Tusikatae chakula tu, tuikatae pia misaada na mikopo ya fedha kutoka kwa wazungu

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,838
18,250
Mchezo wa kukataa mchele kutoka Marekani ni zaidi ya mchezo maarufu wa kombolela unaochezwa na watoto. Mchezo wa kitoto haukeshi. Sote tunafahamu kuwa msaada ni kitu kinachotolewa kwa hisani (goodwill) bila mpokeaji kuhitaji kumpa masharti mtoaji. Taarifa za Bashe (Waziri wa Kilimo) kuukataa msaada wa mchele wenye virutubisho zimepokelewa kwa mshtuko na watanzania wazalendo wanaofahamu madhara ya kukataa msaada kutoka Marekani.

Na madhara haya yanaweza kuwa makubwa pale Bashe alipoonesha wasiwasi kuwa huenda mchele huu umetiwa sumu au kuwachanganyia homoni za kishoga kwa lengo la kuwadhuru watanzania. Bashe amesema haya kabla ya kufanya uchunguzi wa kina (food analysis) kuhusu chakula kilicholetwa kama kimebeba sumu au homoni za kishoga.

Kibaya zaidi, kabla vumbi hili halijatulia, shirika la viwango la Taifa (TBS) limetoa taarifa sahihi kuwa mchele huu wameufanyia uchunguzi na kugundua kuwa unakidhi vigezo vya kuliwa na binadamu na uingizaji wake hapa nchini umefuata taratibu zote zinazotakiwa.

1710761143841.png
Hapa tayari tumejenga ugomvi na Marekani. Tukumbuke kuwa Marekani haina rafiki wa kudumu na wakiamua kukushughulikia hawakosi sababu. Tazama jinsi walivyokuwa na urafiki na Osama lakini baadaye wakatofautiana na kumshughulikia hadi kumuua.

Pia tusijitoe ufahamu jinsi Marekani alivyotafuta sababu za kuingia Iraki na hatimaye kumuua Sadam Hussein kwa kisingizio ambacho hakikuwepo. Sembuse Tanzania ambayo imeonyesha dharau ya waziwazi na kuituhumu Marekani kuwa imewatilia sumu na homoni za kishoga kwenye chakula.

Hivi huyu mtu anajua gharama za vita kutoka nchi yenye vifaa vya kisasa na mifumo mizuri ya kupigana? Ikitokea Marekani wakakinukisha na Tanzania. Je, sisi raia tutakimbilia wapi?

Tunapaswa kufahamu kuwa nchi zinaishi kwa kutegemeana. Hakuna nchi iliyojitosheleza kwa kila kitu. Hata Marekani kuna wakati wanahitaji misaada kutoka China, Japan, Uingereza, Urusi na nchi nyingine. Itakuwa Tanzania, nchi hohehahe isiyokuwa na mbele wala nyuma!

Sisi tunategemea karibu kila kitu kutoka Ulaya na Marekani. Chanjo na dawa zote za binadamu zinatoka Marekani. Mfano mzuri ni chanjo ya COVID-19. Chanjo hii kwa kiasi kikubwa imetoka Marekani na bado tunayo dozi ya kutosha inayoendelea kutolewa kwa watanzania bure. ARVs zinazotolewa bure kwa wagonjwa wa UKIMWI zinatoka Marekani. Hivi Marekani leo hii wakigoma kutoa ARVs wagonjwa wetu si watakufa? Nani ana uwezo wa kugharamia dawa hizi? Sio serikali wala wananchi wanaoweza kugharamia dawa hizi.

Sasa huyu Bashe anayetaka kutugombanisha na Marekani anataka watu wetu wafe kwa kukosa dawa au anataka nini hasa? Ikiwa dawa na chanjo zote hizi tunazitegemea kutoka kwa wazungu, je wangekuwa na nia ya kutuua nani angebaki salama? Chanjo zote ambazo watoto wanachanjwa tangu wakiwa wadogo zingekuwa na madhara si kila mtanzania angekuwa zombie? Kungekuwa na mtanzania hata mmoja mwenye akili timamu? Acheni kutafuta matatizo na wazungu huku ukijua bado huna uwezo wa kusimama mwenyewe.

Kana kwamba hili halitoshi, bado 60% ya bajeti yetu inategema michango na mikopo kutoka kwa wahisani. Je, wahisani hawa wakigoma kutuchangia kwenye bajeti tutajiendeshaje? Watu wengine wanajitoa ufahamu na kudai eti tunazo rasilimali za kutosha kujiendesha wenyewe. Rasilimali hizi tunazo tangu dunia hii ilipoumbwa lakini hatuna uwezo wa kuzichakata na kuzitumia. Mambo madogo kama ujenzi wa barabara na reli tunawatumia wazungu na wachina. Tunashindwa kutengeneza vitu vidogo kama vijiti vya meno na sindano. Huo uwezo wa kuchimba madini na kuchakata rasilimali nyingine tulizo nazo tutaupata wapi ikiwa tunashindwa kufanya mambo madogo kama haya?

