Boda boda tusaidiwe na sio kubezwa

Boda boda tusaidiwe na sio kubezwa

sangaone98

Senior Member
Joined
Apr 16, 2024
Posts
159
Reaction score
286
Muhali gani ndugu jamaa na marafiki waume kwa waume, Heshima kwa wakubwa zangu na kwa wadogo zangu me sijambo.

direct kwenye mada

Kama kichwa cha habari hapo juu
kinavyo jieleza watu wote tunao tumia pikipiki kama kifaa cha kutupatia mkate wetu wa kila siku na jua kali la mji huu wa anasa na matatizo pamoja na fulsa nyingi (Dar Es salaam) maarufu kama BODA BODA,

Jamii imekuwa ikitutazama kama watu tusio jielewa, waizi, tusio jali uhai wetu na watu wengine hasa tukiwa barabarani,
Tumepewa majina mengi yenye kuumiza na yasio ya kuumizi kama vishandu na afisa usafilishaji.

Leo nataka niongee na jamii ya hili jiji nakubaliana na nyote ya kwamba boda boda ni kero na zinasababisha maafa,ulemavu na kupoteza ramani za maisha kwa kukosa mwenendo ulio staharabika kama watumiaji wengine wa barabara

Tatizo sio waendesha pikipiki wote wana hizo tabia au walikuwa na hizo tabia ni namna ya kufanya kazi na kuhakikisha ziku inaisha bila matatizo na kama yatatokea basi tutawajibika na hilo lilio tokea. Au kukimbia

Mbali na kwamba bodaboda imekuwa ni usafiri rahisi na bei nafuu kwa kila mtumiaji wa chombo hichi bado kumekuwa na matatizo mengi yanayo husishwa na sisi boda boda nje na ndani ya jiji la maarifa ya ujinga na kujijenga kwenye nyanja ya uchumi. Tumekuwa na majina mengi mjina kama
-Wezi
-Vishandu
-Wasiojali
-Wajinga
-Maskini wa akili na mwili pamoja na fedha
-Malaya(kuharibu wanafunzi kwa danganya toto ya chipsi na lift)
-Wasababisha ajali kila kukicha
-Uchafu mjini kwa wingi wetu na mambo mengi yanayo umiza moyo na nafsi kwa wale wanao iona hii kazi kama njia ya kuwatoa kwenye wimbi kubwa la upungufu wa ajira pamoja na ukosefu wa mtu unae mjua kwenye office flani au tasisis flani( connection)

Vijana wengi walio soma na wasio soma boda boda imekuwa kimbilio lao la kujitaftia mkate wao wa kila siku,kwa njia tofauti lakini nguzo yao ni chombo cha mkopo kinacho uzwa milioni mbili na laki tano mpaka milioni tatu na laki tatu ila wanalipa elfu themanini na nne(84,000) kila wiki kwa wiki hamsini na tisa ( 59)
Mbali na matatizo yao kiuchumi, jamii na kisiasa
Bado ni watu wanao hitajika sana kwenye nyanja hizo ili kuendeleza shughuri za usafilishaji ndani na nje ya mji

M.f

UCHUMI boda boda ndio usafili pekee unao tunza matumizi ya muda kiuchumi ndani ya jiji lililo kuwa na miundombinu midogo na mibovu inayo sababisha foleni,
Kwa hesabu za kiuchumi utagundua mtu akipanda boda kutoka mbagara mpaka kariakoo anaweza tumia dk 20 hadi 18 tofaut na mtu anaepanda gari( daradara) akitumia dak 50 had 70 kufika kariakoo, je ni masaa mangapi yanapotea kwa watu 500 wanao panda magari binafsi na uma? Kwa kila siku za kazi hapa mji wa matajiri wa maneno ila ni PANGU PATUPU

KIJAMII, Wanafunzi, watu wazima, wafanyakazi na watu wote wa mishe mishe huwa wanaomba msaada kwa boda boda kuwafikisha mahali wanapo enda bila kuwa na nauli kabisa na boda boda wengi huwapakia nakuondoka nao kama msaada (Japo sio wote) kusaidia jamii kwa wale wenye kipato cha chini kabisa

