Bodi ya mikopo yatoa majina ya wanaodaiwa.

wengine tulishaanza kukatwa hiyo mikopo,japo nimesahau kila kitu,sijui nilisaini lini au nadaiwa sh ngapi.Nilipata barua toka kwa mwajiri kuwa wamepewa amri na sio ombi toka ofisi husika nianze kukatwa kila mwezi % fulani.Nimekubaliana na matokeo na naendelea kulipa taratibu ili nisipate presha zisizo na sababu.
 
Watanzania bwana sijui ni lini tutapanga mipango inayotekelezeka bila utata. Kwanza wakati wa mkopo sikumbuki kuona mkataba ya wanangu kuwa walitakiwa kukopeshwa kiasi gani na serikali na namna ya kulipa. Sana sana walikuwa anasema wamejaza form za mikopo. Ni wapi kila mdaiwa ataonyeshwa kumbukumbu ya kile alichokopeshwa na serikali yake? Sijui zoezi hili litafanikiwa kwa kiasi gani. Hebu tusubiri waende mahakamani. Huu ni upuuzi maana sidhani kama kuna ambaye atakataa kurejesha huo msaada wao kwa wananchi wakati mafisadi wanakula na hawarejeshi.

Hivi zile za EPA, DEEP GREEN, MEREMETA, RICHMOND, IPTL fake contracts, DOWANS malipo ya kijinga, you name all, si zinazidi hiyo mikopo wanayodai wazalendo!!?? Mbona hakuna mikakati ya kushughulikia haya, basi mnataka kukamua wazalendo ambao hata hiyo mikopo ilikuwa haitoshi na wazazi walikuwa wanagharimia pesa nyingi ili watoto wasome kwa mazingira mazuri? Give Wazalendo a break!!
 
Waajiri wanahusikaje hapa? Hii ni dalili kuwa Bodi haiwafahamu wadeni wake. Sasa mimi nimeajiri vijana waliomaliza Chuo Kikuu hivi karibuni. From nowhere, unakuja kunipa majukumu ya kukutafutia taarifa za hawa vijana ili kurahisisha ukusanyaji wa madeni yako. Kiutaratibu, siruhusiwi kutoa taarifa za staff wangu. Na mimi(mwajiri) ninanufaika vipi hapo kwa kufanya kazi ya kukusaidia kukusanya madeni? Ulipotoa mkopo, mlikubaliana nini kuhusu utaratibu wa malipo? Mimi ninadhani hii bodi ikubali ilichemsha. Waweke utaratibu mzuri(ikiwa ni pamoja na kufuta watumishi wote wa bodi kazi) waanze upya. Ikiwezekana, kampuni binafsi ipewe hiyo kazi ya kusimamia mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (e.g. PWC, Delloitte etc.). Yes, gharama itakuwa kubwa lakini ni bora kuliko kuendelea na hii bodi. In the long run, faida itaonekana. Watu watakopeshwa kwa utaratibu mzuri na watalipa madeni.
Hapa ni swala la sheria. Sheria iliyopitishwa na bunge inasemaje kama bodi itataka taarifa kwako na ukakataa au ukatoa taarifa ya uongo?
Je sheria inasema ukikataa kukata pesa hiyo na kuirejeza kwao itakuwaje?
Hapa ni sheria tu ndugu. Kama sheria iko blind kuhusiana na jambo hili wao wameliwa! Tafuta kwanza uisome kabla ujaingia matatizoni maana kutojua sheria hakukuondoi hatiani!
Utajiju!
 
tunailaumu serikali wakati mwingine pasipo kuangalia mimi na wewe tunafanya nini.
miaka 13 unakaa na deni, huoni ungelipa vijana kadhaa kijijini wangewezeshwa kupewa mkopo wakaenda chuo kikuu?
kwanza sijajua uwezo wa bodi ya mikopo kufuatilia madeni, kujua nani yuko wapi na amelipa shngapi hadi muda huo, nani yuko wapi na anadaiwa shngapi.
 
Msaada tutani??

1) Hivi hiyo sheria ya bodi ya mikopo ilianza lini??

2) Wakati bodi inaashizwa je sheria inasemaje kuhusu wakopaji na ulipaji??

3) Je cost sharing nayo ilkuwa ni mkopo??

3) Watu wa cost sharing wameinzwaje kwenye mkopo wa bodi na ni asilimia ngapi walikopeshwa au walipaswa kuchangia??
 
