BodaBoda date-out or delivery?

BodaBoda date-out or delivery?

Achana na date.

Mimi hata kwa usafiri wa kawaida tu sijawahi na nafikiri sitapanda bodaboda.

Bora hata Bajaji.
Hapa umebugi! Ungekuwa Dar, usingetoa kauli hiyo. Kuna wakati wa kwenda Airport na foleni imebana. Utaikwea tena kwa kumshukuru Mungu kwa kuipata hiyo bodaboda. Mifano ni mingi sana
 
Nimekutana na utani mwingi huko Tiktok unaosema kuwa

“Unatoka out na mpenzi wako afu mnapanda bodaboda? Sasa io ni out au delivery mwanetu????" 😂
View attachment 3642089

Kwa mimi ninavyoelewa Boda boda au Pikipiki ni usafiri wa abiria wenye gharama nafuu kama 3k-5k.

Na wengine hutumia usafiri huo kwenda nao kazini na katika shughuli nyinginezo.

Usafiri huu wakati mwingine una kadhia nyingi mfano mnaweza kuloa na mvua, vumbi, na kuchomwa na jua. Hakuna AC, hakuna privacy.

Mnafikia destination mkiwa na macho mekundu na nywele zimeharibika. Sio gari, sio Uber, ni usafiri wa mwananchi wa kawaida kabisa.

Sasa hapa ndipo ugomvi unapoanzia:

Timu ya "Hii ni Delivery tu"

Wanasema out ina hadhi yake. Inatakiwa iwe na mipango, gari, restaurant, na kumpa mwanamke wako “privacy”.

Wanasema kutoka out na boda ni sawa na ku-order food, si date.


Timu ya "Out ni nia, sio gari”
Wanasema Upendo unapimwa na muda na malengo, sio na gari wala tax.Kuna watu walioanza na boda boda leo wana nyumba na magari.

Wanaongeza kuwa kama mnaelewana kweli hata usafiri waboda boda utakuwa kumbukumbu tamu. Kumpa mtu shida ya gharama kila mara ndio kunaua uhusiano.

Swali
1. Vigezo vya "Out" kwako ni nini?

2. Kama mpenzi anakualika "twende out" kwa usafiri wa boda boda utaenda au utagoma?

3. Wanaume unaweza kumchukua malkia wako kwa kutumia usafiri wa boda boda bila kujisikia vibaya?View attachment 3642087
Iwe Kwa, miguu,baiskeli, pikipiki,ngamia gari vyovyote vile,,inategemea na uwezo wangu ndio maana tunaambiwa tujikune tunapofikia,,hata mpenzi au mke namchagua wa level zangu Mambo yasiwe mengi full stop
 
Kila mtu afike na Usafiri wake,

NB: Kuna kikundi cha watu kitapinga hii kauli, Kikundi hicho hata boda boda hakitaki kupanda.
 
Back
Top Bottom