Kama tuna jeuri ya kukataa msaada wa chakula, basi tusiishie hapo tu. Tukatae pia michango ya bajeti kutoka kwa wahisani na tukome kukopa mikopo ya maendeleo kutoka benki za wazungu (WB, IMF, etc). Ikiwa hatuwezi haya, tukae chini tutulize matako tuache chokochoko za kijinga wakati bado hatuna uwezo wa kusimama wenyewe kama nchi inayojitegemea.

Nawasilisha.
 
Waziri Bashe nadhani ameteleza kwa aliyoyasema. Ukweli ni kwamba bad Tanzania tunahitaji kill aina ya misaada kutoka nchi rafiki.

Suala hili la msaada wa mchele limetoa picha halisi ya alivyo Waziri na Serikali yake. Hivi msaada chakula hiki ungetoka Uarabuni kungekuwa na hoja hizi?

Ukweli ni kwamba, zamani Tanzania ilikuwa ni Nchi ya wakulima na wafanyakazi; lakini leo wafanyakazi ndio wamekuwa wakulima wakubwa na wale wakulima wa zamani wengi wao sio wakulima tena bali wamebaki kukodisha mashamba yao: kwa hiyo hawa wakulima wafanyakazi wanaona mchele huon kutoka Merikani unaweza kuadhiri bei ya mchele wao kuwa ndogo na hivyo kupata hasara.

Tuna saidiwa chakula bora bure, kwa ajili ya watoto wetu mashuleni, tunakataa lakini tunatumia $ nyingi kwa ajili ya kununulia chupi, shidiria na nguo zingine za mitumba: KWA KWELI HAIPENDEZI NA NI AIBU KWA TAIFA
 
Mchezo wa kukataa mchele kutoka Marekani ni zaidi ya mchezo maarufu wa komboleya unaochezwa na watoto. Mchezo wa kitoto haukeshi. Sote tunafahamu kuwa msaada ni kitu kinachotolewa kwa hisani (goodwill) bila mpokeaji kuhitaji kumpa masharti mtoaji. Taarifa za Bashe (Waziri wa Kilimo) kuukataa msaada wa mchele wenye virutubisho zimepokelewa kwa mshtuko na watanzania wazalendo wanaofahamu madhara ya kukataa msaada kutoka Marekani.

Na madhara haya yanaweza kuwa makubwa pale Bashe alipoonyesha wasiwasi kuwa huenda mchele huu umetiwa sumu au kuwachanganyia homoni za kishoga kwa lengo la kuwadhuru watanzania. Bashe amesema haya kabla ya kufanya uchunguzi wa kina (food analysis) kuhusu chakula kilicholetwa kama kimebeba sumu au homoni za kishoga.

Kibaya zaidi, kabla vumbi hili halijatulia, shirika la viwango la Taifa (TBS) limetoa taarifa sahihi kuwa mchele huu wameufanyia uchunguzi na kugundua kuwa unakidhi vigezo vya kuliwa na binadamu na uingizaji wake hapa nchini umefuata taratibu zote zinazotakiwa.
View attachment 2938233
Hapa tayari tumejenga ugomvi na Marekani. Tukumbuke kuwa Marekani haina rafiki wa kudumu na wakiamua kukushughulikia hawakosi sababu. Tazama jinsi walivyokuwa na urafiki na Osama lakini baadaye wakatofautiana na kumshughulikia hadi kumuua. Pia tusijitoe ufahamu jinsi Marekani alivyotafuta sababu za kuingia Iraki na hatimaye kumuua Sadam Hussein kwa kisingizio ambacho hakikuwepo. Sembuse Tanzania ambayo imeonyesha dharau ya waziwazi na kuituhumu Marekani kuwa imewatilia sumu na homoni za kishoga kwenye chakula.

Uropokaji kutoka mpuuzi na mshenzi mmoja tu unaweza kuligharimu taifa zima. Hivi Bashe kama huu msaada ungekuwa unapelekwa kwao Somalia angeukataa kweli? Amezoea kuwa ni wao tu wanahitaji msaada lakini watanzania wakipewa msaada anaona nongwa? Kunya anye kuku tu, akinya bata kaharisha?

