Sakata la kupotea kwa Ben Saanane

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
Jana kikundi cha Bavicha kiitwacho UTG kilifanya mkutano na wanahabari kuhusiana na suala ya Ben Saanane, kiukweli Mimi Kama Mtanzania mpenda amani niliposikia UTG wanaongelea kuhusu suala la kamanda Ben nilijawa na Shauku kubwa kutaka kujua Kama wamepata angalau fununu alipo kijana huyu wa kitanzania.

Kilichonishangaza baada ya kupitia taarifa yao kwenye Mitandao ya kijamii Pamoja na vyombo vya Habari nikakuta porojo zilezile Za Akina Mbowe, Lissu, zitto kabwe na Joseph selasini ambazo siku zote tunazisoma kwenye Mitandao na media.

Suala la Saanane limekuwa LA kutupiana Mpira Kati ya polisi na chadema bila kupata ufumbuzi alipo kijana huyu.

Tutakumbuka Kuwa wakati Ben Saanane anatoweka Akina Mh Freeman Mbowe walikuwa na Safari Katka nchi za Jumuiya ya ulaya lakini sambamba na ilo ndicho kipindi ambacho Mh Tundu Lissu aliibuka na neno dikteta uchwara. Kuna Tetesi isiyo rasmi lakini ambalo linaweza kuwa na mashiko kwa kiasi kikubwa.

Tetesi Hizo kutoka kwa chanzo kilicho Karibu na uongozi wa CHADEMA, kinasema kuwa wakati Akina Mbowe na timu yake wanaenda ulaya kuomba Misaada walitafuta kitu ambacho wangekitumia kwa wafadhili wao kuhusu kuminywa kwa demokrasia Hapa nchini ndipo walipokubaliana na kamanda Ben Saanane kuwa ajifiche kwa Ahadi ya kulipwa pesa mpaka watakaporudi.

Tetesi Hizo zinadai baada ya Akina Mbowe kufika Ulaya hawakupta mafanikio kama walivyotarajia Matokeo yake waliporudi wakamtaka Ben ajitokeze lakini inasemekana kijana huyo akagoma akidai mpaka Mbowe atimize Ahadi yake.

Katika press conference ya Jana ya vijana wa Bavicha kupitia taasisi yao ya UTG Nilitegemea kusikia wakisema juhudi binafsi ya Chama kumtafuta Ben Saanane kupitia kitengo cha intelejesia ya Chama angalau kutupa Mwanga alipo Ben Saanane.

Tukumbuke Mbowe kwa kinywa chake Amewai kukaririwa akidai Ben Saanane katekwa lakini hawa vijana wa UTG wameshindwaje kukaa na mwenyekiti wao angalau awajibu maswali machache.

Ben alitekwa liini wapi na Akina Nani amewekwa wapi Nani aliyemwambia kuwa Ben katekwa na yeye amechukua hatua gani? Kwasababu Kama hao watu wanaweza kumwambia kutekwa kwa Ben Saanane vilevile lazima watamwambia alipo Ben na kisa Cha kutekwa.

Tukumbuke Ben Saanane ni katibu myeka wa Mkiti wa Taifa wa chadema mh Freeman Mbowe.

Inaaminika kuwa Ben Saanane ni moja wa vijana wa intelejesia ya chadema aliyepelekwa Israel na Chama kusomea ujasusi kwa mantiki hiyo kitengo cha intelejesia ya Chama kina taarifa gani kuhusu kupotea kwa mwenzao Ben Saanane na wamefanya juhudi Zipi kuhusu kupatikana kwa Ben Saanane?

Lakini pia kwa busara ndogo UTG hawakupaswa kupuzia hata kidogo taarifa iliyowai kutolewa na gazeti la mwanahalisi kuwa Ben Saanane hajatekwa Bali amejificha mwenyewe kwa kusudi la kusaka madaraka ndani ya Chama.

Nadhani sasa muda wa muafaka kama kweli Mbowe alimuhaidi Ben Saanane pesa kufanikisha mkakati ya Misaada kwa jumuiya ya ulaya Basi amlipe ili wazazi wake watoke kwenye simanzi lakini Kama hatafanya ivyo Naona aibu kubwa itakuja kuwapata chadema very soon.

Tangu kamanda Ben Saanane apotee chadema wamekosa great thinker wa kuandaa operation.

Katika hili tuache siasa mwambieni mh Freeman Mbowe amlipe dogo Haki yake.

La sivyo atuambie Ben alitekwa na Akina Nani? Wapi kwa kosa gani? Aliambiwa na Akina Nani na alichukua hatua gani?

Kama kweli nyie ni kizazi Cha kuhoji muwafikishie viongozi wenu Pamoja na Akina Munisi, Mushi na wengine alipo Ben Saanane wasije wakamfanya kama Chacha Wangwe na Alphonse mawazo.

