BAVICHA Ifukuze waasi wote - Ben Saanane

BAVICHA Ifukuze waasi wote - Ben Saanane

Mimi sihafiki kufukuza mtu chamani kabisa tunajua vijana wengi nikiwepo mimi tunakua na matamanio mengi sana ya kufanikiwa haraka kimaisha kupata pesa kuendesha gari nzuri,nyumba nzuri na vinginevyo.

Inawezekana kabisa mtifuano huu ulianza kwenye uchaguzi wa bavicha vijana mnawasema mwanzo walikua na malengo mazuri sana kwa chama nilikua nafanya research zangu toka 2010 kwenye uchaguzi misimamo yao ilikuaje.

Lakini baada ya uchaguzi wa bavicha msimamo ikabidilika vijana wawili mnawasema walikosa ubunge 2010 ukafuata uchaguzi wa bavicha ambao wengi wao wanalalamika hakua huru na wa haki rushwa ilitawala wengine wakafutwa majina.

Sasa kama tatizo lilianzia bavicha ina maana viongozi na wazee wa chama wanaweza kuwapa onyo kali kuwafutia vyeo vyao na wakabaki wanachama wakawaida tu ndani ya chama.

Ukipita kwenye post zao facebook utaona kuna chuki ya wazi dhidi ya Dr slaa,john mrema ipo chuki ya wazi kabisa inafikia kipindi mchange anahoji watu walioenda kwenye harusi ya john mrema kweli hii chuki ni mbaya sana.

Nakukumbusha tu ndugu yangu ben saanane chama kiliwafukuza vijana kina kafulila na wenzake tulipoteza seat tatu za bungeni ambazo zilienda NCCR.lazima tufanye uamuzi sahihi fukuza fukuza haisaidii kitu.

Hawa ni vijana wengi hawajafika 30 kuna muhemuko fulani wa matamanio wengi hawajapevuka vichwani kujua kwenye siasa lazima mshindi awepo.tunachopaswa kufanya ni kuwaweka chini kuwarudisha kwenye mstari.

Kumchafua katibu wako mkuu kina mchange na shonza na mwanampamba haitasaidia kujenga chama kwanini umebadilika baada ya uchaguzi wa bavicha mwanzo mlikua kwenye momentum nzuri sana.

Najua mtapita hapa ni wakati wa kurudi na kutulia vijana tujenge chadema imara sehemu zote kuna matatizo na tunapo yamaliza matatizo ndo tunasimama imara naombeni sana mrudi kundini.

Ikishindikana kubadilika chama kiwafutie vyeo vyao vyote ndani ya chama lakini si kufukuza mtu ndani ya chama narudia tena sio kuwafukuza ndani ya chama.mtoto akikunyea mkono unafuta au unaukata mkono.

Hawa ni vijana wazuri sana kama watarudi kwenye mstari na kusamehe yaliyopita na kuacha chuki za ajabu kwenye social network.chama kinawahitaji sana kina mchange,mwampamba na shonza nina uhakika wakirudi kwenye mstari watashinda majimbo yao.

Tunapofanya maamuzi tukumbuke ujana ni kipindi kibaya sana kwa mwanadamu kama utakupeleka vibaya waswahili wanasema ujana majimoto,hivyo tuwarudishe kwenye mstari hawa vijana ni kweli wanatukana viongozi wao lakini kuna tatizo wabadilike wapewe onyo na chama kisifukuze mtu.

Ujana maji ya moto kweli unaweza ukadanganyika kwa trip za nje,kupewa wanawake wazuri,pesa,gari,kazi ukasahau chama chako ccm haishindwi kukupa hivyo vitu wao si wana dola bana watashindwaje.

Fukuza haitajenga chama
Warudishwe kwenye mstari

N.B ujana maji ya moto tufanye maamuzi sahihi bila kumuonea mtu

Fred kavishe

mIMI nimekusoma ushauri wako ni sawa na wa mzee BUTIKU aliotoa jana pale mlimani.Kufukuza si dawa na unaowafukuza ni watoto wadogo, ni lazima chama kijifunze kulea vijana watutkutu na kuweza kuwabadili taBIA na baadae kuwa viongozi.Nyerere angefuata ushauir kama huu leo hii SAMUEL SITTA asingekuwepo katika siasa na uongozi.Natoa ushauri kwa DR.SLAA kuwa mvumilivu wewe ni baba wa wote leo wanaokushauri ufukuze kesho watasema tulijua huyu babu ni mkorofi.
Tunakubali inapobidi fukuza lakini si kila wakati tunakujua DR.wewe ni chuo cha mafunzo wengi wamepita kwako japo leo wanakutukana.Tunakusubiri magogoni so you can excel your charisma
 