Hii kitu inachanganya sana,mie nilipokuwa admitted chuo, barua yangu ilisema nakuwa admitted under Government sponsorship,lakini nilikuja shangaa nilipoenda kufuata transcript niliambiwa kuna sehemu ya ada Bodi hawajalipa..nikastaajabu sana
 
Zakumi.. mkataba haueshimiwi kwa sababu ni mkataba:

a. Mkataba ni lazima uwe wa haki. Huwezi kuingia mkataba under false pretense or misleading of the other part or not in good faith.

b. Mkataba ni lazima uwe umekubaliwa na pande zote mbili. Mkataba unaoingiwa huku upande mmoja umeshikilia masharti ya pande zote mbili siyo mkataba ni kitanzi!

c. Bodi ya Mikopo haitoshi kusema kuwa "tunamdai x, y kiasi z".. ni lazima ioneshe kuwa ilimkopesha huyo x,y, kwa mkata alioingia tarehe fulani, na kwa masharti fulani na kwamba huyo mtu amedefault. Kusema ati mtu ajitolee kulipa mkopo ambao hakuna maandishi au ushahidi kuwa alichukua ni kuchezea watu akili. At least waoneshe kuwa hao wanaodai walichukua huo mkopo.

d. Ni hatari sana kwa wananchi kuitikia serikali "inaposema" bila kuhoji au kuibana serikali hiyo. Matokeo yake wao wenyewe wanafungulia ubabe (tyranny) huku wakikenua meno. Serikali ikisema tulikukopesha hiki kiasi na ulipe na wewe huna kumbukumbu na wao hawana kumbukumbu iweje ulipe? The burden of proof ya deni iko mikononi mwa bodi. Otherwise, watu hawatakiwi kulipa, period. Next time, waingie na mikataba yenye kuweze kusimamiwa.

e. Hii bodi tayari imeshafuja mabilioni ya fedha za Watanzania na sasa wanataka kuwabana watu kutokana na uzembe wao wenyewe. NI wao waliwalipa watu mara mbilimbili (double allocation) na ni wao walilipwa wanafunzi hewa (ghost students) na ni wao waliojimegea baadhi ya mikopo hiyo (kama nilivyoonesha almost three years ago with undisputable emperical evidence)..

Lakini kwa vile watu wamesikia "serikali imesema" basi watu wanatetemeka.

Mwanakijiji:

Tuchukulie mfano wako binafsi. Kwa miaka fulani umekuwa kwenye harakati ziwe za kuwahamsha watu kifikra au kutetea unachoona kuwa ni sahihi. Na kuna watu wanataka kukuharibia jina lako au kazi yako. Pamoja na hayo yote record zako ndizo zinazofanya watu kukupa sikio au lah. Hivyo kuwa na record isiyo na shaka ni kitu muhimu.

Maneno ya ufisadi yameanza kama miaka minne iliyopita. Na kuna wadaiwa kabla ya kuanza huo ufisadi walitakiwa kulipa. Mtu ambaye hajalipa kwa zaidi ya miaka 13, je miaka 9 kabla ya ufisadi kujulikana ufisadi alikuwa anafanya nini?

Fikra za mafisadi hazipitani sana na wale wanaokataa kulipa mikopo. Wote wanafikri kuwa rasimali ya umma ni free money.
 
Mwanakijiji:

Tuchukulie mfano wako binafsi. Kwa miaka fulani umekuwa kwenye harakati ziwe za kuwahamsha watu kifikra au kutetea unachoona kuwa ni sahihi. Na kuna watu wanataka kukuharibia jina lako au kazi yako. Pamoja na hayo yote record zako ndizo zinazofanya watu kukupa sikio au lah. Hivyo kuwa na record isiyo na shaka ni kitu muhimu.

Maneno ya ufisadi yameanza kama miaka minne iliyopita. Na kuna wadaiwa kabla ya kuanza huo ufisadi walitakiwa kulipa. Mtu ambaye hajalipa kwa zaidi ya miaka 13, je miaka 9 kabla ya ufisadi kujulikana ufisadi alikuwa anafanya nini?

Fikra za mafisadi hazipitani sana na wale wanaokataa kulipa mikopo. Wote wanafikri kuwa rasimali ya umma ni free money.


