz nayo).

Wakitokea Kenya tutawamaliza wote kwa ushirikiano na kenya yenyewe (Kenya haitokubali wahifadhi).

Wakitokea Uganda napo matokeo ni yaleyale.

Burundi ni mshirika wetu mkubwa unless utawala uliopo uvunjike aingie kiongozi ambaye hatutaelewana nae na hata akitokea akawafadhili naamini tutaingia wapiga vizuri

Rwanda wana ndoto zao kuimiliki EA economically hawatakubali upuuzi huo uwakatize.

Congo J.kabila ni ndugu yetu na hata akitoka bado tuna jeshi kule halitoweza waacha salama.

Malawi hawana udini mkubwa kiasi cha kuwahifadhi hata kama tuna mgogoro nao.

kifupi Tanzania tumekaa angle ambayo Boko haram kuweka kambi na kushambulia vigumu, WE ARE SAFE TO SOME EXTENT
 
Ukiangalia vzuri ata Sudan ya kusin wanapitia hayo hayo yule mpinzan anatumik na west kwasababu kun wese pale
 
Wakati wa utawala wa Bush, ndani ya Nigeria kulianzishwa kile kilicho fahamika kama ACRI, yaani Africa Response Initiative, lakini taasisi hii ilikuwa kama msimamizi wa taasisi nyingine inayofahamika kama ECOWAS au zaidi ilifahamika kama ECOMOG, kutokana na shughuli yake iliyofanyika Liberia ya kutuliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Nigeria ndani ya ECOMOG mchango wake ulionekana waziwazi, Nigeria iliweza kulimaliza sakata lile la Liberia bila msaada wowote kutoka kwenye taasisi za kimataifa na mataifa ya kimagharibi wala Washington. Taarifa za kijasusi kwenye mataifa ya Magharibi zinasema, mataifa hayo yalihofia endapo Nigeria itaendelea kuyamaliza matatizo yake na nchi jirani kwa kutumia ECOMOG, tafasiri yake ni kwamba, Nigeria itapata heshima kubwa ndani ya Afrika kiasi kwamba umuhimu wa mataifa ya kikoloni eneo hilo kama vile Uingereza na Ufaransa ukatoweka kabisa. Hivyo ushawishi wa mataifa hayo ya kimagharibi ukawa si chochote si lolote kwenye eneo hilo la Afrika Magharibi.
Sababu Liberia ilikuwa ni matokeo ya kazi chafu za Marekani, ingekuwa ni hatari sana kwa Liberia kuangukia kwenye mikono ya Nigeria kwa kutumia ECOMOG ambayo ilionesha mafanikio makubwa ya kutatua mizozo ya eneo hilo. Hivyo Marekani nayo haikuwa na budi ila kuingilia kati kuona uchafu wake bado unaendelea kuwepo kwa faida yake. Kwa maneno mengine ushawishi wa Marekani ndani ya Liberia nao ungefutwa na Nigeria, na maslahi ya mataifa ya magharibi katika eneo la Afrika magharibi yangebakia kwa watu hao wenyewe, kitu ambacho hakikubaliki katika sera zozote, kwenye zama zozote za mataifa ya Magharibi.
Suluhisho ikaonekana ni lazima Marekani na washirika wake, wahakikishe kuwa hali hiyo wanaibadilisha.
Ushawishi wa Nigeria kwenye mataifa ya Afrika lazima uzikwe na ECOMOG lazima ibaki kama mbwa asiyekuwa na meno. Lakini bila kuwashtua walio lala na kutengeneza mazingira ya chuki baina ya Marekani, washirika wake na nchi za Afrika Magharibi ambapo ushawishi wa Nigeria ni mkubwa, mpango huu ukaonekana utakuwa na tija zaidi kwa kutumia njia za kidiplomasia.
Ndipo Marekani walipokujwa na kile kilicho kuja kufahamika kama Africa Response Initiative (ACRI), lakini wakachagua nchi mahususi za kuwauzia ACRI na Nigeria ikawekwa kushoto, sababu ACRI ilikuja kufanya kazi ambayo tayari ilishamalizwa na ECOMOG, hivyo kwa Nigeria isingeuzika.
Hivyo wakatafuta washirika muhimu ndani ya ECOMOG na kuwauzia ACRI lengo ikiwa ni kuzitoa nchi hizo kwenye ushirika wa ECOMOG na hivyo kuibakiza Nigeria peke yake. Hivyo Nigeria ikaachwa na zikatafutwa nchi zilizo na ushawishi mkubwa ndani ya ECOMOG na kuuziwa ACRI ambayo iliahidi kuleta msaada ya kijeshi na kibinaadam.
Wakati Marekani na washirika wake, ambao ni Uingereza na Ufaransa wakiwauzia baadhi ya Waafrika ACRI, wakati huohuo walikuwa wakiziambia nchi hizo kuna haja ya ECOMOG kutizamwa upya na kupatiwa mwelekeo mwingine.
