Zakumi.. mkataba haueshimiwi kwa sababu ni mkataba:
a. Mkataba ni lazima uwe wa haki. Huwezi kuingia mkataba under false pretense or misleading of the other part or not in good faith.
b. Mkataba ni lazima uwe umekubaliwa na pande zote mbili. Mkataba unaoingiwa huku upande mmoja umeshikilia masharti ya pande zote mbili siyo mkataba ni kitanzi!
c. Bodi ya Mikopo haitoshi kusema kuwa "tunamdai x, y kiasi z".. ni lazima ioneshe kuwa ilimkopesha huyo x,y, kwa mkata alioingia tarehe fulani, na kwa masharti fulani na kwamba huyo mtu amedefault. Kusema ati mtu ajitolee kulipa mkopo ambao hakuna maandishi au ushahidi kuwa alichukua ni kuchezea watu akili. At least waoneshe kuwa hao wanaodai walichukua huo mkopo.
d. Ni hatari sana kwa wananchi kuitikia serikali "inaposema" bila kuhoji au kuibana serikali hiyo. Matokeo yake wao wenyewe wanafungulia ubabe (tyranny) huku wakikenua meno. Serikali ikisema tulikukopesha hiki kiasi na ulipe na wewe huna kumbukumbu na wao hawana kumbukumbu iweje ulipe? The burden of proof ya deni iko mikononi mwa bodi. Otherwise, watu hawatakiwi kulipa, period. Next time, waingie na mikataba yenye kuweze kusimamiwa.
e. Hii bodi tayari imeshafuja mabilioni ya fedha za Watanzania na sasa wanataka kuwabana watu kutokana na uzembe wao wenyewe. NI wao waliwalipa watu mara mbilimbili (double allocation) na ni wao walilipwa wanafunzi hewa (ghost students) na ni wao waliojimegea baadhi ya mikopo hiyo (kama nilivyoonesha almost three years ago with undisputable emperical evidence)..
Lakini kwa vile watu wamesikia "serikali imesema" basi watu wanatetemeka.