Imefika wakati huyu mtu anyanganywe uraia na asafirishwe kwenda kwao kabla hajatuharibia nchi. CDF anahangaika na wahamiaji haramu wakati kuna mhamiaji haramu mmoja anataka kuichonganisha nchi na wahisani. Hivi huyu mtu anajua gharama za vita kutoka nchi yenye vifaa vya kisasa na mifumo mizuri ya kupigana? Ikitokea Marekani wakakinukisha na Tanzania yeye atakimbilia kwao. Je, sisi raia tutakimbilia wapi?

Tunapaswa kufahamu kuwa nchi zinaishi kwa kutegemeana. Hakuna nchi iliyojitosheleza kwa kila kitu. Hata Marekani kuna wakati wanahitaji misaada kutoka China, Japan, Uingereza, Urusi na nchi nyingine. Itakuwa Tanzania, nchi hohehahe isiyokuwa na mbele wala nyuma!

Sisi tunategemea karibu kila kitu kutoka Ulaya na Marekani. Chanjo na dawa zote za binadamu zinatoka Marekani. Mfano mzuri ni chanjo ya COVID-19. Chanjo hii kwa kiasi kikubwa imetoka Marekani na bado tunayo dozi ya kutosha inayoendelea kutolewa kwa watanzania bure. ARVs zinazotolewa bure kwa wagonjwa wa UKIMWI zinatoka Marekani. Hivi Marekani leo hii wakigoma kutoa ARVs wagonjwa wetu si watakufa? Nani ana uwezo wa kugharamia dawa hizi? Sio serikali wala wananchi wanaoweza kugharamia dawa hizi.

Sasa huyu mpuuzi anayetaka kutugombanisha na Marekani anataka watu wetu wafe kwa kukosa dawa au anataka nini hasa? Ikiwa dawa na chanjo zote hizi tunazitegemea kutoka kwa wazungu, je wangekuwa na nia ya kutuua nani angebaki salama? Chnjo zote ambazo watoto wanachanjwa tangu wakiwa wadogo zingekuwa na madhara si kila mtanzania angekuwa zombie? Kungekuwa na mtanzania hata mmoja mwenye akili timamu? Acheni kutafuta matatizo na wazungu huku ukijua bado huna uwezo wa kusimama mwenyewe.

Kana kwamba hili halitoshi, bado 60% ya bajeti yetu inategema michango na mikopo kutoka kwa wahisani. Je, wahisani hawa wakigoma kutuchangia kwenye bajeti tutajiendeshaje? Watu wengine wanajitoa ufahamu na kudai eti tunazo rasilimali za kutosha kujiendesha wenyewe. Rasilimali hizi tunazo tangu dunia hii ilipoumbwa lakini hatuna uwezo wa kuzichakata na kuzitumia. Mambo madogo kama ujenzi wa barabara na reli tunawatumia wazungu na wachina. Tunashindwa kutengeneza vitu vidogo kama vijiti vya meno na sindano. Huo uwezo wa kuchimba madini na kuchakata rasilimali nyingine tulizo nazo tutaupata wapi ikiwa tunashindwa kufanya mambo madogo kama haya?

Kama tuna jeuri ya kukataa msaada wa chakula, basi tusiishie hapo tu. Tukatae pia michango ya bajeti kutoka kwa wahisani na tukome kukopa mikopo ya maendeleo kutoka benki za wazungu (WB, IMF, etc). Ikiwa hatuwezi haya, tukae chini tutulize matako tuache chokochoko za kijinga wakati bado hatuna uwezo wa kusimama wenyewe kama nchi inayojitegemea.

Nawasilisha.

Tatizo Watanzania wanapenda sana story za mtaani. Halafu story ikishasambaa sana mtaani watu wakaamini hata viongozi wetu nao wanaiamini.

Miaka yote tumechanjwa chanjo. Watoto wetu wamechanjwa ... leo kuna watu wamekuja wanakuja na story kwenye chanjo ya Covid na watu wanaamini. Sasa mbona Tanzania ni wa kwanza kudai vyeti vya chajo ya homa ya manjano Airport. Kama wanakataa chanjo wazikatae zote mpaka za surua na ndui.

Sasa hili la mchele ndiyo kituko kabisa ... yaani mchele unamfanya mtu awe msenge ... seriously. Yaani hizo homons zimpikwe zitokote halafu mchele uive bado zipo tu ... hiyo science imekuja lini!!? Yaani watu kusikia kuwa kuna virutubisho tayari wanachanganyikiwa ... hawajui kuwa hiyo ni fortification ambayo imekuwa inafanywa kwenye vyakula vingi tu hasa vya watoto.

Yaani leo wanakataa unga wakati huo huo wanapokea maziwa ya unga na kuwavywesha watoto wachanga na toddlers na hakuna mtu anasema chochote. In fact Tanzania maziwa yote ya unga yanaagizwa toka nje. Sasa kama wanataka kutufanya mashoga nchi nzima si waweke kwenye maziwa ya unga, sukari au mafuta ya Korie!
 
