Danny Jully
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 4,416
- 3,860
Mkuu kwa upande wangu sijaona tatizo kubwa la mleta mada. Shetani akikuletea ujumbe mzuri, wewe pokea lakini umwache na ushetani wake. Lengo na kusudi la mleta mada hata kama ni ovu bado kuna ujumbe wa taadhari hapo.Tatizo sio mada bali ni mleta mada na kusudio la kuleta hii mada.
Tunataadharishwa hapo kwamba sasa tumekua, siyo watoto wa kubebwa bebwa tena. Mtoto akishakua kuna vitu anakosa kwa mama yake.
Kama nchi tumepanda daraja ambalo kuna vimisaada na mikopo tutakosa, kwa hiyo lazima tujipange kupambana na hiyo hali. Siyo rahisi sana kama tunavyodhani, lakini ndiyo hivyo mtoto akishaweza kutembea habari ya kubebwa inaisha. Kama nchi ni muhimu kujua hayo