BAVICHA Ifukuze waasi wote - Ben Saanane

BAVICHA Ifukuze waasi wote - Ben Saanane

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Mwanasiasa kijana ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye nyota yake iko juu Ben Saanane amelitaka Baraza la vijana CHADEMA BAVICHA kuwafukuza waasi wote wanatumiwa kukihujumu chama.

Namnukuu:
Let me speak loud and clear...BAVICHA sasa ni muda wa kuwafukuza wale wote waliothibitika kuihujumu CHADEMA kwa kulipwa na viongozi wa CCM.

Nitaunga mkono HATUA KALI za kinidhamu na KISIASA zitakazochukuliwa dhidi ya vijana hawa wajinga....hatuwezi kukumbatia Mediocre.

Let them face the consequences...Wepesi.
 
Naunga mkono hoja. Hata jimboni kwetu Ukonga kuna tetesi ya kiongozi mmoja wa Bavicha kununuliwa na uongozi wa CCM wa wilaya. Nasikia wanaandaa siku ya mapokezi yatakayoshirikisha viongozi wa wilaya wa CCM na hotuba yake ya kuitukana CHADEMA imeshaandaliwa. Sisi tunafuatilia suala hili kwa karibu.

Vile vile kinachotusikitisha ni kwamba, kabla ya kwenda CCM alienda makao makuu na kuchukua kadi 200 za CHADEMA, sijui wana malengo gani.

Hawa watu wanatusumbua sana ndio maana nasema nakubaliana na pendekezo la Saanane, hivi virusi viondolewe.
 
Ni vyema kweli kuwaweka kando mamluki walio ndani ya chama kwani wanafifisha nguvu ya mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.
wamekuwa wepesi kununuliwa na magamba na kuyumbishwa na propaganda.
 
Ni kutimua tu Bora chama kibakie na wanachama hata 100 lakini wenye spirt ya ukombozi na sio kuwa na wanachama wachumia tumbo, tena wakati wa kuwatimua ni sasa kabla hata ya 2014
 
Huyu Habibu Mchange na Shonza Juliana ni virus vinavyohitaji KASPERSKY
 
Ben
You have said all my brother.
Chadema huu ni wakati sasa wa kuwafukuza hawa waasi.Ni vizuri watimuliwe muda huu kabla hatujafanya uchaguzi wa ndani ya chama.

Hiki kikundi cha waasi kinajulikana kwa muda sasa kifukuzwe ili wapate muda mzuri wa kuitukana Chadema wakiwa huru kule CCM kuliko sasa wanavyoichafua Chadema kupitia mitandao.

Ni wakati sasa wa John Heche na kamati yake kuwafukuza hawa wahuni ndani ya Bavicha na chama kitamalizia
 
hivi kwa nini Zitto hajawahi kukemea vijana mamluki ndani ya CHADEMA?
 
Bavicha kuna uozo sana kwanza sijaona kazi walio ifanya mpaka sasa,mambo yote niheche pekeyake,viongoz wengind hata majina siwajui,heche analazimika kuzunguka nch nzima wenzie wamekaa tu.vijana wa Tz wanaijua BAVICHA?

Na wengine ni wajumbe wa kamati kuu wanadiliki kumtukana dr wazi wazi hivi watu wasio na nidham wana nafasi gani katika CHADEMA?timuwen wote wataka vyeo na waingia tamaa na wasaliti,Mbowe na Dr. Slaa ni majembe na wanaongoza vema ila kuna wajinga wajinga wanataka kufanya CHADEMA nikama CCM. Viongoz wajuu fukuzen hao bana maana huku mtaan CHADEMA nikila upande msihofu kuchukua maamuz magumu fanyeni kama katiba ya CHADEMA isemavyo CHADEMA ni chama tawala ifikapo 2015,ila tutapitia mabonde mengi sana tusife moyo ushind ushafika
 
Jihadharini lakini. Msije mkafukuza watiifu katika chama kwa kudhani ni mamluki na kuwaacha mamluki wenyewe! Hapo itakuwa hatari.
 