Tatizo Watanzania wanapenda sana story za mtaani. Halafu story ikishasambaa sana mtaani watu wakaamini hata viongozi wetu nao wanaiamini.

Miaka yote tumechanjwa chanjo. Watoto wetu wamechanjwa ... leo kuna watu wamekuja wanakuja na story kwenye chanjo ya Covid na watu wanaamini. Sasa mbona Tanzania ni wa kwanza kudai vyeti vya chajo ya homa ya manjano Airport. Kama wanakataa chanjo wazikatae zote mpaka za surua na ndui.

Sasa hili la mchele ndiyo kituko kabisa ... yaani mchele unamfanya mtu awe msenge ... seriously. Yaani hizo hormos zimpigwe zitokote halafu mchele uive bado zipo tu ... hiyo science imekuja lini!!? Yaani watu kusikia kuwa kuna virutubisho tayari wanachanganyikiwa ... hawajui kuwa hiyo ni fortification ambayo imekuwa inafanywa kwenye vyakula vingi tu hasa vya watoto.

Yaani leo wanakataa unga wakati huo huo wanapokea maziwa ya unga na kuwavywesha watoto wachanga na toddlers na hakuna mtu anasema chochote. In fact Tanzania maziwa yote ya unga yanaagizwa toka nje. Sasa kama wanataka kutufanya mashoga nchi nzima si waweke kwenye maziwa ya unga, sukari au mafuta ya Korie!
Hapa ndipo watu wengi wanapojitoa ufahamu na kujifanya wajanja wakati kichwani ni weupe. Kama wana jeuri basi wakatae misaada ya wahisani kwenye bajeti. Yaani nchi hii ina vituko hadi inakera.
 
Waziri Bashe nadhani ameteleza kwa aliyoyasema. Ukweli ni kwamba bad Tanzania tunahitaji kill aina ya misaada kutoka nchi rafiki.

Suala hili la msaada wa mchele limetoa picha halisi ya alivyo Waziri na Serikali yake. Hivi msaada chakula hiki ungetoka Uarabuni kungekuwa na hoja hizi?

Ukweli ni kwamba, zamani Tanzania ilikuwa ni Nchi ya wakulima na wafanyakazi; lakini leo wafanyakazi ndio wamekuwa wakulima wakubwa na wale wakulima wa zamani wengi wao sio wakulima tena bali wamebaki kukodisha mashamba yao: kwa hiyo hawa wakulima wafanyakazi wanaona mchele huon kutoka Merikani unaweza kuadhiri bei ya mchele wao kuwa ndogo na hivyo kupata hasara.

Tuna saidiwa chakula bora bure, kwa ajili ya watoto wetu mashuleni, tunakataa lakini tunatumia $ nyingi kwa ajili ya kununulia chupi, shidiria na nguo zingine za mitumba: KWA KWELI HAIPENDEZI NA NI AIBU KWA TAIFA
Hiki ni kipimo kuwa nchi hii inatawaliwa na AKILI NDOGO kuliko tunavyoweza kudhani
 
Kataa mpaka internet tuone umeikataa Marekani kweli.

Internet imeanzishwa na mabeberu hawa Wamarekani na wameiwekea vitu vys kukuchunguza.
 
Hadi kompiuta tuzikatae mkuu
Kataa mpaka internet tuone umeikataa Marekani kweli.

Internet imeanzishwa na mabeberu hawa Wamarekani na wameiwekea vitu vys kukuchunguza.
 
Kama ni ule mchele ambao unakuwa umechanganywa na maharage fulani Jamii ya kunde, na chumvi n.k., ninaufahamu. Wamisionari fulani wa Kimarekani walikuwa wakiutoa kwenye shule fulani za Kanda ya Ziwa.

Kama ni huo, ni chakula kizuri tu. Binafsi nilishaula sana tu, pindi nikiwa Kanda ya Ziwa.

Hauhitaji kuungwa! Ni kuchemshwa tu, na kuliwa ukishaiva. Ukiamua kuweka viungo na "vikorombozwe" vingine ni uamuzi wako, lakini wenyewe ulivyo, umejitosheleza.

Kama ndiyo huo, Waziri amekosea. Kuna watoto wa Kitanzania wamekuwa wakiula kwa miaka mingi tu, na hawakuwahi kuonekana kuwa na shida. Ni chakula kizuri, kama ni huo mchele.
 
Ndio wenyewe mkuu. Hata mm nimeishaula sana tu. Namshangaa huyu msomali anakataa chakula sijui anataka nini.
 
Back
Top Bottom