Bodi ya mikopo yatoa majina ya wanaodaiwa.

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,332
12,898
Moderator, Naomba hii ikae kwa muda ili tupate some infomation kutoka kwa walio nchini.

Nasikia Bodui ya mikopo leo imetoa majina ya wanaodaiwa na wametowa siku 30 otherwise wanakufikisha kotini.

Kuna wengine kama sisi ambao tulimaliza zaidi ya miaka 13 iliyopita nasikia kuwa majina yetu yapo.

I am not sure if I am wrong, kwavile wanaonekana wana details zetu kwa nini hawakuamua kutuandikia barua kwenye permanent address zetu kutupa hii taarifa. Au wana assume wote tuna access na magazeti. Toka ni graduate hiyo miaka ya 90 sikuwahi kusikia anything kuhusu huo mkopo na namna ya kuulipa until today niliposikia kuwa jina langu limetoka kenye the Gurdian ya leo.

Mwenye info naomba atuletee hapa, sitaki nijekuwa arrested airport nikirudi likizo.
 
Binafsi siko nchini lakini nilianza kukatwa mkopo huo mwaka 2007 kwenye mshahara wangu ambapo nalipa TZS 25,000 kila mwezi na denni ni TZS 5,000,000. Ukiangalia deni ni kubwa kuliko pesa waliyo nikopesha, nilikwenda kuwauliza bodi wakadai watashughulikia lakini bado nakatwa kiwango hicho hadi leo.

Mbaya zaidi baadhi ya classmates wangu tuliokuwa darasa moja hawadaiwi na wote tulipewa mkopo huo, wengine wanandaiwa TZS 2,000,000. Kwa hiyo bodi hawana data za wakopaji walicho fanya ni kukadiria madeni.

Sasa mkuu labda tusubiri walioko TZ kwa sasa watupe details.
 
Kwanza hiyo mikopo wakati inaanza tulilazimishwa kuomba kwa kujaza form. Kwa kumbukumbu yangu sikuwahi kupata barua ya kusema nimepata mkopo na ni kiasi gani. Sasa kama bodi imeishiwa pesa na wanataka kuokoteza kila mahali then watumie utaratibu mzuri badala ya kuzuka na kutoa majina ya watu magazetini. Hawajui kuwa wanaweza kuchafua majina ya watu kwa utaratibu huu???
 
Wamefulia tu hao watoto wa watu wanateseka huko vyuoni.Wametoa majina,Mwanafunzi anaandikiwa amepata mkopo asilimia mia,mzazi anafurahi lakini mpaka leo baadhi hawajapewa hizo pesa.Wadogo zetu wamegeuka machangu ili kuweza kujikimu.

website yao pia imekufa sasa...

Km wapo humu majina hayo watuwekee kwenye website.Ili tuwavae mapema iwapo madeni ni ya uongo.Najua hawana data,maana kipindi tunasoma,kuna watu walikuwa wakiwekewa mikopa hadi mara 3 ya kiwango halisi.Hapo watadai zote au kiwango halisi?
 
Binafsi siko nchini lakini nilianza kukatwa mkopo huo mwaka 2007 kwenye mshahara wangu ambapo nalipa TZS 25,000 kila mwezi na denni ni TZS 5,000,000. Ukiangalia deni ni kubwa kuliko pesa waliyo nikopesha, nilikwenda kuwauliza bodi wakadai watashughulikia lakini bado nakatwa kiwango hicho hadi leo.

Mbaya zaidi baadhi ya classmates wangu tuliokuwa darasa moja hawadaiwi na wote tulipewa mkopo huo, wengine wanandaiwa TZS 2,000,000. Kwa hiyo bodi hawana data za wakopaji walicho fanya ni kukadiria madeni.

Sasa mkuu labda tusubiri walioko TZ kwa sasa watupe details.
Mr. Zero hizi taarifa umezisikia wapi?
Binafsi tangu mwaka jana nimewaandikia hawa jamaa nilipe mkopo hadi leo hawajawahi kuniletea statement niliyowaomba.
Kiekweli data hawajazioganaizi vema.
 
moderator, naomba hii ikae kwa muda ili tupate some infomation kutoka kwa walio nchini.

nasikia bodui ya mikopo leo imetoa majina ya wanaodaiwa na wametowa siku 30 otherwise wanakufikisha kotini.

kuna wengine kama sisi ambao tulimaliza zaidi ya miaka 13 iliyopita nasikia kuwa majina yetu yapo.

mwenye info naomba atuletee hapa, sitaki nijekuwa arrested airport nikirudi likizo.
hebu njoeni mlipe madeni bana, watanzania wengine nao wanahitaji kusoma, ebo.
 
