BodaBoda date-out or delivery?

BodaBoda date-out or delivery?

Iwe Kwa, miguu,baiskeli, pikipiki,ngamia gari vyovyote vile,,inategemea na uwezo wangu ndio maana tunaambiwa tujikune tunapofikia,,hata mpenzi au mke namchagua wa level zangu Mambo yasiwe mengi full stop
Nzuri sana hii
 
Gari ni muhimu sana, kama huna uwezo wa kununua, basi usikose app ya bolt/Uber kama unaishi mjini

Kama upo vijiji kama babu zenu, basi usikose hata pikipiki Incase mwenza wako ama mtoto wako akipata homa ya usiku iwe rahisi kumkimbiza zahati/kituo cha afya cha jirani
Huu ndio ukweli wenyewe 😜
 
Bora bajaji, hizi boda boda ni risk sana kwa safari ndefu
Kama tupo na beibe na hatuna gari, tutarequest tu bajaji
 
Nimekutana na utani mwingi huko Tiktok unaosema kuwa

“Unatoka out na mpenzi wako afu mnapanda bodaboda? Sasa io ni out au delivery mwanetu????" 😂
View attachment 3642089

Kwa mimi ninavyoelewa Boda boda au Pikipiki ni usafiri wa abiria wenye gharama nafuu kama 3k-5k.

Na wengine hutumia usafiri huo kwenda nao kazini na katika shughuli nyinginezo.

Usafiri huu wakati mwingine una kadhia nyingi mfano mnaweza kuloa na mvua, vumbi, na kuchomwa na jua. Hakuna AC, hakuna privacy.

Mnafikia destination mkiwa na macho mekundu na nywele zimeharibika. Sio gari, sio Uber, ni usafiri wa mwananchi wa kawaida kabisa.

Sasa hapa ndipo ugomvi unapoanzia:

Timu ya "Hii ni Delivery tu"

Wanasema out ina hadhi yake. Inatakiwa iwe na mipango, gari, restaurant, na kumpa mwanamke wako “privacy”.

Wanasema kutoka out na boda ni sawa na ku-order food, si date.


Timu ya "Out ni nia, sio gari”
Wanasema Upendo unapimwa na muda na malengo, sio na gari wala tax.Kuna watu walioanza na boda boda leo wana nyumba na magari.

Wanaongeza kuwa kama mnaelewana kweli hata usafiri waboda boda utakuwa kumbukumbu tamu. Kumpa mtu shida ya gharama kila mara ndio kunaua uhusiano.

Swali
1. Vigezo vya "Out" kwako ni nini?

2. Kama mpenzi anakualika "twende out" kwa usafiri wa boda boda utaenda au utagoma?

3. Wanaume unaweza kumchukua malkia wako kwa kutumia usafiri wa boda boda bila kujisikia vibaya?View attachment 3642087
Kikubwa ute uwepo tu.
 
Back
Top Bottom