President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 34,015
- 93,382
Hapo kwenye red ndio propaganda zenyewe kaka. