BBC: Tanzania kuingia uchumi mdogo wa kati wajipange, misaada na mikopo nafuu yote itakoma na haitapata misaada kama zamani na upendeleo wa kifedha

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Kwa furaha tunayofurahia ndio tujipange kwa sababu maumivu yanayokuja kwa kupanda daraja ni makubwa.

1. Misaada iliyokuwa inapata kama nchi maskini itakatwa
2. Mikopo iliyokuwa inasemwa nafuu itakuwa haipo tena.
3. Mikataba yenye unafuu wa kibiashara itakuwa tofauti ile dhana ya kusaidiwa inaondolewa kwa sababu unajiweza.
4. Misaada kama ya madawa mfano HIV inaweza kuondoleaa ikiwemo na baadhi ya chanjo.

Hivyo tujipange.

Pia soma
- Nini maana ya Tanzania kutangazwa kuwa Nchi ya Uchumi wa Kati (MIC) na Benki ya Dunia?
- News Alert: - Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati
 
Hilo la kujitegemea ndio lengo la kila taifa duniani. Hata familia, baba ukiwa ni mtu wa kuonewa huruma na kusaidiwa huwa inauma sana na kila wakati unatamani uilishe familia yako mwenyewe, huo ndio uanaume.

Btw, kwa beberu hakuna kitu 'msaada', akikupa chochote ni lazima ukilipie kwa namna nyingine × 7. Na hapo ndipo kiini cha umaskini wa mataifa mengi kilipo.

Wanasema wenyewe... No free lunch!
 
Ni kweli.

Lakini kweli kuna nchi inayofurahia kuwa maskini ili ipate misaada?

Kama kuna sababu za kusikitikia kupanda daraja, binafsi sizioni hizi kuwa za muhimu.

Ndio, ni kama kijana kabalehe, kawa mtu mzima, acha akapambane na dunia. Pengine tukipata ugumu huo, ndio akili itatuingia vichwani.
Nafkiri mtoa hoja amekusudia kutukumbusha kujipanga ktk hatua hii kubwa!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom