Waraka wa watoto wa mafukara kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini (heslb)

KennedyMmari

JF-Expert Member
Dec 12, 2012
979
183
Ndugu zangu maofisa,waasibu, mameneja na wakurugenzi wa bodi ya mikopo ya Elimu ya juu nchini Tanzania (HESLB), poleni sana kwa kazi nzito mnayoifanya maana nimeota ndoto kuwa mara baada ya timu ya taifa kushindwa kufanya vizuri mmeazimia kulisaidia taifa katika kitengo hicho na ndoto inaonesha kuwa wiki jana tu mlikuwa Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abed kusakata kabumbu, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.

Lakini naomba ieleweke wazi hapa kuwa tatizo kwetu sisi watoto wa mafukara si kutaka kuhoji
juu ya jitihada zenu za kukuza na kuendeleza vipaji vyenu au juu ya nia yenu njema ya kukuza na kuendeleza soka nchini ili siku moja Tanzania iweze kushiriki walau kombe la dunia hata kwa nafasi ya viti maalum, lakini maswali yetu sisi tusojua ladha ya utamu wa maisha ni kuwa:-

Je wakati mkipanda mabasi au hata ndege kwenda Arusha kwa kutumia kodi za Baba na Mama zetu wauza maparachichi kule Santilya Umalila Mbeya mlikuwa mnajua kuwa vyuoni kuna watoto wa mafukara wa m
waka wa kwanza ambao mpaka sasa tunaishi vyuoni kama kinda aliyekosa mama kwani tumekosa mahali pa kulala na hata chakula cha uhakika huku ikikumbukwa wazi kuwa wengi wetu.

Tulitoka kwetu Tandahimba Mtwara na kwingineko tukiwa na matumaini makubwa kuwa tungepata pesa ya kujikimu kutoka serikalini kwani hata kile tunachosoma kwa sasa tulikichagua kwa kuwa ndio kilikuwa na uwezekano wa kutufanya kupata mkopo ukilinganisha na kile kilichokuwa ndoto zetu.

Lakini pamoja na haya yote mlitunyima hicho mnachokiita mkopo na mkatutaka kusubiri majina ya banchi la kumi ambayo mpaka ninapoandika waraka huu bado hayajatolewa na ndio kwanza ninyi mpo Arusha kuonesha vipaji ambavyo sisi hatukuviona kwenu hapo awali.

Naam labda ni kupitiwa tuu na kujisahau kutokana na kiyoyozi cha ofisini kwenu magari ya kifahari na maisha bora ya familia zenu lakini naomba kuhoji, kwani mlipita njia gani kusafiri mpaka Arusha? njia ambayo hamkuona hata kijiji kimoja cha Tanzania na kuona huko mnapo paita bushi ambapo kiuhaalisia ndipo tulipo toka sisi watoto wa mafukara tulioomba mkopo kwa kutumia pesa za mahindi ya kuikimu.

Familia ambayo bibi yangu Shogoo aliamua kuyauzaa ili mimi nikanunue fomu yenu ya shilingi 30,000, nikahangaika sana kupata kibali cha kifo cha baba na mama yangu lakini nakumbuka nilishirikiana na rafiki yangu Tabu ambaye alikuwa amefiwa na Baba yake na kubakiwa na mama yake ambaye kwa sasa ni mgonjwa sana lakini bado mkanipa mimi asilimia 0% na yeye mmempaa TSH3,800 katika 1800,000 anayopaswa kulipa kwa mwaka mmoja wa masomo.

Tulipohoji juu ya kukata rufaa ili tuongezewe pesa mkatujibu kuwa tusubiri mpaka mtakapo kamilisha taratibu lakini kumbe taratibu zenyewe tunazosubiri mpaka sasa ni ninyi kurudi kutoka michezoni?

Samahani sana naomba kuuliza wakuu mlipofika Arusha hakuna hata mmoja wenu aliyezinduka na kukumbuka kuwa kuna watoto wa wakulima wa ndizi kutoka Matombo Morogoro Vijijini na sehemu kama hizo nchini ambao wapo mwaka wa pili na watatu sasa lakini waliomba mkopo miaka ya hapo nyuma na mliwanyima wakasoma kwa kuombaomba kama wakimbizi ndani ya nchi yetu na kwa mwaka wa masomo 2015/2016 imetugharimu TSH 30,000 nyingine tuliyokopa kwa mzee Msemwa na kuweka rehani kijumba chetu cha mbavu za mbwa kilichopo kijijini ili kuweza kuomba upya mkopo.

Na mpaka sasa mmetuambia tusubiri ili muweze kutupa mkopo katika kile mnachokiita banchi ya kumi lakini cha kusikitisha kumbe sisi tunasubiri kwa matumaini lakini ninyi mpo Arusha kwenye michezo ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

MASWALI KUNTU YA KUJIULIZA HAPA NI JE?

Kulikuwa na umuhimu gani wa kufanya bonanza la michezo kwa kipindi hiki ambacho majina ya wanafunzi wanaonufaika na mkopo kwa mwaka wa kwanza yamechelewa kutolewa ikilinganishwa na miaka mingine ya masomo na mpaka sasa mchakato wa majina yao bado haujakamilika?

Kama michezo ni starehe, furaha na kufahamiana kulikuwa na umuhimu gani wa kuyafanya hayo katika kipindi hiki ambacho maisha ya maelfu ya watanzania kubaki ama kuondoka vyuoni yapo katika mikono yenu iliyo na mamlakaa juu ya hatima ya watanzania hawa?

MWISHO.

Sisi kama watoto wa mafukara ambao kimsingi ndio walipa kodi wa Tanzania tunaomba kupewa majibu ya wazi katika vyombo vyaa habari kuwa.