KISIASA, Hawa watu na vyombo vya wanatumiaka kwenye kampen za kisiasa kuwasafilisha watu wanao toka mbali hata kwa malipo ya mafuta tu mpaka mikutano iishe kisha kutelekezwa na kuitwa uchafu,wezi,wabakaji,wasiojitambua na mambo mengi tu mabaya,

HIZO NI BAADHI YA FAIDA YA KAZI YETU NA HASARA YA KAZI YETU KWENYE NYANJA TOFAUTI ZINAZO GUSIA MAENDELEO

SASA TUNASAIDIWAJE SISI KAMA WATUMIA PIKIPIKI (BODA?)
1-Huduma za pyschology
Asilimia kubwa ya boda boda huwa wanakuwa njee ya mawazo yao pale tu wanapo kamata pikipiki zao kwaajili ya shughuli tofauti
Hawa watu wanaongea pekeyao wakiwa barabarani kama sehemu ya kumaliza uchungu wa maisha na gazabu za mateso ya barabarani na kwa kufanya hivo sio kama wanapenda hapana ni kwasababu tu wameona mengi na hakuna anae wasikiliza hata mmoja kila mtu akikutumia kwa bei ndogo anakuacha ukateseke mbele ya safari,

Canceling ya akiri;
kazi ya boda boda imekuwa ni kama kazi ya mtu anae enda vitani swala la kuludi nyumbani mzima ni changamoto kutokana na mambo ya hatari wanayo kutana nayo na kukumbana nayo kila wakipata fursa ya kupata kipato
Kwa taifa letu ndio watu wanao shuhudia maafa mengi kuliko mwanajeshi au doctor
Yaani mtu kakupita saivi mzima wa afya dk tatu mbele kapata ajali kafa papo kwa kwa papo( UBONGO UMESAMBAA) na unapita unamuona ila hauna budi kuwasha pikipiki na kuondoka bila kujua labda wewe ndio unafuat ajali ya mbele kwa uzembe wako au kwa uzembe wa mwingine hakika akili yako haitakuwa sawa kabisa
Boda boda ndiye mtu pekee anae kutana na vifo vingi pamoja na majeraha ya watu wengine mengi ndani ya siku mbili au tatu
Boda boda ndie mtu ambaye ananusulika kifo au kupata ulemavu kila akipata ajali moja kwa kila wakati, kweli unataka mtu huyu awe sawa kiakili na mtu asiye fanya kazi hii?
Asilimia 70 ya boda boda wa dar es salaam ni watumiaji wa mirungi,bange,pombe na nicotine sio kwa sababu ni hulka yao apana ni kwasababu ya mambo wanayo kutana nayo balabarani yanawanyima usingizi na hamu ya kufanya kazi tena kwa sasbabu hakuna pa kukimbilia wanaamua kutumia fake energy ya pombe,sigara,bangi,mirungi na hata madawa ili tu kupotezea kile walicho kiona au kukutana nacho kwenye kazi yao
Mbaya zaidi hakuna wa kuwasikiliza wala kujali kwa kile wanacho kipitia na hayo ndiyo yanakuwa maamuzi yao
fake energy (GANZI)
Fikiria tu mtu amekutana na ajari 5 za watu wamekufa Ajari 5 watu wamevunjika kwenye mazingira ya kazi yako kwa siku 5 mfululizo Je? unataka awe sawa na wewe kiakili?
TUNAITAJI MSAADA NA SIO KUBEZWA
Nawasilisha
Mr misele dar.
 
Boda boda yenyewe ina chata lilioandikwa "chizi kaachiwa","chizi katoroka" sasa ndo nini hiyo?
 
Wewe ndio unatakiwa ujitambue kwa kuzijua sheria za barabarani, kuvaa helment, kuhakikisha una leseni na bima. Hivi havihitaji msaada wowote toka kwa mtu yoyote bali ni kujitambua na kuiheshimu ofisi yako.