Mamluki wengine wako humuhumu wameshaanza kujitetea, kwamaana ccm waliwapa advance tuu ya hela, wakifanikiwa wakachukue tena mshiko.tumbu tupu na siasa sijui kama vitatufikisha
 
Anzeni na kile kirusi kilichokiri bado kinamiliki kadi ya CCM; msianze na matawi kateni shina ili mutibu ugonjwa!
Hivi mtu akipokea malipo ya kadi ya mwanachama wa chama cha upinzani/kingine hajavunja tu katiba ya CCM? Inawezekana ni mwelekeo wa CCM kuvunja katiba yake na ya nchi (for survival) nieleze/nielemishe kama huo si ugonjwa usio na tiba? Nashauri mtafakari na muanze matibabu au kifo kitawaumbua.
 
Hivi Dr Slaa ukitokea hadharani na kuomba samahani kuwa ulifikiri kuwa na kadi ya CCM ambayo hukuwa unailipia ni kama kumbukumbu tu utakuwa unakosea? Mbona Bill Clinton alikiri kulala na Monica Lewinsky akaomba samahani na mambo yakaendelea. Sasa wewe ndugu yangu umekomaa na ukimya wako hutaki kujutia dosari hii, naona ni kama inaendelea kukumaliza, be careful.
 
Ni sawa na kuushauri mzoga uombe msamaha kwa fisi. Hii ni dosari ni kwa macho ya mbao ya CCM ambayo yanakodoa lakini hayaoni.
 
Ni sawa na kuushauri mzoga uombe msamaha kwa fisi. Hii ni dosari ni kwa macho ya mbao ya CCM ambayo yanakodoa lakini hayaoni.

Naona hujanielewa wewe. But for your information mimi ni mmoja wao wa wengi watakaohama CDM kama Dr Slaa hatajutia dosari ya kuwa na kadi ya Magamba, fullstop.
 
Hivi Dr Slaa ukitokea hadharani na kuomba samahani kuwa ulifikiri kuwa na kadi ya CCM ambayo hukuwa unailipia ni kama kumbukumbu tu utakuwa unakosea? Mbona Bill Clinton alikiri kulala na Monica Lewinsky akaomba samahani na mambo yakaendelea. Sasa wewe ndugu yangu umekomaa na ukimya wako hutaki kujutia dosari hii, naona ni kama inaendelea kukumaliza, be careful.
Avanti, Hizi ni propaganda tu wala usiwe nazo serious .....ni propaganda za magamba...sio lazima kuumiza akili na propaganda....Dr anaweza akawa nayo au asiwe nayo...is not an issue....ila kwa uhakika dr hawezi kulipia hizo kadi....Kwa common sense tu kama dr angekua pandikizi lao hata wasingepiga mayowe..wangetulia coz wanajua tafanya kazi yao....sasa mayowe ya nini
 
Last edited by a moderator:

Mkuu haiwezekani Dr Slaa achukue kadi yangu ya CCM mbele ya hadhara kubwa vile na kwa mbwembwe mnooooo wakati yake kaiweka kwapani, kuna nini? Si bora angeniachia na yangu iwe kumbukumbu?
 
Naunga mkono hoja. Hata jimboni kwetu Ukonga kuna tetesi ya kiongozi mmoja wa Bavicha kununuliwa na uongozi wa CCM wa wilaya. Nasikia wanaandaa siku ya mapokezi yatakayoshirikisha viongozi wa wilaya wa CCM na hotuba yake ya kuitukana CHADEMA imeshaandaliwa. Sisi tunafuatilia suala hili kwa karibu.

Vile vile kinachotusikitisha ni kwamba, kabla ya kwenda CCM alienda makao makuu na kuchukua kadi 200 za CHADEMA, sijui wana malengo gani.

Hawa watu wanatusumbua sana ndio maana nasema nakubaliana na pendekezo la Saanane, hivi virusi viondolewe.