Wewe nawe jaribu kuelewa. Sisi wengine ni watu wa enzi za cost sharing. Na cost sharing siyo mkopo. Sasa kama huelewi maana ya cost sharing ina maana umesoma enzi za bodi hiyo ya mikopo. Wenzako wakati tunasoma hiyo bodi haikuwepo. Sasa kama hawakuwahi kunicontact ulitaka mimi nifanye nini. Kwa taarifa tu nimefanya serikalini kwa almost 1 year kabla sijaacha lakini hakuna aliyeniambia mambo ya mkopo wala nini. Sasa hapa kitu kikubwa ni kuhusu utaratibu wanaoutumia halafu ndiyo tuangaliye hiyo cost sharing iligeuka lini kuwa mikopo???
 
Student loan defaulters face tougher action, given 30 days to surrenderMost ReadMore News

PIUS RUGONZIBWA, 23rd December 2009 @ 21:01, Total Comments: 2, Hits: 278

THE Higher Education Students' Loans Board (HESLB) intends to forward names of about 2,972 students who secured loans in 1994/05 and 2004/05 but have not yet repaid to all banks in Tanzania in a move that might see them being barred from opening bank accounts or denied access to any credit facility.

The board also intends to forward the names of defiant beneficiaries to all foreign embassies in Tanzania, which might make it impossible for them to get visas for travelling abroad.

According to a notice issued by the board yesterday, defiant beneficiaries have been given 30 days to communicate with the board on repayment arrangements, failure of which legal actions will be taken against them. Apart from the legal actions, the defiant beneficiaries will be blacklisted from credit facilities and visas.

"Their names will be forwarded to all higher learning institutions in Tanzania, which might bar them from getting further studying opportunities.

"Their names will be forwarded to all employing institutions advertising jobs vacancies in print media, in lieu of barring them from getting job opportunities", reads part of the notice.

HESLB was established under Act No 9 of 2004. Among other things, the board is entrusted to recover all loans taken since July 1994 to facilitate disbursement to other applicants.

Section (19) (a) of the provisions of the Higher Education Students' Loans Board Act No 9 of 2004 and its amendments of 2007, stipulates that any loan beneficiary who without good course will fail to repay the loan shall be liable to civil proceedings.

Section 21 (1) (a) of the Act states that any person who does or omits to do any act or thing contrary to the provisions of the establishment Act, or the Regulations made in accordance therewith; commits an offence and is liable, on conviction to a fine not exceeding 7,000,000/- or imprisonment for term not less than twelve months or to both such fine and imprisonment".

"The board has on several occasions issued general reminder notices to loan beneficiaries and employers. However, some of the employers, parents, guardians, Guarantors and the students' loans beneficiaries whose names appear herein have not yet heeded to those notices to date," reads the notice in part.

According to the notice, all parents, guardians or a guarantor of the loan beneficiaries should inform the board of the current address and the occupation of the loan beneficiary and the name, postal and physical address of the current employer of the loan beneficiary whom they guaranteed.

"In case a loan beneficiary whose name appears herein is now a deceased one, the parents and or relatives, should inform the Board in respect of his/her death," the board points outs.
Hawa ni Daily News. Jamani hebu tulipeni madeni haya si kwasababu ya kutishiwa bali uzalendo ili na wengine wasome
 
hili deni huwa linanikera kweli kweli kwanza lina ubinafsi wengine eti hawatalipa kabisa kutokana na miaka waliyo soma.
kinachonisikitisha zaidi ni kwamba serikali haiangalii ni kwa kiasi gani wasomi wake wanachangia pato la taifa
wafanyakazi wamekuwa ndio walipa kodi kubwa kwa kuwa wao hawana pa kukwepa fikilia mtu huyo analipa kodi kila mwezi kati ya shs 50,000 na 450,000 kwa mwezi hivi kwa nini serikali isiamue sehemu ya hela inayopata iende moja kwa moja bodi kuliko kuendelea kummumiza mtu anayesoma kwa ajili ya kuitumikia nchi yake
samahani siwezi kueleza vizuri imefika muda sielewi manufaa yake sana ya makusanyo haya ikiwa watoto wa masikini wanapata tabu kupata huo mkopo kwa ajili ya urasimu
 
Nianze kusema Dawa ya deni ni kulipa ni neno zuri sana ambalo hata Rais wetu mstaafu Ben Mkapa alikuwa analitumia sana.

Tatizo linakuja nii iitwayo Bodi ya hiyo mikopo..sio siri mimi ni mmoja wa watu ambao naichukia sana,maana haiko makini katika utendaji wa kazi yake.
Bodi ya mikopo imejaa wababaishaji sana inasema inatumia mfumo wa kisasa wa komputa katika kutambua uhitaji wa mwanafuzi hilo si kweli na kuthibitisha hilo kuna watu wanaenda pale na madaraja yao yanabadilika muda huo huo,huo si wizi na uongo kabisa.


"Database" yao ni mbovu na nina pata hata mashaka na wataalamu wa Teknohama walionao hapo maana kuna vituko vingi sana ambavyo inaendelea na haijulikani ni lini labda vitaisha..hii ni aibu kwa bodi hii ambayo inategemewa na wengi .


mwisho kama wewe unaona ni kweli unadaiwa na deni lako liko sahihi n bora ukalipa mapema tu ili na wengine wapate hiyo pesa ya kusoma kwani kila kukicha idadi ya wahitaji wa hiyo mikopo inazidi kuongezeka kwa kasi.
asanteni.
 
Lipeni deni.

Siyo kwa vile serikali imesema. Ni wajibu wako kulipa. Hakuna cha wakati wa cost-sharing wala sijui wakati wa bodi ya mikopo. Ulisaini mkataba wa mkopo na ukaahidi kuanza kulipa miezi 12 baada ya kumaliza masomo. Sasa kelele za nini?

Na huyo anayesema mbona wagonjwa hawadaiwi kiasi kinacholipiwa na serikali anatakiwa aonyeshe mkataba wa mkopo kati ya mgonjwa na serikali ili nao wadaiwe. Kama kweli upo. Vinginevyo acheni visingizio. Huu ndiyo mwanzo wa fikra za kifisadi na wizi. Eboo.
 
Msaada tutani??

1) Hivi hiyo sheria ya bodi ya mikopo ilianza lini??

2) Wakati bodi inaashizwa je sheria inasemaje kuhusu wakopaji na ulipaji??

3) Je cost sharing nayo ilkuwa ni mkopo??

3) Watu wa cost sharing wameinzwaje kwenye mkopo wa bodi na ni asilimia ngapi walikopeshwa au walipaswa kuchangia??

Mzee kama unadaiwa kalipe na sisi tusome chuo kikiuu....
 
Wewe nawe jaribu kuelewa. Sisi wengine ni watu wa enzi za cost sharing. Na cost sharing siyo mkopo. Sasa kama huelewi maana ya cost sharing ina maana umesoma enzi za bodi hiyo ya mikopo. Wenzako wakati tunasoma hiyo bodi haikuwepo. Sasa kama hawakuwahi kunicontact ulitaka mimi nifanye nini. Kwa taarifa tu nimefanya serikalini kwa almost 1 year kabla sijaacha lakini hakuna aliyeniambia mambo ya mkopo wala nini. Sasa hapa kitu kikubwa ni kuhusu utaratibu wanaoutumia halafu ndiyo tuangaliye hiyo cost sharing iligeuka lini kuwa mikopo???

Unadaiwa ua hudaiwi? Ulisomeshwa na Serikali au Hapana?
 
Ukigoma kulipa wewe huna tofauti na Fisadi. Nyie mnafikiri kisa ni pesa ya serikali kwa hiyo muwe mnaitafuna tu. Tutafika wapi sasa. Ulipewa mkopo umekusaidia umepata ajira nje ya nchi. Leo unaleta mizinguo. Bila kupewa hiyo pesa mngekuwa wapi leo? Ebu kuweni na shukrani....
 
Moderator, Naomba hii ikae kwa muda ili tupate some infomation kutoka kwa walio nchini.
Nasikia Bodui ya mikopo leo imetoa majina ya wanaodaiwa na wametowa siku 30 otherwise wanakufikisha kotini.
Kuna wengine kama sisi ambao tulimaliza zaidi ya miaka 13 iliyopita nasikia kuwa majina yetu yapo.
I am not sure if I am wrong, kwavile wanaonekana wana details zetu kwa nini hawakuamua kutuandikia barua kwenye permanent address zetu kutupa hii taarifa. Au wana assume wote tuna access na magazeti. Toka ni graduate hiyo miaka ya 90 sikuwahi kusikia anything kuhusu huo mkopo na namna ya kuulipa until today niliposikia kuwa jina langu limetoka kenye the Gurdian ya leo.
Mwenye info naomba atuletee hapa, sitaki nijekuwa arrested airport nikirudi likizo.
Ok mkuu hii hapa
 

Attachments

  • HESLB_DEFAULTERS_BATCH_1.pdf
    230.2 KB · Views: 64
Back
Top Bottom