Mwisho wa yote ECOMOG ikawekwa pembeni kwenye mgogoro wa Liberia, na Marekani wakatengeneza AFRICOM kama kiranja wa mgogoro wa Liberia.
Kinyume na ilivyokuwa ACRI ambayo ilijaribu kila lililowezekana kuficha maslahi ya Marekani ndani ya mpango huo, kiasi cha kuzishirikisha nchi za Latin Amerika na Asia na mpaka UN, ilimradi tu, mapango uonekane ni kwa ajili ya Waafrika wenyewe na maendeleo yao. AFRICOM ilikuwa ni tofauti kabisa.
AFRICOM ilionekana kuandaliwa kufanya mipango na stratejia za kijeshi kulinda maslahi ya Marekani kwenye eneo hilo dhidi ya Wachina ambao ushawishi wao kidunia na ndani ya Afrika umefikia kwenye silingi bodi. Ushawishi huo wa Wachina ni changamoto kubwa na kikwazo kwa maslahi ya Marekani na washirika wake kwenye bara hili.
Ilikukabiliana na ukuaji huu wa ushawishi Wachina ndani ya Afrika na upanukaji wa viwanda vya Wachina kwenye bara hili, ni kazi ya AFRICOM kuhakikisha inayakamata maeneo yote ya kistartejia ndani ya Afrika na kuyaweka kwenye milki ya Marekani ilikuweza kumzuia Mchina kuzifikia hizo rasilimali na nishati kwa ajili ya uchumi wake unao kuwa kwa kasi ya ajabu.
Sasa basi ili AFRICOM iweze kufanya kazi yake vyema, inabidi nchi ambazo zimechaguliwa kama ni maeneo ya kistartejia, kwanza zizoroteshwe ndani kwa ndani kiasi kwamba zenyewe zitambue kwamba katu haziwezi kushindana na hali hiyo bila kwanza kupata msaada eidha kiufundi, kivifaa, wataalam kutoka Marekani.
- Kiufundi ni wanajeshi wako kwenda kupatiwa mafunzo ya kijeshi ndani ya Marekani au kwa Washirika wake.
- Kivifaa ni nchi yako kukopeshwa zana mahususi za kijeshi kupambana na janga husika.
- Kiutaalam ni nchi yako kuletewa wataalam kutoka Marekani kama vile FBI na wenzao kuja kukusaidia.
Nchi ambayo itakuwa imechaguliwa na Marekani na washirika wake halafu wakawa wabishi kwamba hawaelewi au wanajua sana na hawahitaji msaada wowote kutoka kwa mabwana wakubwa hao, itaanza kutengwa huku na huko kama Zimbabwe, na kuwekewa vikwazo kadha wa kadha kama Sudan na mwisho watatengenezwa watu wa kujifanya kuwa na mrengo tofauti na serikali na kutengeneza vurugu baina ya serikali na watu hao kiasi cha kupaza kelele kuingiliwa kwa nchi hiyo kijeshi na mataifa ya magharibi wakiongozwa na Marekani kama ilivyo tokea Libya
Tumeona kwa macho yetu hayo yakitoka kwenye nchi za maziwa makuu, ambapo Marekani mara kadhaa imepeleka wanajeshi wake na bado wapo Uganda na Rwanda kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kuzilinda nchi hizo na maharamia ambao wao Marekani wamewatengeneza. Wanajeshi hao utawakuta Somalia, Kenya sasa mlango nao upo wazi kama itakuwa bado hawajaingia kupitia ‘CTU’ ya Kenya.
Sudan tumeona kupitia blangeti la ‘Humantarian Aids’ lililoshonwa kwenye mashine ya Darfur ambapo Al-Bashir alishushiwa lawama zote. Watu wa kawaida wanakuambia ni kwa sababu ya Uislamu wake, au Waarabu hawawataki Wakristo. Sudan ya Kusini kunayo Mwarabu au Mwislamu? Mbona vurugu ndiyo zinashika kasi?
Waafrika tuna nini sisi jamani? Sudan ya Elbashir imetengwa na ulimwengu kutokana na kisanga hicho. Lakini hiyo ilikuwa ni kiboko kwa Elbashir kutokana na kusaini kwake ‘Dili la Mafuta ’ na Wachina na ‘kuzipotezea’ kampuni za Marekani. Hakuna ishu ya Uislamu hapo, wala Shariah, wala Uarabu, ishu ni nani kapata nini, na Mchina hatakiwi Afrika na Obama hiyo ndiyo jukumu lake kubwa alililogewa wakati anaachiwa ofisi na Bush.
Kwa mchezo huohuo tumemuona Gaddafi wa Libya akipotozwa. Ishu ilikuwa na bado inaendelea kuwa ni mafuta hakuna cha udikteta wala utawala bora, mafuta kwanza. Lakini zawadi kubwa kabisa kwa AFRICOM na malengo lake mahususi ni kujenga dola ya Marekani ndani ya Afrika, PAX AMERICANA IN AFRICA.
Libya hayupo, nani kabaki Afrika? Mwenye jeuri kama Libya? Mwenye utajiri na kiburi cha rasilimali na nishati muhimu kama Libya? Hapana shaka ni jina moja tu ndilo litasimama kwenye kinyang’anyiro hicho; NIGERIA. Hapo ndipo umuhimu wa BOKO HARAM ndani ya NIGERIA UNAPO ONEKANA.
WAKATI WEWE UNASHABIKIA KWAMBA NI SAWA HIVYO, ATI WANASIMAMISHA DOLA YA KIISLAM, ATI WANASIMAMISHA SHARIAH, ATI ... ... ... ADUI YAKO MBAYA KULIKO WOTE ANAWATAWALA NYOTE WEWE NA BOKO HARAM.
WANAENDELEA NA MCHEZO HUOHUO KWA KUTUMIA VIKUNDI VYA KIISLAM NA SISI TUNASHABIKIA, LAKINI TUTAKAPO GEUZA NYUSO ZETU NA KUTAZAMANA USO KWA USO NA ADUI YETU ...
KAZI YA BOKO HARAM
Tangu Oktoba 2010 mirindimo ya mabomu imekuwa ikisikika ndani ya Abuja, kutoka kwenye majengo ya serikali, taasisi za elimu, maeneo ya wazi na kwenye mikusanyiko ya watu na kuuwa takribani watu 15,000 na mauaji yupo huru kila akijisikia anatoa vidio yake na kuuambia ulimwengu kile anacho jisikia kuambia.
Serikali ipo, inayo majeshi, vifaa, mbinu na pesa, lakini haijaweza kufanya chochote mpaka Aprili 14 wanafunzi zaidi ya 300 wakatekwa na Boko Haram na kutokomea nao kusiko julikana. Sasa ni kama dunia nzima imeamka, turudishieni, turudishieni, turudishieni mabinti zetu ndiyo habari zinazo pamba vyombo vya habari.
Kama kawaida Boko Haram wakafetua albamu yao inayo sema hawatawarudisha kamwe mpake wapatiwe wenzao waliokamatwa na serikali, albamu hii nayo imeuza sana kutoka kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, kitaifa, magazeti na hata mitandao ya kijamii.
Watu tunajiuliza ni nani hao Boko Haram, wanacho taka nini? Vipi kwa muda wote huo serikali imeshindwa hata kufahamu makazi yao, sura zao? Mohammed Yussuf, kiongozi wa kundi asiye na maarifa na mbinu za kijeshi, kufumba na kufumbua anaikimbiza Nigeria yote na serikali yake mchakamchaka. Mbinu hizi za hali ya juu za kutega mabomu, kuteka watu nyara, kulipua majengo makubwa na kutoweka bila kuacha hata unyayo wake kajifunzia wapi? Ametolea wapi silaha hizo nzito za kivita? Anatolea wapi fedha za kuwalisha wanamgambo wake kiasi wasiweze kumsaliti?
Maswali ni mengi, mazito si ya kudharaulika na wala hayahitaji majibu mepesi.
Tafiti zinatambulisha kuwa, kazi inayo fanywa na Boko Haram kwa sasa ni shughuli kivuli za CIA ambazo zinaratibiwa na ubalozi wa Marekani ndani ya Nigeria.
Kwa kipindi sasa CIA wamekuwa wakiendesha kambi za siri za mafunzo na kuwafunda dhana za wahabisim and new salafisim kwenye vichochoro vya mipaka ya Niger, Chad na Cameroon.
Mwisho wa siku, hakuna Jihad, hakuna Shariah, hakuna dola ya Kiislam wala Uislam. Mwisho wa siku kuna Marekani na maslahi yake, na sisi wengine wote ni wanasesere tu
Kwanini nchi ambayo hapo kabla iliweza kutatua matatizo yake yenyewe, bila ushirika wowote wa kimataifa, na hata kutatua matatizo ya nchi jirani kama Liberia leo imegeuzwa kuwa mwanasesere na kituko kwenye jukwaa la kimataifa?
Je wananchi milioni 160 wa Nigeria watasimama pembeni na kuwaachia Marekani waifanye nchi yao kama walivyo ifanya Libya, Iraq, Afghanistan, Syria, Egypti, Latini Amerika na kwengineko? Ambako kote huko rekodi ya taifa hili jeuri na lenye kiburi imekuwa ni chafu na mbaya kurekodiwa kwenye vitabu huru vya historia.
Huu ni mtihani kwa Wanigeria, na somo kwa Waafrika wote.

ungeipunguza kidogo ili watu waisome nakuielewa.
 
Wafrika huwa nawashangaa sana. Makosa wafanye wenyew wasingizie wengine.
Ww kuitwa Abdul au John ni makosa yako au ni makosa ya mwarabu au mzungu?
Km ni zao kwann hawapigani wenyew?
Nitakuwa wa mwisho kuamini hili.
Boko haramu imeanzishwa na wafrika wenyew hakuna mkono wa marekani hapo.
 
Back
Top Bottom