Mwanasiasa kijana ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye nyota yake iko juu Ben Saanane amelitaka Baraza la vijana CHADEMA BAVICHA kuwafukuza waasi wote wanatumiwa kukihujumu chama.Kijana huyo machachari ameweka wazi msimamo wake kwenye Facebook Wallpage yake kama inavyoonekana hapa chini:

Ben Wa Saanane

Let me speak loud and clear...BAVICHA sasa ni muda wa kuwafukuza wale wote waliothibitika kuihujumu CHADEMA kwa kulipwa na viongozi wa CCM.Nitaunga mkono HATUA KALI za kinidhamu na KISIASA zitakazochukuliwa dhidi ya vijana hawa wajinga....hatuwezi kukumbatia Mediocre.Let them face the consequences...Wepesi.
Haya ndiyo nilisema Jana .Nilisema nilichokuwa najua.Bavicha come out get all sacked .Ongezeni ulinzi ulinzi kwenye documets za Chama .Vijana simamemi imara chukua hatua tuone madhara tujipange.
 
Wat goes arround comes arround.......nilidhani huku hakuna kucheka na kima kumbe ni yale yale ya kulalamika tuuuuuu.......

Kama M4C na nguvu yote hii hawawezi ku deal na a patch on cloth (inside job) mpaka watu machachari na wenye nyota zilizo juu kisiasa walalamike kwa walls......je kwa nguo nzima????????


Inquisitively waiting............................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Naunga mkono hoja asilimia 100% ni bora lawama kuliko fedheha naitamani sana iyo siku ya kiama cha Hawa mamluki
 
Naungana na kamanda Ben! Wasaliti wote niwa kufukuza ingali bado asubuhi, hatuwezi kuvumilia watu wachache wenye tamaa na vipande vya fedha wadhoofishe nguvu ya mabadiliko kwenye chama, wakizidi kuachwa watakuja kukiumiza chama zaidi kuliko wanavyofanya sasa kupitia vitabu vyao vya sura (FB). Hili limekemewa wakati unao faa, ni bora wachague pakwenda ili wachache tutakao baki tujue mkondo sahihi wa kukivusha chama.

Tumesha anza kuwatambua kwa matendo yao, wanazidi kujivua nguo, wamebaki watupu na tupu zao zina dondosha funyo wanao nuka harufu ya lile gamba, gamba chakavu lenye rangi ya kijani na picha ya jembe na nyundo, jembe kuzika fikra za mabadiliko na nyundo kupigilia msumali demokrasia ya kweli.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Waanze na katibu mamluki mwenye uanachama wa vyama viwili.Halafu waje kwa Heche asiyefanya kazi zake bali kuwa bendera wa Viongozi wa chama
 
Mkuu hizo kadi 200 ndio anataka awape CCM ili Akikamilisha mpango wake na watu wake aseme CCM kupitia yeye imevuna wanachama 200 wa CHADEMA poor politics tumewajua hawata tusumbua



Naunga mkono hoja. Hata jimboni kwetu Ukonga kuna tetesi ya kiongozi mmoja wa Bavicha kununuliwa na uongozi wa ccm wa wilaya. Nasikia wanaandaa siku ya mapokezi yatakayoshirikisha viongozi wa wilaya wa ccm na hotuba yake ya kuitukana Chadema imeshaandaliwa. Sisi tunafuatilia suala hili kwa karibu.
Vile vile kinachotusikitisha ni kwamba, kabla ya kwenda ccm alienda makao makuu na kuchukua kadi 200 za chadema, sijui wana malengo gani.Hawa watu wanatusumbua sana ndio maana nasema nakubaliana na pendekezo la Saanane, hivi virusi viondolewe.
 
Imetosha,Chadema watuoneshe wataweza kusimamia serikali kwa ukali! Charity begin at home!
 
Greenwhich
Asante sana kwa kuleta bandiko hili.Niliwahi kutoa mada hapa jamvini kuhusu uwezo wa Ben Saanane.Hakika nimefurahishwa na jinsi alivyotoa hili tamko kali bila kuangalia mtu usoni.

Chadema wakitaka kufika mbali inatakiwa wachukue maamuzi magumu tena sana.Chadema wanapaswa kujua kukamata ikulu sio kazi rahisi kama wengi wanavyodhani.

Inatakiwa Dr Slaa afuate siasa za Raila Odinga wa Kenya.Raila hacheki na kenge na ndiyo maana anaukaribia urais wa Kenya sasa.Wale wote waliokuwa wanakwamisha njia ya Raila hasa kwa usaliti walitupwa nje.

Chadema iachane kabisa na kulea wahuni,watu wajinga kabisa ambao vitendo vyao vinawastahili kufungiwa jiwe kubwa la kusagia na kutupwa baharini.
 
CCM mipango yao yote hujulikana mapema . Nawahurumia wanaohamia CCM kwa kununuliwa maana ndo kisiasa wamekwisha. Ni tendo moja tu Dume hutupwa chooni tena kwenye taka ngumu
 
Back
Top Bottom