Wapo wachache sana wanao jitambua na wanajua kufuata sheria, ila wengi wenu hamfuati na hata mkielekezwa hamtaki kuelewa huku mkiendekeza virugu hata sehemu mlizo kosea nyinyi, tushukuru nchi yetu umiliki wa silaha ni mgumu kwa lugha zenu na vurugu sijui ingekuwaje.
 
Bodaboda

Hivi hii ni kifupi au ndo limeisha. Km ni kifupi, kirefu chake ni kipi na km ni kirefu maana yake nini?
 
Muhali gani ndugu jamaa na marafiki waume kwa waume, Heshima kwa wakubwa zangu na kwa wadogo zangu me sijambo.

direct kwenye mada

Kama kichwa cha habari hapo juu
kinavyo jieleza watu wote tunao tumia pikipiki kama kifaa cha kutupatia mkate wetu wa kila siku na jua kali la mji huu wa anasa na matatizo pamoja na fulsa nyingi (Dar Es salaam) maarufu kama BODA BODA,

Jamii imekuwa ikitutazama kama watu tusio jielewa, waizi, tusio jali uhai wetu na watu wengine hasa tukiwa barabarani,
Tumepewa majina mengi yenye kuumiza na yasio ya kuumizi kama vishandu na afisa usafilishaji.

Leo nataka niongee na jamii ya hili jiji nakubaliana na nyote ya kwamba boda boda ni kero na zinasababisha maafa,ulemavu na kupoteza ramani za maisha kwa kukosa mwenendo ulio staharabika kama watumiaji wengine wa barabara

Tatizo sio waendesha pikipiki wote wana hizo tabia au walikuwa na hizo tabia ni namna ya kufanya kazi na kuhakikisha ziku inaisha bila matatizo na kama yatatokea basi tutawajibika na hilo lilio tokea. Au kukimbia

Mbali na kwamba bodaboda imekuwa ni usafiri rahisi na bei nafuu kwa kila mtumiaji wa chombo hichi bado kumekuwa na matatizo mengi yanayo husishwa na sisi boda boda nje na ndani ya jiji la maarifa ya ujinga na kujijenga kwenye nyanja ya uchumi. Tumekuwa na majina mengi mjina kama
-Wezi
-Vishandu
-Wasiojali
-Wajinga
-Maskini wa akili na mwili pamoja na fedha
-Malaya(kuharibu wanafunzi kwa danganya toto ya chipsi na lift)
-Wasababisha ajali kila kukicha
-Uchafu mjini kwa wingi wetu na mambo mengi yanayo umiza moyo na nafsi kwa wale wanao iona hii kazi kama njia ya kuwatoa kwenye wimbi kubwa la upungufu wa ajira pamoja na ukosefu wa mtu unae mjua kwenye office flani au tasisis flani( connection)

Vijana wengi walio soma na wasio soma boda boda imekuwa kimbilio lao la kujitaftia mkate wao wa kila siku,kwa njia tofauti lakini nguzo yao ni chombo cha mkopo kinacho uzwa milioni mbili na laki tano mpaka milioni tatu na laki tatu ila wanalipa elfu themanini na nne(84,000) kila wiki kwa wiki hamsini na tisa ( 59)
Mbali na matatizo yao kiuchumi, jamii na kisiasa
Bado ni watu wanao hitajika sana kwenye nyanja hizo ili kuendeleza shughuri za usafilishaji ndani na nje ya mji

M.f

UCHUMI boda boda ndio usafili pekee unao tunza matumizi ya muda kiuchumi ndani ya jiji lililo kuwa na miundombinu midogo na mibovu inayo sababisha foleni,
Kwa hesabu za kiuchumi utagundua mtu akipanda boda kutoka mbagara mpaka kariakoo anaweza tumia dk 20 hadi 18 tofaut na mtu anaepanda gari( daradara) akitumia dak 50 had 70 kufika kariakoo, je ni masaa mangapi yanapotea kwa watu 500 wanao panda magari binafsi na uma? Kwa kila siku za kazi hapa mji wa matajiri wa maneno ila ni PANGU PATUPU