Na Frey Cosseny
 
Kwa maelezo hayo,hiyo ni kazi ya polisi kumtafuta Ben eidha kwa kumhoji Mbowe kama ulivyo eleza au Mwanahalisi kwa jinsi walivyo ripoti juu ya Ben.Lakini polisi wanaona ugumu gani kumtafuta Ben?Ili akipatikana ujulikane ukweli wa nani alimteka?Serikali ina kigugumizi cha nini kumtafuta raia wake kama haihusiki?Tuache porojo kwenye uhai wa mtu
 
Chadema wana kitengo cha intelejesia wamefanya juhudi Zipi kumtafuta mwenzao? Je Kama chama wamefanya nini kuhusu kupatikana kwa Ben Saanane? Naona marafiki zake na UTG a. K. A UTI Ndiyo wanaoangaika Vipi? Mbona Ney WA mitego tuliona mawakili Walipelekwa polisi kwa nyodo Vipi kWA Ben Saanane Kulikoni kigugumizi?
 
Roma alipotea wasanii na wadau wao wakapaza sauti, sauti ya juu kabisa hadi Roma kapatikana.

Ben kapotea miezi sasa, chadema na wadau wao hawajapaza sauti, na kama wapepaza hiyo sauti, ni ya chini na pengine haikusikika.

great

siamini kabisa eti CDM imekomaa kumtafuta Ben saa nane
 
Na Roma alivyopotea mlisema mbowe watu wakapiga kelele bashite yakamgusa akatuahidi kumleta na akamleta sasa sjui tutakuamin hivyo?
 
Kwa maelezo hayo,hiyo ni kazi ya polisi kumtafuta Ben eidha kwa kumhoji Mbowe kama ulivyo eleza au Mwanahalisi kwa jinsi walivyo ripoti juu ya Ben.Lakini polisi wanaona ugumu gani kumtafuta Ben?Ili akipatikana ujulikane ukweli wa nani alimteka?Serikali ina kigugumizi cha nini kumtafuta raia wake kama haihusiki?Tuache porojo kwenye uhai wa mtu

Polisi wanaanzaje? wana report ben kapotea? nani alifungua jalada? wapi? askari mpelelezi ni nani? na majibu ya polisi ni yapi?

wazazi wa Ben wamesema polisi wametoa majibu gani? polisi wamemuhoji mbowe? wamemuhoji kubenea?

kwa nini wengi mmevutika na hili ambalo inaonekana wazi kuna gap sehemu fulani au habari ambayo ni hidden??

unaona presha ya mbowe iko sawa kabisa kumtafuta msaidizi wake? hauoni anajua yuko wapi?
 
Imani na mbowe ilinitoka tangu siku alipohusishwa na kuitwa kuhojiwa kuhusu suala la madawa. Kiukweli ni makosa yalitumika kwanjia aliyotumia makonda.
Lakini kwa uzito wa suala la madawa na athari zake kwa taifa. Yeye kama kiongozi mkubwa wa upinzani angetumia hekima tu na kukubali kwenda kuhojiwa ili kutoa ushirikiano wake. Ngwajima ni mtu makini sana mana yeye alikubali kuenda akahojiwa na akapimwa na ukweli ukabainika na mpaka sasa hakuna anaye mtilia shaka. Lakini huyu yeye kakimbilia mahakamani mapema sana ili akapate kinga ya mahakama.
Kitu hiki sisi wengine bado kinatutia shaka hadi leo. Aliogopa nini kwenda kule kuhojiwa hata kama ni kweli sio njia sahihi?
Alafu na chadema nao wamemkingia kifua moja kwa moja bila uchunguzi wowote kuhusu tuhuma zile.( inamaana anaaminiwa 100% ) hili linatia shaka sana kwa wale wafuatiliaji wa mambo.

Ubabe wa mbowe katika chama hasa ukichukulia uteuzi wa mgombea urais 2015.

Kushikilia uongozi kwenye chama kwa muda mrefu huku akidai demokrasia ni kosa lingine kubwa japo ni gumu kuonekana machoni pa wengi kwa sasa.

Hivyo basi zinapokuja tuhuma kama hizi kwake wengine sisi inatufanya tuzidi kumtilia mashaka. Kulingana na mambo hayo yanajitokeza kwake wazi kabisa.

Kwa kweli ni vizuri kwake aanze kwanza kutumia busara zaidi katika uongozi kama vile wanavyomhimiza Rais kuhusu kuwa na maamuzi ya busara basi na yeye ayafuate hayo. Ili kuondoa mashaka yanayoanza kujijenga miongoni mwa wengi dhidi yake ili tuweze kuwa na upinzani imara ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Note; nimetoa maoni yangu bila kufungamana na chama chochote kile.
 
Kwa maelezo hayo,hiyo ni kazi ya polisi kumtafuta Ben eidha kwa kumhoji Mbowe kama ulivyo eleza au Mwanahalisi kwa jinsi walivyo ripoti juu ya Ben.Lakini polisi wanaona ugumu gani kumtafuta Ben?Ili akipatikana ujulikane ukweli wa nani alimteka?Serikali ina kigugumizi cha nini kumtafuta raia wake kama haihusiki?Tuache porojo kwenye uhai wa mtu

Imtafute wapi wakati inajulikana alipo Mbowe kamficha hivi Polisi watafanya kazi hata za maigizo ya wajinga kama chadema wakati kuna majukumu mengi ya kulinda watu na mali zao? Wakae kushupalia igizo la Mbowe na Kampuni yake aanze Mbowe kutafuta kama ni kweli kisha akishindwa atakwenda toa taarifa rasmi na uthibitisho wa kuonyesha kwamba yeye hahusiki na Polisi wataingia kazini na itaeleweka nini kilichotokea sasa mwenye mlinzi kauchuna leo polisi wafanye nini acheni utani jamani hayo ni maigizo ya chadema rejeeni gazeti la mwana halisi lina majibu yote.
 
