Mwigulu Nchemba: Washirika wa maendeleo waridhishwa na uhusiano uliopo kati ya washirika na serikali ya Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200

MWIGULU NCHEMBA - WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UHUSIANO ULIOPO KATI YA WASHIRIKA NA SERIKALI YA TANZANIA​


01 Mar, 2024
WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UHUSIANO ULIOPO KATI YA WASHIRIKA NA SERIKALI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akihutubia wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam
wenye kaulimbiu:


  • Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050;
  • Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, .

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo endelevu.

Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo ngazi ya Juu.

Alisema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuwa na maendeleo endelevu ambayo hayamuachi Mtanzania yoyote nyuma kwa kufanya uwekezaji katika Sekta za Uzalishaji.

“Kipaumbele kimewekwa kwenye uwekezaji katika mtaji wa binadamu, maendeleo ya miundombinu, kuhamasisha ukuaji wa kiuchumi, kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii, utawala bora, kuwawezesha wanawake na uhifadhi wa mazingira”, alibainisha Mhe. Nchemba.

Alisema kuwa kwa kutekeleza mikakati hiyo pamoja na kukuza ushirikiano na sekta binafsi, asasi za kiraia na washirika wa maendeleo, Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa kuelekea kufikia ukuaji wa Uchumi endelevu.

Dkt. Nchemba alisema Serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha mazingira ya ukuaji wa biashara, kuongeza ushindani na kukuza ubunifu ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Dkt. Nchemba, alisema Tanzania pia inatumia Diplomasia ya Kiuchumi kama mkakati muhimu wa kuendeleza uchumi wake na kubainisha kuwa nchi ina dhamira kubwa ya kufuata kanuni za ushirikiano wa kimataifa wenye manufaa kwa pande zote.

Kwa upande wake, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. David Concar, alisema kuwa wadau wa maendeleo wanampongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoyafanya na wanayaona mabadiliko mbalimbali anayofanya katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, biashara pamoja na uwekezaji katika sekta ya uzalishaji.

Alisema kuwa wadau wa maendeleo wako tayari kuendelea kuiwezesha nchi kufikia maendeleo ya kukuza uchumi wa wananchi.

Mhe. Concar alisema wadau wa maendeleo wametoa zaidi ya Dola bilioni 2.7 kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo asilimia 51 ya fedha hizo ni misaada na asilimia 49 ni mikopo yenye masharti nafuu.

Alibainisha kuwa asilimia 40 ya fedha hizo zilitolewa na nchi moja moja za washirika wa maendeleo na asilimia 60 za fedha hizo zimetolewa na Taasisi za Kimataifa za fedha ikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)

Nao washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SRF, Prof. Fortunata Makene na Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Dk. Donald Mmari, walisema kuwa majadiliano hayo ni muhimu kwa maendelo ya nchi kwa kuwa yanaikutanisha Serikali na wadau wa maendeleo.

Mwisho
 
01 March 2024
Dar es Salaam, Tanzania

Tanzania's Strategic Dialogue Eyes Inclusive Growth, Embraces Mega Projects for 2024 Budget​

1709338499523.png

Senior cabinet ministers and development partners convened to unveil Tanzania's economic strategy for inclusive growth, focusing on agriculture, fisheries, and forestry.


Finance Minister Dr Mwigulu Nchemba unveiled the government's blueprint to bolster the economy through substantial investments in agriculture, fisheries, and forestry, sectors poised to bridge the poverty gap and promote public engagement in the nation's progress. This strategy aligns with Tanzania's long-term vision, aiming for resilience in an uncertain global landscape.

Building an Inclusive Economy Through Agriculture​

Dr Nchemba emphasized the government's commitment to making the economy more inclusive by focusing on agriculture and related sectors. By tapping into these areas, the government aims to empower the majority of the population, thereby tackling poverty head-on. The Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP), soon to be operational, is a testament to this commitment. It's expected to significantly improve electricity supply, further bolstering agricultural productivity and economic growth.

The dialogue, themed 'Towards Vision 2050: Accelerating Resilience and Inclusive Development in Times of Uncertainty', highlighted the government's focus on reducing economic disparities. Investment in production sectors, according to Dr Nchemba, will not only mitigate employment challenges but also fortify the private sector, creating ample opportunities for the youth. This approach seeks to balance economic growth with environmental sustainability and social inclusiveness, preparing Tanzania to navigate global uncertainties more effectively.

Enhancing Business Environment and Fostering Private Sector Growth​

REPOA Executive Director Dr Donald Mmari pointed out the significance of improving the business environment to ensure the Tanzanian economy grows in a more inclusive, competitive manner. Investment in infrastructure and the fostering of private sector growth are crucial for attracting foreign direct investment (FDI) and creating jobs. The successful completion and operationalization of the JNHPP are expected to alleviate foreign exchange shortages, particularly in USD, marking a pivotal step towards economic stability and growth.

As Tanzania strides towards its Vision 2050, the concerted efforts in making the economy more inclusive and resilient are promising. The strategic investments in key sectors, coupled with the anticipated benefits from the Julius Nyerere Hydropower Project, set a solid foundation for sustainable development. This holistic approach not only aims at economic growth but also ensures that the growth is shared by all, making Tanzania a beacon of inclusive development in uncertain times.
 
Back
Top Bottom