Wanafunzi vyuo vikuu kutumbua jipu bodi ya mikopo

fieldmashal

Member
Nov 22, 2015
78
3
JIPU LA BODI YA MIKOPO LIMEWASHINDA NINYI LAKINI NAWAHAKIKISHIA KUWA SISI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TUTALITUMBUA NA KULIKAMUA WENYEWE.

na SHITINDI VENANCE

Hii bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inapaswa kubadilishwa jina na kuwa bodi ya pensheni kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutokana na ukweli kuwa bodi hii imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake mpaka pale panapokuwa na mashinikizo mazito kutoka kwa wanafunzi.

Hali hii inathibitishwa na ukweli kwamba mpaka sasa ninapoandika waraka huu bado kunawanafunzi ambao ni wanufaika wa mikopo lakini mpaka sasa hawajapewa fedha zao pasipokuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo.

Chakisikitisha zaidi na kinachoonesha kukosa huruma kwa watu hawa ni kuwa mapaka sasa kuna baadhi ya walemavu, watoto yatima na wale wenye mzazi mmoja ambao kwa misingi ya vipaumbele ndio watu ambao wanakipaumbele zaidi chakupata mikopo lakini hawajapata mikopo mpaka sasa na wengine wanazungushwa kama pia kila uchao.

Lakini pia tunayo idadi kubwa ya wanafunzi ambao mpaka sasa hawajui hatima yao ya mikopo kwani majina yao hayajatolewa mpaka kufikia kipindi hiki ambacho vyuo vingi vimeshaanza kufanya mitihani ya awali ya majaribio kitu kinachowafanya wanafunzi hawa kukosa haki zao za kufanya mitihani kutokana na ukweli kwamba bado hawajasajiliwa katika vyuo husika na kiutaratibu tuu ni kuwa huwezi kufanya mtihani bila kujisajili na usajili haufanyiki bila kulipa ada na ada hailipwi bila kujua unapewa mkopo asilimia ngapi.

kwa hali hii watoto wa mafukara tumeonekana kushindwa kujikim na kulipa ada ya chuo hivyo wengi wetu wameshaanza kurudi majumbani kwao kwenda kuuendeleza umasikini uliokithili katika familia zao na kuachana na elimu ya juu ambayo huenda ingeweza kupunguza kama si kumaliza mnyororo wa umasikini katika familia hizi.

yote haya yanatokea kutokana tuu na utendaji mmbovu wa bodi ya mikopo kwani watendaji wa bodi hii wamekuwa wakitumia muda mwingi zaidi kujiandaa na mashindano ya soka na hata kushiriki mashindano hayo zaidi ya kutekeleza majukumu yao jambo ambalo linapelekea wanafunzi kushindwa kupata mikopo na hata wanaopata basi hawapati pesa hizo kwa wakati muafaka.

Pamoja na uzembe huu lakini pia wafanyakazi wa bodi hii ndio wafanyakazi wenye rugha mbovu na zakukatisha tamaa kuliko taasisis yoyote nchini na hata wameweza kukiuka kwa makusudi kauli iliyotolewa na naibu waziri wa wizara ya Elimu Eng siku ya tarehe 14/12/2015 kwani aliwataka kutatia matatizo ya wanafunzi nchini ndani ya masaa 24 lakini mpaka ninapoandaa waraka huu hakuna kilichofanyika .

Kwakuliona na kulitambua hili wanafunzi wa vyuo vikuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mikopo SHITINDI VENANCE tuliungana na kwenda kuhoji utekelezaji wa kauli hii Bodi ya mikopo mnamo tarehe 16/12/2015 lakini baada ya kukosa majibu tulifika mpaka ofisi za Wizara ya Elimu na kupeleka hoja zetu zote lakini pia tulishapeleka malalamiko yetu kwa Ofisi ya Waziri mkuu kwa maandishi mnamo tarehe 13/12/2015 na mpaka sasa hatuja pata majibu yoyote,

Kinachoonekana hapa ni kuwa jipu la bodi ya mkopo limekosa mkamuaji maana Naibu waziri limeshamshinda hivyo kama wanafunzi wa vyuo vikuu nchini hatuwezi kukaa tunalialia tuu tukingoja aliyeshiba kuja kutupa chakula.

Mpaka sasa tumebakiwa na wiki tatu tuu za kuanza kudai boom la pili kwa mwaka huu wa masomo na kwa dalili zinavyoonesha kuwa pesa hizi zitacheleweshwa sana kwani mpaka sasa hakuna maandalizi yoyote yanayoendelea katika kuhakikisha wanafunzi wanazipata pesa hizi kwa wakati kama ilivyo kawaida ya bodi hii kuchelewesha pesa za kujikimu mara kwa mara

MAAMUZI MAGUMU
NAOMBA WANAFUNZI WA VYUO VYOTE NCHINI WALIO NA WASIO NA MKOPO MJIANDAE KWA KUFANYA MASHINIKIZO MAKUBWA YASIYO NA KIKOMO NCHI NZIMA MPAKA PALE SERIKALI ITAKAPOAMUA KUITAZAMA UPYA BODI YA MKOPO NA KUUFUMUA MFUMO WAKE MBOVU.
UTARATIBU WA MASHINIKIZO HAYO UTATOLEWA NA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU NCHINI HIVI KARIBUNI.