Kamanda Michael

Tuwasiliane. Niko concerned na suala la kadi. Kuna vitu ni vyema ukasaidia kwa kutoa maelezo ya kutosha kadri unavyojua kwa upande. Nitaku-pm kaka.
 
...wanao nuka harufu ya lile gamba, gamba chakavu lenye rangi ya kijani na picha ya jembe na nyundo, jembe kuzika fikra za mabadiliko na nyundo kupigilia msumali demokrasia ya kweli.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Du! Mtoi.
 
Mkuu haiwezekani Dr Slaa achukue kadi yangu ya CCM mbele ya hadhara kubwa vile na kwa mbwembwe mnooooo wakati yake kaiweka kwapani, kuna nini? Si bora angeniachia na yangu iwe kumbukumbu?

Unajua haya ni matokeo ya cheap politics za kadi....Ishu it has to be matendo...leo hii mimi naweza kuwa na kadi hata za vyama vyote hapa Tz....Is it an issue? Issue ni itikadi ipi ambayo unaiamini...Ukitaka kuona hii ni mere propaganda ambayo mtu mwenye upeo hutakiwi kupoteza mda jiulize...Dr amekua mbunge wa karatu foo years in Chadema,amekua ni mtu anayesimamia upinzani kweli kweli.....Leo hii yeye kama kweli ana kijikaratasi chenye rangi ya kijani...is it a big issue worth of discussion nzito...come on pal
 
Kuweni macho na mapandikizi kwenye chama, kadi kwa taarifa yenu wakati wa chama kimoja kila mtu alitakiwa kuwa na kadi ya ccm na lazima kuaoma miezi mitatu, vinginevyo hupati nafasi chuo, ama kazi, baada ya vyama vingi na yote yanayokemewa na vyama vya upinzani mtu kuwa na kadi asiyoilipia sio hoja ya msingi.
Tuangalie chadema na vyama vingine viko wapi, kutetea maslahi ya wananchi. Pingo
 
Hii siasa ya Tabwe style nimechoka nayo. Nchi iko hoy bin taaban kiuchumi still chama kilichowafikisha raia hapo walipo kimebaki na mzaha wa mtu kuwa na kadi yao. Hizi siasa za namna hii zipelekeni kwa ile jamii ya stone age. Tunachotaka kutoka kwa watawala ni jinsi ya kujikwamua kiuchumi ktk tope walilotunasisha.
.
 
Naunga mkono hoja. Hata jimboni kwetu Ukonga kuna tetesi ya kiongozi mmoja wa Bavicha kununuliwa na uongozi wa CCM wa wilaya. Nasikia wanaandaa siku ya mapokezi yatakayoshirikisha viongozi wa wilaya wa CCM na hotuba yake ya kuitukana CHADEMA imeshaandaliwa. Sisi tunafuatilia suala hili kwa karibu.

Vile vile kinachotusikitisha ni kwamba, kabla ya kwenda CCM alienda makao makuu na kuchukua kadi 200 za CHADEMA, sijui wana malengo gani.

Hawa watu wanatusumbua sana ndio maana nasema nakubaliana na pendekezo la Saanane, hivi virusi viondolewe.

Mkuu Michael P Aweda mbona mnatia mashaka? inakuwaje viongozi wenu wananunulika kirahisi hivyo? Vijana wananunulika, wazee wananunulika sasa manusura ni nani hapo?

Hili suala la kusema huyu kanunuliwa na yule kanunuliwa (hasa viongozi) sioni kama lina tija sana kwani linaki expose chama kwamba viongozi wake wanaweza kununulika. Ingekuwa vyema kama mngekuwa mnachukua hatua kimya kimya badala ya kutangaza kwamba wamenunuliwa. Hii ya viongozi wenu kununuliwa will work against your party.

Nakala Ben Saanane Molemo
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Mwanasiasa kijana ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye nyota yake iko juu Ben Saanane amelitaka Baraza la vijana CHADEMA BAVICHA kuwafukuza waasi wote wanatumiwa kukihujumu chama.

Namnukuu:

Naomba kutofautiana na wachangiaji walio wengi ndani thread hii, nachokiona mimi ni kuwa ndani ya BAVICHA kuna mgongano wa kimaslahi na zaidi maslahi ya kifedha, inavyoonekana kuna kundi moja linafaidi zaidi fedha za chama kwa kujipa safari za kuzunguka Nchi nzima na kundi la pili ambalo halina safari hizo na zaidi linahoji uhalali wa matumizi ya fedha kwa baadhi ya viongozi wa BAVICHA na matokeo halisi ya ziara zao za kila siku.

