Biashara ya Kuuza Nyama (Butcher's Shop): Mambo Mbalimbali ya Kujifunza

Aiseee!!upatkanaj wa nyama Ndo naona ukiwa rahis sana maanaa machinjio yako karbu sana. Kuna machinjio ya Vingungut
G/mboto Mombasa, kama unaenda Moshi bar. Kuna inatiwa Mazizin iko hapo.
 
ngoja nianze hivi wenzangu wataongezea.

1. Uwe na mtaji wakutosha
2. Uwe na location nzuri kwajili ya kufungua hiyo bucha/mabucha.
3. Kama unaweza tafuta na kununua hao wanyama mikoani uchinje mwenyewe hii itakuongezea faida
4. Shirikiana na wazoefu katika biashara hii waliopo eneo husika.
5. Fanya kazi kwa bidii na kujituma..hii biashara inalipa sana hasa ukiwa miji mikubwa.
kila la heri mkuu
Appreciated..
 
Niongezee tu kukuuliza, hivi inatakiwa uwe na mtaji wa kuanzia kama million ngapi?
Ili ujue ni kiasi gani kitahitajika fanya haya:-

1. Orodhesha vifaa vyote utavyohitaji kuwa navyo mf. Cutting machine, freezer (la kuhifadhia nyama iliypbaki ili isiharibike), mzani , fan (hii inasaidia kufukuza nzi, mteja akija akakuta mazingira machafu manzi yamejazana kesho, hatorudi tena) n.k (hakikisha umelist vitu vyote muhimu)

2. Ulizia bei ya kila kifaa (tembelea kwa wauza bucha kwanza uwaulize ili wakupe estimate ya kila kifaa ili usilanguliwe pesa nyingi huko dukani wanapouza)

3. Baada ya hapo piga hesabu ya vifaa vyoote ulivyoorodhesha(+usafirishaji kutoka sehemu uliponunua mpaka kwenye frem), bila kusahau kodi ya frem (angalau ya miezi sita sio mbaya), mshahara kwa muuzaji (kama utakua umemuajiri mtu), umeme, n.k

Kwa kufanya hivi, utaweza kujua ni kiasi gani cha pesa kitahitajika. Hapa sijapigia hesabu za kufatilia leseni na vibali (sijui kama vipo/vinahitajika au lah), matengenezo ya fremu kuwa na hadhi ya bucha (mara nyingi huwa wanaweka aluminum door na tiles kufanya mazingira kuwa nadhifu na kuvutia wateja) n.k
 
Mkuu mi nakupa kimoja ambacho wengi hawakisema ni katika faid, nyama jumla unaweza nunua Tshs3500 then wewe unakuja uza Tshs6000 pia kunasehemu nyingine wanauza chini au zaidi kidogo, ukiweka na usafiri kusafirisha nyama nadhani unaweza gundua unaweza pata kiasi gani.
 
Unahitaji Freeze kubwa,Unahita mashine ya kukata Nyama.Biashara ya bucha inalipa ukianza na bucha moja ahalafu ukawa na gari ya kusambaza nyama.Unaenda Unanunua Ngombe Mzima. Unaanza kumuuza machinjioni.Inayobaki unasambaza kwa watu kisha unaweka nyingine buchani kwako.Mtaji wa Chini ni kodi plus laki tano ya nyama
 
mkuu mi nakupa kimoja ambacho wengi hawakisema ni katika faid, nyama jumla unaweza nunua Tshs3500 then wewe unakuja uza Tshs6000 pia kunasehemu nyingine wanauza chini au zaidi kidogo, ukiweka na usafiri kusafirisha nyama nadhani unaweza gundua unaweza pata kiasi gani
Chief niko Kilimanjaro nataka kufanya hii biashara sijapata sehemu nzuri ya kuweka office
 
Biashara ya nyama nzuri

1.frem ( tafuta maeneo yakawaida hata yenye mabutcher mengine manake utauza tu ukiwa na muuzaji mzuri) kodi itategemea na eneo

2. Gogo la kukatia nyama kwa dar 40000 hadi 50000 inategemea na mahali

3. Mashine yakukatia nyama sikushauri unune mwanzoni ingawa ni yamuhimu kiasi bei ni 1.3 mpka 1.5 kkoo
4. Friza la 250000 linatosha kuanzia manake ni kwa dharura kwa nyama inayobaki na usipange kununua nyama nying kujaza butcher wakati haitoki kwa wingi
5.meza ya bati kwaajili yakuweka vitu kama mizani,visu n.k
6.mizani ni laki kkoo
7.chuma la kuninginizia nyama
8. Lesseni ya biashara 80
9.TFDA certificate

Inakusaidia mkuu kiasi.
Rangi ni lazima iwe nyeupe? Maana wengine tunataka ongeza na vitu vya ziada
 
Unahitaji Freeze kubwa,Unahita mashine ya kukata Nyama.Biashara ya bucha inalipa ukianza na bucha moja ahalafu ukawa na gari ya kusambaza nyama.Unaenda Unanunua Ngombe Mzima.Unaanza kumuuza machinjioni.Inayobaki unasambaza kwa watu kisha unaweka nyingine buchani kwako.Mtaji wa Chini ni kodi plus laki tano ya nyama
Ohoooo na gari je?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kwenye mabucha nilisikia watawala wakisema wanatoa miezi sita wenye mabucha wawe wameweka machine ya kutatia Nyama hawataki kuona magogo.umeme ukikatika wanunue jenerator ambapo Kwa hesabu za haraka haraka ni kama 2m sasa nawaza Kwa wale wenye biashara changa na makodi ndio hayo dah,wafikirie upya jamani wawape angalau mwaka wajipange au mnaonaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kwa kwenye mabucha nilisikia watawala wakisema wanatoa miezi sita wenye mabucha wawe wameweka machine ya kutatia Nyama hawataki kuona magogo.umeme ukikatika wanunue jenerator ambapo Kwa hesabu za haraka haraka ni kama 2m sasa nawaza Kwa wale wenye biashara changa na makodi ndio hayo dah,wafikirie upya jamani wawape angalau mwaka wajipange au mnaonaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ulisikia? Wapi na naomba uthibitishe usemacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom