BBC: Tanzania kuingia uchumi mdogo wa kati wajipange, misaada na mikopo nafuu yote itakoma na haitapata misaada kama zamani na upendeleo wa kifedha

Siasa za kibongo hatari sana,yan mtu amechukia kabisa nchi yake kuingia low mid income
Duh....!
Sijaona kwenye hii mada mahali kuna chuki.
Ni hatua nzuri tumeingia, lakini tunatakiwa tujipange sawasawa, kuna vitu tutakosa hivyo tunatakiwa kuchapa kazi zaidi na zaidi.
 
Ni kweli.

Lakini kweli kuna nchi inayofurahia kuwa maskini ili ipate misaada?

Kama kuna sababu za kusikitikia kupanda daraja, binafsi sizioni hizi kuwa za muhimu.

Ndio, ni kama kijana kabalehe, kawa mtu mzima, acha akapambane na dunia. Pengine tukipata ugumu huo, ndio akili itatuingia vichwani.

Mkuu kwani kwenye huu uzi kuna mtu anasikitika Tz kupanda daraja?

Umetoa mfano mzuri sana, na ndivyo kama nchi tunatakiwa sasa kupambana na hali yetu. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayefurahi nchi kuwa ombaomba.
 
Kwahiyo unashauri tupambane kurudi daraja la chini ili tuendelee kusaidiwa?
Kubishana na chadema utaua MB zako za akili bure!!

Chadema litangazwe kuwa janga la kitaifa ni shida! Ukiumwa watasema kwa nini umeumwa? ukipona watasema kwa nini upone ulistahili ufe? usipougua watasema huumwi tu kwa sababu hujapima afya? Ukipima afya ukaonekana mzima watasema vipimo ulivyopimia ni feki! Chadema utoto mwingi!
 
Ni vizuri kabisa misaada na mikopo ikapungua sababu mingi haina maslahi kwetu wala kwa nchi yetu. Sisi kana taifa tuchukue changamoto yoyote kuwa chanya kwetu ili tuweze kupiga hatua na sio kulala.

Rais Magufuli alishaonyesha njia kwa vitendo alipokataa mikopo ya kupambana na COVID19. Nadhani hata wenye kutoa washaelewa Tanzania iko na msimamo gani
 
Kwa hatua hii tuliyofikia lazima tumpongeze Mh. Rais na serikali yake kwa ujumla. Kujitegemea ni kwenye baadhi ya nyanja ni jambo jema na hii tutafanikiwa ikiwa kutakuwa na ufanisi wa kutosha katika ukusanyaji wa kodi ni dhahiri serikali bado inapoteza kodi nyingi kutoka kwenye vynzo vyake vya kodi, risiti za EFD hazitumiki maeneo mengi.

Kuna malipo mengine kwenye taasisi bado yanafanyika manual hakuna control namber, ukienda sehemu zingine kununua kitu ukidai risit wanasema mashine imeharibika ipo kwenye matengenezo.

Uchumi wetu unatajengwa na sisi wenyewe na heshima ya mtu ni kujitegemea tukijijengea utamaduni wa kudai na kutoa risiti tutaishangaza dunia mda sio mrefu maana mapato yanayopotea ni mengi sana.
 
Mkuu kwani kwenye huu uzi kuna mtu anasikitika Tz kupanda daraja?
Umetoa mfano mzuri sana, na ndivyo kama nchi tunatakiwa sasa kupambana na hali yetu. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayefurahi nchi kuwa ombaomba.
Mkuu usishangae hili la nchi kupanda daraja kiuchumi.... Tanzania kuna watu wana akili za ajabu sana, imagine wapo wanaosikitika COVID19 kutokuua watu wengi. Mtu mzima wanatamani vifo vya COVID viwe vingi ili rais aonekane ameshindwa kazi, sad.
 
Duh....!
Sijaona kwenye hii mada mahali kuna chuki.
Ni hatua nzuri tumeingia, lakini tunatakiwa tujipange sawasawa, kuna vitu tutakosa hivyo tunatakiwa kuchapa kazi zaidi na zaidi.
Nimepitia mitandaoni nimeona hiyo kitu bro,cha kupaswa kujua vitu kama hivi vitakuja kusaidia vizazi vyetu vijavyo,iwe mid income,iwe sgr iwe ndege etc,ila wengi wetu tunajiangalia sisi tu atuangalii miaka 30 mbele na ndio maana tunapinga tu
 
Back
Top Bottom