Chamoto
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 9,856
- 22,191
Nimekuwa nikisema hapa miaka mingi kuwa uwezo tunao ila nimekuwa nikibezwa kuwa ni nadharia tuu.Ni magufuli kafanya sasa watanzania tuna uthubutu wa kuwaza hivi kwa mambo ambayo zamani yalionekana impossible kwa Tanzania, sasa magufuli kafanya possible
Ndio maana watanzania tumeshajijengea tabia kwamba kwa sasa kila kitu kinawezekana, viva JPM viva Tanzania
Zile kauli za JPM kwamba Tanzania tunaweza sasa zimezaa matunda kwenye fikra za watanzania.
Unajua majority ya watu wanahitaji ruhusa ya kufanya mambo, ni watu wachache sana wenye uthubutu wakufanya maamuzi yao wao pekeyao. Alichokifanya Rais ni kuwapa watanzania permission ya kutambua kuwa tunaweza. Tunaweza kumwambia Barrick hapana, tunaweza kuwaambia wajerumani, "kama hamtatupa mkopo wa kujenga SGR tutajenga kwa fedha zetu".
Na hii ndiyo sababu hasa ya Magu kuchukiwa na mabeberu, yeye anawafumbua macho waafrika wengine na kadri siku zinavyoenda itaondoa unyonyaji Afrika.
Ila Magu noma aisee, kila kitu anachofanya kinabarikiwa, na anajua kuruka viunzi na mitego mingi. Ona ishu ya Kibiti, makinikia, bwawa la umeme (watu wa mazingira), kununua ndege (Leo imeenda India kubebea wabongo), hivi vyote vilikuwa ni visiki vikubwa sana. Na sasa hii Corona anavyoipangua, hata Maradona haoni ndani.