Mje mlipe.
Uzalendo ni kulipa hilo deni.
Sio kukazania ufisadi,ufisadi
wakati na huo ni ufisadi.
 
hebu njoeni mlipe madeni bana, watanzania wengine nao wanahitaji kusoma, ebo.

Kwani tumekataa kulipa. Watuambie ni kiasi gani then tutalipa?? Si wa kuwaamini hawa, ni mafisadi. Walikuwa wapi kuweka utaratibu wa kueleweka. Inaelekea umememaliza chuo miaka ya 2000 ndiyo maana huwezi kuelewa. Wengine wakati tunaanza mikopo haikuwepo, tulibambikiziwa kiaina aina tu. Hivyo hatujui hata kiasi tulichokopeshwa, nafikiri hata wao hawajui.
 
Mje mlipe.
Uzalendo ni kulipa hilo deni.
Sio kukazania ufisadi,ufisadi
wakati na huo ni ufisadi.

Mawazo yako hayo. Wakati tunaanza hiyo mikopo haikuwepo ilikuja katikati, na wala sikuwahi kupata barua kunipa mkopo wala barua ya kunitaarifu ni kiasi gani nadaiwa. sasa ulitaka nilipeje. Hiyo bodi ya mikopo haikuwepo!!!
 
Au labda Mkuu jamaa washachoka na kashfa zako unazowatupia, maana unasema we hata ujui wanakudai kiasi gani, na wala ujawahi pata barua toka kwao leo waaamke asubuhi na Jina lako kwenye gazeti.

Hii hatari Mkuu.
 
Kwa wale mlimaliza miaka 12 iliyopita na serkali ilikaa kimya huo mkataba ia time barred .hapa wakienda mahakamani ni objection mapemaa
 
Kwa wale mlimaliza miaka 12 iliyopita na serkali ilikaa kimya huo mkataba ia time barred .hapa wakienda mahakamani ni objection mapemaa
Hebu tuache hadithi na wengine wasome. Nadhani ni vyema kila mtu ajipeleke ili alipe. Turudishe hizo pesa jamani na wengine wasome otherwise ni ubinafsi
 
Mawazo yako hayo. Wakati tunaanza hiyo mikopo haikuwepo ilikuja katikati, na wala sikuwahi kupata barua kunipa mkopo wala barua ya kunitaarifu ni kiasi gani nadaiwa. sasa ulitaka nilipeje. Hiyo bodi ya mikopo haikuwepo!!!

lipeni na wengine wasome
 
Dawa ya deni ni kulipa, hivyo nawaomba wote mjitahidi kulipa ili wadogo zetu pia nao wapate Elimu
 
Waswahili bwana ni watu wa ajabu.
Wasipopewa mkopo shida tupu. Walipewa mkopo leo wanajifanya kuuliza sijui barua sijui statement, hivi kweli hujui ulikopa shilingi ngapi na unatakiwa kulipa shilingi ngapi?
Hii inaonyesha hamkuwa na nia ya kulipa ndio sababu mmesahau madeni yenu ni shilingi ngapi!
Lipeni au wawapeleke mahakamani. Hivi bond zenu ilikuwa ni nini vile? zile nyumba za baba zenu? na mashamba yao?
Mama yangu weeeeeeeeeee mmekwisha. Kalipeni haraka wengine wasome.
 
Ni vema watu tuchangie kwa kuangalia hali halisi iliyopo, na si kwa ushabiki. Hoja walioleta wadau ya kwa kwamba hakukua na utaratibu wa kurejesha mikopo kipindi cha nyuma ni suala la msingi na ndivyo ilivyokuwa.
Sitetei watu kutolipa mkopo na sioni mdau aliyechangia kuwa hataki kulipa mkopo, lakini watu wanataka kuwa na uhakika kuwa ni kiasi gani wanadaiwa.
Kumbukumbu yangu zinaonyesha kuwa mikopo inaanza kulipwa kuanzia mwaka fulani huko nyuma (mwenye kumbukumbu atusaidie). Pili kama wadau wanavyosema tulipokuwa tunasoma kipindi kile tulikuwa tunapewa tu pesa na kuwa kuna cost sharing (ilikuwa haijulikani ni sh ngapi)
Binafsi nilishaanza kulipa, walileta taarifa kwa mwajili. Lakini ni ngumu kuthibitisha kuwa deni nililoandikiwa ndilo nililostahili kulipia kwani hili halikuwa wazi.
pendekezo langu ni kuwa ni vema bodi ikatowa hizi taarifa hizo kwa wanaopewa mikopo hiyo kwa sasa ili hata baadaye mtu binafsi awe na record zake sahihi juu ya alichopewa na atakachokuwa anadaiwa. Of course ni rahis kufuatilia kwa sasa ukiwa bado mwanafunzi kama data si sahihi kuliko baada ya miaka 13 na hauna record za kukusupport.
 
