Benki ya Dunia: Licha ya Uchumi wa Tanzania Kukua Lakini Haupunguzi Umaskini.Yashauri Ukuaji Uongozwe na Sekta Binafsi Badala ya sekta ya Umma.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,054
49,742
Benki ya Dunia imesema licha ya Ukuaji mzuri wa Uchumi wa Tanzania wa wastani wa Asilimia 5-7% Kwa miaka 20 Iliyopita umeshindwa kupunguza umaskini na idadi ya maskini Nchini Kwa kiwango kinachotakiwa.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia Tanzania Nathan Beleke amesema hayo wakati wa mapitio na tathmini ya kina ya sera za Uchumi za Tanzania na matokeo yake kwenye uchumi.

Bwana Beleke amesema Kwa miaka Mingi Sasa uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua Kwa msukumo wa Serikali yaani Public Investment hasa kwenye miundombinu lakini sio kukuza uchumi wa mtu mmja mmja(Private Sector) hivyo pamoja na takwimu kuonesha Ukuaji mzuri Kwa miaka Mingi ila Tanzania ni Kati ya Nchi Zenye idadi kubwa ya Watu maskini.

Bwana Beleke ametaka Serikali kubadili muelekeo na kubinafsisha Uchumi Kwa watu Ili Ukuaji ulete maana Kwa kuondoa umaskini na kupunguza idadi ya maskini(Inclusive growth).

Ameshauri vikwazo vyote vinavyozuia kukua Kwa sekta binafsi viondolewe ndipo uwekezaji wa Umma utaleta maana Kwa watu.

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1737111937610321930?t=Pub4rjj8SvTr2G5O828rWg&s=19

My Take
Naungana na bwana Beleke Kwa sababu haiingii akilini kuwekeza mabilioni kwenye mamiradi ya kupigia picha kama Sgr na kuacha sekta Zenye Mamilioni ya watu kama Kilimo na Ufugaji.

Hata hivyo naipongeza Serikali ya mama Kwa kuliona Hilo na kujikita zaidi kwenye kukuza sekta ambazo Zina watu wengi kama Kilimo na Ufugaji.

Aidha Rais Samia anajitahidi kuivuta sekta binafsi kadiri inayohitajika Kwa kuondoa vikwazo vya biashara Ili ifike mahala mtu aniskie fahari kujiajiri badala ya kuwaza Kuajiriwa na Serikali.

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1737715929407013051?t=UhjVZPkOOtGzCXT_-vSQmg&s=19
 
Back
Top Bottom