Hayo maswali kayaulize polisi wewe mammalia
Acha ujinga wewe kondoo wa kafara hawezi kwenda kuhoji polisi kwani Ben alikuwa anafanya kazi Polisi? Kwanini mnamuogopa mwajiri wake badala yake mnalazimisha Polisi wawape majibu ambayo alitakiwa awape Mbowe shikeni adabu zenu kusumbua Polisi wetu.
 
Wewe mammalia hivi hujui kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao hebu peleka ubashite wenu huko kolomije

Sasaacha mlango wazi kwakuwa ni jukumu la polisi kukulinda watakuja kukulinda maana mnadhani kulinda mtu na mali zake ni katika utaratibu wa kipuuzi kama mliotumia kuficha huyo muhuni mwenzenu eti muwape jukumu Polisi lala tu mlango wazi au mkeo atoroshwe na bwana mwingine kama wewe hujaripoti polisi wao wataota waje kukutafutia mkeo??? Tumia akili kufikiri na siyo Masaburi, Mbowe aliyekuwa anamtumia hajaenda kutoa taarifa polisi wewe Mmamalia unakomaa polisi wamtafute nani kakuambia Ben kapotea ???
 
Chadema wana kitengo cha intelejesia wamefanya juhudi Zipi kumtafuta mwenzao? Je Kama chama wamefanya nini kuhusu kupatikana kwa Ben Saanane? Naona marafiki zake na UTG a. K. A UTI Ndiyo wanaoangaika Vipi? Mbona Ney WA mitego tuliona mawakili Walipelekwa polisi kwa nyodo Vipi kWA Ben Saanane Kulikoni kigugumizi?
Huna akili we we! Jambo liko polisi kisha unataka kitengo cha chama cha inteligensia kiendeshe uchunguzi? Kisha waambiwe wana ingilia uchunguzi wa polisi?
Siasa zenu za kijinga msiziingize kwenye uhai wa watu. Ben ni mtoto wa watu, baba wa mtoto na kaka wa watu. Kuna watu unawatia uchungu kwa upumbavu wako unaoandika hapa.
 
Imani na mbowe ilinitoka tangu siku alipohusishwa na kuitwa kuhojiwa kuhusu suala la madawa. Kiukweli ni makosa yalitumika kwanjia aliyotumia makonda.
Lakini kwa uzito wa suala la madawa na athari zake kwa taifa. Yeye kama kiongozi mkubwa wa upinzani angetumia hekima tu na kukubali kwenda kuhojiwa ili kutoa ushirikiano wake. Ngwajima ni mtu makini sana mana yeye alikubali kuenda akahojiwa na akapimwa na ukweli ukabainika na mpaka sasa hakuna anaye mtilia shaka. Lakini huyu yeye kakimbilia mahakamani mapema sana ili akapate kinga ya mahakama.
Kitu hiki sisi wengine bado kinatutia shaka hadi leo. Aliogopa nini kwenda kule kuhojiwa hata kama ni kweli sio njia sahihi?
Alafu na chadema nao wamemkingia kifua moja kwa moja bila uchunguzi wowote kuhusu tuhuma zile.( inamaana anaaminiwa 100% ) hili linatia shaka sana kwa wale wafuatiliaji wa mambo.

Ubabe wa mbowe katika chama hasa ukichukulia uteuzi wa mgombea urais 2015.

Kushikilia uongozi kwenye chama kwa muda mrefu huku akidai demokrasia ni kosa lingine kubwa japo ni gumu kuonekana machoni pa wengi kwa sasa.

Hivyo basi zinapokuja tuhuma kama hizi kwake wengine sisi inatufanya tuzidi kumtilia mashaka. Kulingana na mambo hayo yanajitokeza kwake wazi kabisa.

Kwa kweli ni vizuri kwake aanze kwanza kutumia busara zaidi katika uongozi kama vile wanavyomhimiza Rais kuhusu kuwa na maamuzi ya busara basi na yeye ayafuate hayo. Ili kuondoa mashaka yanayoanza kujijenga miongoni mwa wengi dhidi yake ili tuweze kuwa na upinzani imara ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Note; nimetoa maoni yangu bila kufungamana na chama chochote kile.
Maneno meeeengi lakini upeo wa kuelewa mdogo. Mbowe hawezi kukubali kuitwa kihuni hata kidogo. Nafasi yake sii ya kuamriwa na makonda kijinga namna ile.
Nadhani hujui nafasi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani ikoje!
 
Back
Top Bottom