iko hivi buda,kiswahili kilianzia kilifi na lamu,sawa.
lakini kiswahili kinachopendwa na watu wengi EA na wale wa kutoka mataifa mengine nje ya EA,ni kiswahili cha tz.
wenyewe wanasema kiswahili cha tz kina madoido (swag) na kinaleta raha pale unapomsikia mtu anazungumza.
hata wadada warembo wa kisasa wa nairobi wanavutiwa sana kiswahili cha vijana wa kiume wa tz kuliko kile kiswahili cha vijana wa nairobi,mombasa,kilifi na lamu.
nimeshuhudia mara kadhaa nikiwa nairobi,vijana wengi waki-struggle ku- master kiswahili cha tz.hii ni kuonyesha ni kiasi gani kiswahili cha tz kinapendwa sana ukanda huu.
kingereza pia,japo asili yake ni wazungu wa united kingdom,lakini watu wengi duniani wanavutiwa na kingereza chenye lafudhi ya kimarekani.
hata hapo kenya,vijana wanaomudu kuzungumza kingereza,wanapenda kuzungumza kama wamarekani,mfano mwanamuziki caligraph jones na prezzo.
huo ndio ukweli buda,kama utaamua kubisha,wewe bisha tu ila ni ngumu kupinga ukweli.