KUUTUMA WARAKA HUU KWA WANAFUNZI WENGINE NI MCHANGO MUHIMU KATIKA HARAKATI HIZI. SHARE

SHITINDI VENANCE
0759704444
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO YAELIM YA JUU TAIFA.
 
Ni lazima tuungane sote kuishinikiza serikali kama VIP wavifunge vyuo tuu turudi zetu nyumbani
 
Kila siku Tanzania kwa nini!!!? Juzijuzi tu nilisikia wanafunzi wote eti wamepata mikopo kumbe ni uongo kabisa, naomba serekali imulike bodi ya mikopo kwa jicho la tatu (viongozi kusema uongo ni aibu kubwa kwa Taifa)
 
leo baadhi ya wanafunzi wa udom wameshindwa kusoma kabisa hawana pesa ya chakula wameshakopa sana hapa serikali inatakiwa iwe makini sana na maisha ya wanafunzi chuoni
 
Tatizo la bodi ya mikopo ni serikali yenyewe, mara nyingi serikali haipeleki pesa kwa wakati na hata wakipeleka ni makaratasi tu yenye data

za pesa zipelekwe. Bodi kama bodi hawana chanzo chochote cha pesa. fikiria serikali haijeweka mfumo mzuri kuwezesha bodi kukusanya

kile walichokopesha.Maguful ashughulike na hazina maana pale ndo kwenye matatizo
 
Tatizo la bodi ya mikopo ni serikali yenyewe, mara nyingi serikali haipeleki pesa kwa wakati na hata wakipeleka ni makaratasi tu yenye data

za pesa zipelekwe. Bodi kama bodi hawana chanzo chochote cha pesa. fikiria serikali haijeweka mfumo mzuri kuwezesha bodi kukusanya

kile walichokopesha.Maguful ashughulike na hazina maana pale ndo kwenye matatizo

Wewe kweli naona hujawahi kwenda board, hawa watumishi wa bodi wanachangia sehemu kubwa sana kwa wanafunzi kuteseka vyuoni.
 
Bodi ya mikopo wanafanya kazi kwa mazoea mfano Mimi mkopo wangu ulienda kwingine na chuo nilichochaguliwa lakini kuuhamisha kuuleta nilipo wanafanya swala la kukaa siku 60 sasa jambo la kujiuliza kuuhamisha mkopo kuuupeleka alipo ni swala LA kukaaa siku 60 wasomi nawauliza?Mimi naweza Sema si kweli kuna kitu nawaomba mamlaka husika mfatilie hilo kuuhamisha mkopo siku 60 ,sio fair unategemea huyu mtu aishije?kuweni makini fanyeni kazi .
 
Kuna utengano wa kichwa cha habari na ulichoandika. Mimi nilidhani kuwa ninyi wanafunzi wenyewe (kama kichwa kinavyosema) mtawafukuza kazi hao wakuu wa bodi ya mikopo kumbe mtatoa mashinikizo kwa serikali ili ifanye hivyo. Sasa ikiwa mtaishinikiza serikali iwatimue hao viongozi wa bodi ya mikopo ni nani hapo kati yenu na serikali atakuwa ametumbua jipu? kwa mtizamo wangu hapo ni serikali.Ikiwa mwanafunzi wa ngazi ya chuo kikuu huwezi kuandika hoja rahisi iliyonyooka unatujuza sisi great thinkers kuwa kuna hitilafu katika mfumo wetu wa elimu.
 
dah!,,, ni hatua nzuri inayokusudiwa,,, uyo jamaa namkubali sana tulikuwa nae pale loan board last wk, aliwaeleza vzur sana waandish wa habar,, tukatoka nae kuelekea wizaran,, naomben tuungane kwa pamoja,, roho inauma kuona mwana chuo nashndia miogo ya mia3 asubh,mia3 mchana na jion yan bila ushaur wenu wakuu nilkata tamaa KABISA,, mfumo wa nchi yetu hauthamini ELIMU kwa vtendo ni porojo tu,,,
 
dah!,,, ni hatua nzuri inayokusudiwa,,, uyo jamaa namkubali sana tulikuwa nae pale loan board last wk, aliwaeleza vzur sana waandish wa habar,, tukatoka nae kuelekea wizaran,, naomben tuungane kwa pamoja,, roho inauma kuona mwana chuo nashndia miogo ya mia3 asubh,mia3 mchana na jion yan bila ushaur wenu wakuu nilkata tamaa KABISA,, mfumo wa nchi yetu hauthamini ELIMU kwa vtendo ni porojo tu,,,

Hizi porojo ndo tunataka tuzitafutie modarity nzuri ya kuziondoa, within this forum we have different people with different carriers and professionals so let's use this as stepping stone to solve our problems your's fieldmashal udom (education).
 
Hizi porojo ndo tunataka tuzitafutie modarity nzuri ya kuziondoa, within this forum we have different people with different carriers and professionals so let's use this as stepping stone to solve our problems your's fieldmashal udom (education).

aah mkuu na mimi npo udom coed first year ni muhanga wa tatizo hili, npo block T ni PM tupeane maujanja ya kupigana na hi hali!
 
Hizi porojo ndo tunataka tuzitafutie modarity nzuri ya kuziondoa, within this forum we have different people with different carriers and professionals so let's use this as stepping stone to solve our problems your's fieldmashal udom (education).

ndy mkuu,, acha tanzania tuioneshe upande wa pili wa shiling "LETS ALL OF US BELIEVE THAT WE CAN DO IT"
 
Back
Top Bottom