Ni vizuri watu wasiingizwe mkenge kwa kushabikia tu, makundi haya mawili lazima yataanza kuhujumiana kwa kutungiana tuhuma, na ni wazi kundi litakaloibuka washindi ni lile lenye mafungamano na magazeti kama Tanzania daima nk.CHADEMA wawe makini sana wasipoweza kuweka mipango yao sawa watawakwaza wapenda mabadiliko kwa kukumbatia watu wanaojipendekeza kwa mwenyekiti na katibu mkuu na kuwazushia wenzao tuhuma kila kukicha.Inavyoonekana ndani ya chadema ni viashiria vya tabaka la kiuongozi mwenye macho anaweza kuona, tujadili kwa manufaa ya Taifa na mabadiliko na sio kwa ubinafsi na ushabiki.
 
Naona hujanielewa wewe. But for your information mimi ni mmoja wao wa wengi watakaohama CDM kama Dr Slaa hatajutia dosari ya kuwa na kadi ya Magamba, fullstop.

unasubiri nini? Si uhame hata sasa.
 
Naomba kutofautiana na wachangiaji walio wengi ndani thread hii, nachokiona mimi ni kuwa ndani ya BAVICHA kuna mgongano wa kimaslahi na zaidi maslahi ya kifedha, inavyoonekana kuna kundi moja linafaidi zaidi fedha za chama kwa kujipa safari za kuzunguka Nchi nzima na kundi la pili ambalo halina safari hizo na zaidi linahoji uhalali wa matumizi ya fedha kwa baadhi ya viongozi wa BAVICHA na matokeo halisi ya ziara zao za kila siku.

Ni vizuri watu wasiingizwe mkenge kwa kushabikia tu, makundi haya mawili lazima yataanza kuhujumiana kwa kutungiana tuhuma, na ni wazi kundi litakaloibuka washindi ni lile lenye mafungamano na magazeti kama Tanzania daima nk.CHADEMA wawe makini sana wasipoweza kuweka mipango yao sawa watawakwaza wapenda mabadiliko kwa kukumbatia watu wanaojipendekeza kwa mwenyekiti na katibu mkuu na kuwazushia wenzao tuhuma kila kukicha.Inavyoonekana ndani ya chadema ni viashiria vya tabaka la kiuongozi mwenye macho anaweza kuona, tujadili kwa manufaa ya Taifa na mabadiliko na sio kwa ubinafsi na ushabiki.

Ni kweli, BAVICHA inaonekana kuwa na Viongozi wawili tu yaani HECHE na MUNISHI. Ni majembe ambayo yanajitahidi kuinga'arisha BAVICHA likini yapo mapakashume yanayopambana nao huku wakijidai wao nao ni BAVICHA. Naweka picha hapo chini kuonyesha jinsi majembe haya yanavyojituma

HECHE NA MUNISHI WAKIWA MAENEO TOFAUTI YA NCHI KWA KAZI ZA UHAMASISHAJI WA VIJANA

[TABLE="class: cms_table, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema (BAVICHA)John Heche akihutubia umati wa watu Mkoani Tunduma ambapo wanachama wengi wa CCM wakiwemo wa UVCCM walirudisha kadi zao za kujivua UCCM na kuhamia Chadema.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Katibu mkuu wa Bavicha Bw, Deogratias Munishi akipokea kadi ya kujivua uanachama wa UVCCM kutoka kwa Mwanachama wa UVCCM mkoani Rukwa jimbo la Mpanda Vijijini.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: cms_table, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Munishi anamwaga Sera Kahama[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Jihadharini lakini. Msije mkafukuza watiifu katika chama kwa kudhani ni mamluki na kuwaacha mamluki wenyewe! Hapo itakuwa hatari.

Hawa huwa wanajulikana wazi. Kwa hiyo usiwe na shaka kwa hilo. WATIMULIWE MAPEMA. KAMA ILIWEZEKANA KWA MADIWANI WAASI SEMBUSE HAO.

TUNZENI MAADILI KULIKO KITU CHOCHOTE KINGINE katika BAVICHA na Chama kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom