Benki ya Access Tawi la Mbagala Imevamiwa!

Benki ya Access Tawi la Mbagala Imevamiwa!

6-20.jpg
Polisi wakiimarisha ulinzi kwenye benki hiyo iliyovamia na wanaosadikiwa kuwa majambazi Mbagala, Dar.

WATU wanaosadikiwa kuwa majambazi na ambao idadi yao inasadikiwa kuwa sita wakiwa na mabomu na bunduki za kisasa jana walivamia Benki ya Access tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam ambako walipora viroba vya fedha, kuua mlinzi na baadaye wanne kati wakauawa na polisi.
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema baada ya watu hao kufika katika benki hiyo kwa bodaboda nne majira ya saa nane mchana, walimuua mlinzi wa benki hiyo, kisha kubomoa kwa risasi mlango wa vioo na kuingia ndani na kuzua taharuki kubwa ndani ya benki hiyo.

5-1-3-614x1024.jpg

Mmoja wa majambazi hao baada ya kuuawa.

Mashuhuda hao walisema, katika tukio hilo lililodumu kwa karibu saa moja, mmoja wa majambazi hao aliyekuwa amevaa kininja, alikuwa barabarani akiamuru magari kupita haraka huku akifyatua risasi hovyo.

Ilielezwa kuwa jambazi huyo aliyeonekana kuwa na uzoefu wa matumizi ya bunduki alikuwa akifyatua risasi kwa kutumia mkono mmoja na ndiye aliyewajeruhi baadhi ya wapita njia.

3-31.jpg

Majambazi wawili kati ya wanne waliouawa wakiwa katika gari la polisi.

Wakati uporaji ukiendelea na jambazi huyo akiimarisha ulinzi barabarani baadaye hakukuwa na magari wala pikipiki zilizokuwa zikipita.

Mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi jirani na benki hiyo, Ramadhani Tairo, alisema baada ya jambazi huyo kuliona gari la polisi likielekea eneo la tukio, alifyatua risasi na kulipiga kabla halijafika. Gari hilo lilipoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni.

Tairo alisema mbali na jambazi huyo kulipiga risasi gari la polisi pia alilirushia bomu la mkono, lakini liliangukia barabarani bila kulipuka. Polisi walifanikiwa kulifyatua bomu hilo baadaye likiwa halijasababisha madhara kwa wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Rebecca Maliva, alisema majambazi walioingia ndani ya benki hiyo walionekana wakitoka na viroba vitatu vya fedha ambavyo walivipakata kwenye pikipiki na kuondoka kwa kasi kuelekea Mkuranga kupitia barabara ya Kilwa.

Rebecca alisema polisi zaidi walifika kwenye eneo hilo wengine wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwafukuza majambazi hao ambapo walipofika eneo la shule ya St. Mary’s, walitupa kiroba kimoja cha fedha ambacho wananchi waliokuwa jirani waligombania na kuchukua fedha zilizokuwemo na kisha kila mmoja kukimbia na bulungutu la noti.

Baada ya nusu saa wakati umati ukiwa bado upo kwenye benki hiyo, magari ya polisi yalipita katika eneo hilo yakitokea eneo la Mkuranga yakiwa yamebeba miili ya majambazi waliouawa.

Magari hayo yalikuwa yakisindikizwa na vijana wa bodaboda waliokuwa wakishangilia kazi iliyofanywa na polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alizungumzia kwa ufupi tukio hilo akasema majambazi wanne wameuawa na kukamata silaha tatu, lakini hakutaka kuingia kwa ndani zaidi akisema atatoa taarifa baadaye.

Chanzo.Wanne wauawa na polisi kwa kuvamia benki Mbagala
 
Nawapongeza askari polisi kwa kazi nzuri. Lakini hivyo viroba vya pesa vilivyosalia mbona hatusikii vikiripotiwa, au ndo tusha......!!!
 
Nawapongeza askari polisi kwa kazi nzuri. Lakini hivyo viroba vya pesa vilivyosalia mbona hatusikii vikiripotiwa, au ndo tusha......!!!
Vyote vilishapotea..hio ni.hasara kwa benki.imekula kwao
 
Hatuwezi kwenda mbele kama nchi kwa kubahatisha usalama. Hii nchi imeishafikia wakati wa kuwa na CCTV cameras kwenye miji mikubwa kwa kuanzia Dar. With CCTV camera labda majambazi yangeonekana yanatokea wapi na kuelekea wapi na huenda tukio lisingetokea. Pia polisi wabadili style za kulinda benki maana kila kibanda cha walinzi kinaonekana kirahisi, waanze kutumia na makachero wasio na uniform kulinda au kufanya doria za kimya kimya na bastora wakionekana kama raia wa kawaida
 
vyombo vya ulinzi inabidi waboreshewe mishahara hayo maana wanafanya kazi katka mazingira magumu pia wana kundi kubwa la familia lina wategemea imagine kama akifa afu ukicheq mshahara hauzidi laki 3 unadhani familia yake itaambulia nn katka mirathi huo nduo mwanzo wa kuwa na kaya maskini...
 