NI KWANINI MSICHUKULIWE HATUA KALI ZA KIUTENDAJI HASA KATIKA ZAMA HIZI ZA ?HAPA KAZI TUU?

PILI NAOMBA MUELEZE WAZI NI KWANINI MUHESHIMIWA RAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI ASIFANYE ZIARA YA GHAFLA KATIKA OFISI ZENU KESHO ASUBUHI?

?PAMBANA NA HOJA USIPAMBANE NA MTOA HOJA?

SHITINDI VENANCE ROLANDI, MWENYEKITI WA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO TANZANIA. 0759704444.
 
Mbona nilisikia wanavyuo wote wamepewa mikopo? Au ulikuwa ni usanii wa Magufuli tu kupata umaarufu?
 
Mbona nilisikia wanavyuo wote wamepewa mikopo? Au ulikuwa ni usanii wa Magufuli tu kupata umaarufu?

Usanii mtupu kiongozi , chuo cha ada million 2.5 unapewa unapewa tuition fee ya sh 3800 sasa hapo wamekusaidia nini kwa mtoto toka nanjilinji??
 
Hawa jamaa ni wakutimua wote pale ofisini , kwa siku hufika watu zaidi ya 250 kwenye ofisi zao lakini kwenye help desk wapo watu wawili wanaohudumia kiasi huudumia watu 100 tu na wengine mtaambiwa njooni kesho kumbe wao wameenda kurukaruka huko Arusha.Hivi kulikua kuna ulazima gani wao kuondoka Arusha muda huu ambao wahitaji wa huduma ni wengi na wanahitaji msaada wa haraka?
 
Mbona nilisikia wanavyuo wote wamepewa mikopo? Au ulikuwa ni usanii wa Magufuli tu kupata umaarufu?
Magufuli anajipa promo tu lakini naye ni walewale tu. Suala LA mikopo linagusa watanzania wengi maskini lakini nashangaa hatilii maanani. Namkumbuka mzee wangu wa ElimuElimu Elimu Hawa wengine mbwembwe tu
 
UDSM NAO PIA WARUDISHE PESA ZA WANAFUNZI WA DIPLOMA WALOWAKATAA ILI PESA HIZO ZIPELEKWE KWENYE VYUO VIPYA WALIVYOPATA

heslb WATU WATASHINDWA SOMA KABISA

KUNA NDUGU YANGU YUPO MZUMBE YE KAFIWA MAMA NA BABA KAKOSA MKOPO WHY??
 
Mdogo wangu tayari amesharudi Nyumbani Tabora vijijini,kafuatilia mpaka kachoka hakuna dalili za kupata mkopo,Nadhani yale yalikuwa maigizo tu kusema Kila mwanafunzi aliyechuoni atapata mkopo.
 
Usanii mtupu kiongozi , chuo cha ada million 2.5 unapewa unapewa tuition fee ya sh 3800 sasa hapo wamekusaidia nini kwa mtoto toka nanjilinji??
Nimeiona hii, hapana, sasa huu ni utani. Hapa Mheshimiwa Magufuli, kuna shida. katika vitu vinavyokera wazazi ni hili la ada na pesa ya matumizi. Kwa hili Mungu atatuhukumu. 3800 = 1,300,00, how?
 
UKAWA would maka a difference.Tuliahidi elimu bure mpaka chuo kikiuu, hawa CCM hili hawaliwezi wanasubiri kujipanga kwa miaka mingine mitano ndio waje kuiga hii sera yetu kama walivyoiga sasa sera ya elimu bure.

Watanzania wangekuwa ni watu wenye upeo, CCM isingerudi madarakani wala kupata idadi ya wabunge walioipata.

CCM ndio imechangia umasikini wa nchii hii na ndio imetufikisha hapa.
 
Nimeiona hii, hapana, sasa huu ni utani. Hapa Mheshimiwa Magufuli, kuna shida. katika vitu vinavyokera wazazi ni hili la ada na pesa ya matumizi. Kwa hili Mungu atatuhukumu. 3800 = 1,300,00, how?

Asilimia kubwa ya waliopata mkopo tuition fee ni 0 tena sasa hivi hawaandiki asilimia bali direct sh 3800 bila kupepesa macho.
 
Mnang'ang'ana sana kwenda vyuo vikuu kwa ajili ya sifa tu.Unıversıty wanatakiwa kwenda Div one na Diploma holders.Wengne twende VETA na vyuo vingne vya kati kwanı huko ndo wanatengenezwa wazalishaji.Ni kosa kubwa kumpeleka Dıv 3 university.
 
Nilivyokuwa chuo hatukuwah kupewa mkopo on time hata mara moja ... Licha ya kuwa na mkopo maisha yalikuwa magumu sana maana ulikuwa ukipewa mkopo unakuta una madeni chungu nzima... Nawaonea huruma zaidi wenzangu ambao hamna mkopo yani maisha ya chuo kama unatokea hizi familia zetu n shida Sana
 
hapa kuna hoja suala la elimu si la kupuuza endapo utakuwa na wanamichezo bora bila elimu atakwama ,barabara nzuri bila elimu watazifuja tunaona ,hawa watoto wa wakulima wapewe mikopo stahiki shule iendelee wasikwamishwe,
 
How Can UPoor Help A Poor If Ur One Of Them?. Fool! You Need To Get Rich. So That Win - Win. Na Umaskini Wenu Ungepiga Kura Kwa Laigwan, He's Filthy Rich. Elimu Bure Mpaka Mwisho Wa Kusoma.Rip Wat You Saw. Punk
 
Back
Top Bottom