Hii nchi inaendaje?

Hivi kuna any sense of privacy? Haya mambo ya kutaka kufunga wadaiwa wenzetu Uingereza walishayapita miaka kama 100 iliyopita, sisi tunakazania kutaka kuwafunga watu waliokopa kusoa, wakati mafisadi waliojiuzia migodi na kusafisha mifuko ya Benki kuu kwa EPA tunasema ni wakubwa sana na hatuwezi kuwafunga?

Sikatai, mikopo lazima ilipwe, lakini kuna kitu kinaitwa dignity, daini kwa dignity.Hata mimi private citizen mbona kuna watu nawadai, tena wengine madeni sugu, lakini naelewa kwamba kuna kitu kinaitwa privacy, nikitaka kuwadai nawatafuta personally.

Wapelekeni mahakamani, kama kuna court reporter atawaripoti that is another matter, lakini sio kuwavua nguo hadharani na madeni yao, wengine watashindwa hata kuoa/kuolewa :)
 
Waswahili bwana ni watu wa ajabu.
Wasipopewa mkopo shida tupu. Walipewa mkopo leo wanajifanya kuuliza sijui barua sijui statement, hivi kweli hujui ulikopa shilingi ngapi na unatakiwa kulipa shilingi ngapi?
Hii inaonyesha hamkuwa na nia ya kulipa ndio sababu mmesahau madeni yenu ni shilingi ngapi!
Lipeni au wawapeleke mahakamani. Hivi bond zenu ilikuwa ni nini vile? zile nyumba za baba zenu? na mashamba yao?
Mama yangu weeeeeeeeeee mmekwisha. Kalipeni haraka wengine wasome.

Hivi ulisoma wapi Degree yako?
 
Nafikiri Hakuna anaekataa kulipa Deni la serikali, everyone wants wengine wasome.

Serikali haina wala haikuwa na utaratibu wa kukusanya madeni yao. Hii time ya Bodi ya Mikopo Imefeli.

Wakati Fulani tupo Mlimani zilikuja fomu au ilikuwa research ya namna gani serikali inaweza rudisha pesa. Kukawa na mengi yaliyoorodheshwa. lkn hapakuwa na utaratibu unaofahamika wa kurudisha mikopo.

Mtu unafanyakazi, unakatwa kodi 10%, NSSF 20%(Mwajiri+Mwajiriwa), Zote zinakwenda serikalini...sasa ukianza kutaka Mkopo lets say 10%, total 30%, unabakiwa na 70%, ikiwa salary yako ndio kubwa ya 250-500,000 utabakiwa na nini, then utakaa nyumba gani...ule nini...usafiri na mengineyo...? hata kama ikiwa wapokea 1M, then piga hesabu...

Moja ya Fikra wakati tupo mlimani ilitolewa ilikuwa serikali ilishauriwa kila mwanafunzi akimaliza waende kufundisha 1-2yrs shule za sekondari...hii ingepunguza gaps ya walim, lkn pia kila mwanafunzi kwa namna moja au ingine ingekuwa ni kurudisha sehem ya mkopo serikalini(serikali ingekuwa inasave kuajiri)

Ukichunguza fomu, fomu zilikuwa zinaonesha unatakiwa kukopeshwa pesa ya vitabu na mlo, tuition fee haikuwekwa. so wanafunzi hawajui Tuition fee kiasi gani....
 
Kwanza hiyo mikopo wakati inaanza tulilazimishwa kuomba kwa kujaza form. Kwa kumbukumbu yangu sikuwahi kupata barua ya kusema nimepata mkopo na ni kiasi gani. Sasa kama bodi imeishiwa pesa na wanataka kuokoteza kila mahali then watumie utaratibu mzuri badala ya kuzuka na kutoa majina ya watu magazetini. Hawajui kuwa wanaweza kuchafua majina ya watu kwa utaratibu huu???
Kaka kumbe unaushahidi wa kujitetea!
Hiyo maneno utaenda kuisema mahakamani (kama wakikushtaki!)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom