GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,059
- 126,650
Mimi nipo hapa hapa Mbagala Rangi 3, na kwa taarifa rasmi, hawa majambazi hawajaua mtu yeyote, na wala hawakufanikiwa kuiba kiasi chochote cha fedha (meneja chonde-chonde, usije jitwalia akiba zetu).
Hongera kwa walinzi wa benki, maana ndio wamepambana na majambazi kwa muda mrefu, hadi majambazi walipoanza kukimbia, na baada ya muda wakazingirwa na askari, na kuanza kukimbia ovyo.
Nitaendela kuwajuza, maana kuna nyumba wameingia, na imezingirwa na polisi... japo mwenye nyumba amekamatwa na anadai hakuna jambazi aliyengia ndani kwake...!
Kama Hawajaua au Hakuna Aliyekufa Hizo DAMU Hapo Mbele Tunazoziona Ni Za Nini?