Nakubaliana Na wewe kwa kuweka CCTV, lakini silaha kubwa itakayosaidia vyombo vya usalama ni matumizi ya helikopta
 
Duu hawa jamaa wana mabomu ya kurusha hata police wakitumia chopa ni hatari sana pia..kwanza ni kufanya ukaguzi wa siraha nyingi tena zile kivita zipo mtaani..
 
Nakubaliana Na wewe kwa kuweka CCTV, lakini silaha kubwa itakayosaidia vyombo vya usalama ni matumizi ya helikopta
CCTV ni zaidi ya helicopta kwa vile polisi wataweza kuwatambua majambazi kwa sura zao. Na ndio maana tunasisitiza suala la vitambulisho vya taifa kwa kila mtanzania ili tuwe na database yenye sura na alama za vidole za watanzania wote
 
Duu hawa jamaa wana mabomu ya kurusha hata police wakitumia chopa ni hatari sana pia..kwanza ni kufanya ukaguzi wa siraha nyingi tena zile kivita zipo mtaani..
Aiseee!!!! Unajua unachoongea mkuu!!??? Una uhakika mtu anaweza kurusha bomu la mkono (Hand grenade)
Kufikia umbali wa ilipo helikopta angani!? Let's get real fella!
 
vyombo vya ulinzi inabidi waboreshewe mishahara hayo maana wanafanya kazi katka mazingira magumu pia wana kundi kubwa la familia lina wategemea imagine kama akifa afu ukicheq mshahara hauzidi laki 3 unadhani familia yake itaambulia nn katka mirathi huo nduo mwanzo wa kuwa na kaya maskini...
mshahara wa polisi ni zaidi ya laki tatu mkuu.
 
Aiseee!!!! Unajua unachoongea mkuu!!??? Una uhakika mtu anaweza kurusha bomu la mkono (Hand grenade)
Kufikia umbali wa ilipo helikopta angani!? Let's get real fella!
Labda alimaanisha JAMBAZI linaweza kufyatua risasi na kupiga helikopta , matokeo yake kuhatarisha maisha ya raia wa kawaida mitaani pindi itakapoanguka.
 
Labda alimaanisha JAMBAZI linaweza kufyatua risasi na kupiga helikopta , matokeo yake kuhatarisha maisha ya raia wa kawaida mitaani pindi itakapoanguka.
Practically kuweza kuitungua helicopter ikiwa angani it's highly impossible kutokana na umbali itakayokuwa. Usikariri ile issue ilitokea juzi juzi huko porini..kwanza ile helicopter ilikuwa ni zile ndogo na ilikuwa inaruka chini sana kulinganisha na za Polisi. Kuna mambo mengine ya kitaalamu zaidi hatuwezi kuyaweka humu. Ila inawezekana kuyakimbiza majambazi na helicopter na ikafanikiwa kuyadhibiti. Inahitaji utaalamu na helicopter iwe well equipped na gadgets muhimu ie: infrared cameras etc.
 
hawa majambazi hawana viatu? na yule mwingine hana damu wala hana suruali alipigwa kofi akafa?
 
hawa majambazi hawana viatu? na yule mwingine hana damu wala hana suruali alipigwa kofi akafa?
Nafikiri itakuwa yalivaa sandozi za kimasai. Hilo moja lilivaa mlegezo likiwa ujambazini ona sasa matokeo yake makalio yote yako wazi.
 
Practically kuweza kuitungua helicopter ikiwa angani it's highly impossible kutokana na umbali itakayokuwa. Usikariri ile issue ilitokea juzi juzi huko porini..kwanza ile helicopter ilikuwa ni zile ndogo na ilikuwa inaruka chini sana kulinganisha na za Polisi. Kuna mambo mengine ya kitaalamu zaidi hatuwezi kuyaweka humu. Ila inawezekana kuyakimbiza majambazi na helicopter na ikafanikiwa kuyadhibiti. Inahitaji utaalamu na helicopter iwe well equipped na gadgets muhimu ie: infrared cameras etc.
kwahiyo unataka kusema Helikopta ya police haifikiwi na risasi au?
 
kwahiyo unataka kusema Helikopta ya police haifikiwi na risasi au?
Soma vizuri post yangu uelewe kijana. Na ndio maana nilisema kuna vitu vinahitaji mafunzo stadi na mengi hatuwezi kuyaanika humu kwa sababu za kiusalama.
 
ANDIKENIII YOOTEEEE LAKINII HAYA MATUKIOO YASIWAKUTEE MKO BANK

SITOSAHAUU. TUKIOO MOJA AZIKIWE TULILAAA CHINI FASTA KAMA NIKO JKT TOA VITUFUKON YAANII NILITOAA KATOCHII CHANGUU KINA NAMBAA ZOOTE DUNIAN ZINAZONIHUSUU HUKUU NASALII MOLA WAPITIEE HII POCHI INA ALF SABA ..WAKAANZA OKOTS POCHI MOJAMOJA BANA BAADA YA MUDA NAONA MWENZANGU ANANYANYUKA NDIO KUNYANYUKA NAKUTA KATOCHI KA NOKIA KAMESURVIVE AISEE KUANGALIA CHINI

MIITO YA BAHARIII USINIULIZE BAHARIGAN

POLEN WAHUSIKAKAA
 
Ni kweli ni, kabisa kukubaliana

http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Back
Top Bottom