KIJAMII, Wanafunzi, watu wazima, wafanyakazi na watu wote wa mishe mishe huwa wanaomba msaada kwa boda boda kuwafikisha mahali wanapo enda bila kuwa na nauli kabisa na boda boda wengi huwapakia nakuondoka nao kama msaada (Japo sio wote) kusaidia jamii kwa wale wenye kipato cha chini kabisa

KISIASA, Hawa watu na vyombo vya wanatumiaka kwenye kampen za kisiasa kuwasafilisha watu wanao toka mbali hata kwa malipo ya mafuta tu mpaka mikutano iishe kisha kutelekezwa na kuitwa uchafu,wezi,wabakaji,wasiojitambua na mambo mengi tu mabaya,

HIZO NI BAADHI YA FAIDA YA KAZI YETU NA HASARA YA KAZI YETU KWENYE NYANJA TOFAUTI ZINAZO GUSIA MAENDELEO

SASA TUNASAIDIWAJE SISI KAMA WATUMIA PIKIPIKI (BODA?)
1-Huduma za pyschology
Asilimia kubwa ya boda boda huwa wanakuwa njee ya mawazo yao pale tu wanapo kamata pikipiki zao kwaajili ya shughuli tofauti
Hawa watu wanaongea pekeyao wakiwa barabarani kama sehemu ya kumaliza uchungu wa maisha na gazabu za mateso ya barabarani na kwa kufanya hivo sio kama wanapenda hapana ni kwasababu tu wameona mengi na hakuna anae wasikiliza hata mmoja kila mtu akikutumia kwa bei ndogo anakuacha ukateseke mbele ya safari,

Canceling ya akiri;
kazi ya boda boda imekuwa ni kama kazi ya mtu anae enda vitani swala la kuludi nyumbani mzima ni changamoto kutokana na mambo ya hatari wanayo kutana nayo na kukumbana nayo kila wakipata fursa ya kupata kipato
Kwa taifa letu ndio watu wanao shuhudia maafa mengi kuliko mwanajeshi au doctor
Yaani mtu kakupita saivi mzima wa afya dk tatu mbele kapata ajali kafa papo kwa kwa papo( UBONGO UMESAMBAA) na unapita unamuona ila hauna budi kuwasha pikipiki na kuondoka bila kujua labda wewe ndio unafuat ajali ya mbele kwa uzembe wako au kwa uzembe wa mwingine hakika akili yako haitakuwa sawa kabisa
Boda boda ndiye mtu pekee anae kutana na vifo vingi pamoja na majeraha ya watu wengine mengi ndani ya siku mbili au tatu
Boda boda ndie mtu ambaye ananusulika kifo au kupata ulemavu kila akipata ajali moja kwa kila wakati, kweli unataka mtu huyu awe sawa kiakili na mtu asiye fanya kazi hii?
Asilimia 70 ya boda boda wa dar es salaam ni watumiaji wa mirungi,bange,pombe na nicotine sio kwa sababu ni hulka yao apana ni kwasababu ya mambo wanayo kutana nayo balabarani yanawanyima usingizi na hamu ya kufanya kazi tena kwa sasbabu hakuna pa kukimbilia wanaamua kutumia fake energy ya pombe,sigara,bangi,mirungi na hata madawa ili tu kupotezea kile walicho kiona au kukutana nacho kwenye kazi yao
Mbaya zaidi hakuna wa kuwasikiliza wala kujali kwa kile wanacho kipitia na hayo ndiyo yanakuwa maamuzi yao
fake energy (GANZI)
Fikiria tu mtu amekutana na ajari 5 za watu wamekufa Ajari 5 watu wamevunjika kwenye mazingira ya kazi yako kwa siku 5 mfululizo Je? unataka awe sawa na wewe kiakili?
TUNAITAJI MSAADA NA SIO KUBEZWA
Nawasilisha
Mr misele dar.
Masada pekeemnao weza kusaidiwa ni kuambiwa mache upuuzi mkiwa barabarani😀
 
Back
Top Bottom