nimegundua kuwa wewe ni mtanzania mwenzangu, lakini pia ni mgeni hapa kenyaforum.hivyo basi kwa kuwa mimi ni mwenyeji mzoefu hapa KF,nachukua fursa hii kukukaribisha rasmi,karibu sana.
nita kujibu kiustarabu ili kuweka record sawa lakini nitaomba ujibu maswali yangu kwa kuambatanisha na ushahidi.
(tatizo la hapa kenyaforum hatu-comment kisiasa almrad tu,lazima uweke ushahidi kidogo wa either link au picha/screenshot).
ni wapi ulitoa huo mtizamo.Je kuna tafiti yoyote iliyofanywa na taasisi inayotambulika ikadai kwamba mji wenye tenant wa kudumu ndio mji ulioendelea sana?.ushahidi ktk hili please.
kwa hiyo nairobi imeendelea kuzidi dar kwasababu watu wake wengi ni tenants?.ushahidi please.
ni sababu gani iliyosababisha nairobi yenye house tenant wengi kushinda dar ikawa na slums kubwa east africa na africa kwa ujumla.majibu na ushahidi tafadhali
kwa hiyo kwa mtazamo wako wewe,kuishi kwenye nyumba ya kupanga ni fahari na nafuu zaidi kuliko kuishi kwenye nyumba yako binafsi?.
tuanzie kwanza hapo halafu tuendelee na mjadala.
NB.
wakati unatafakari maswali yangu,naombe usome/utazame kwa umakini hii screenshot hapa chini.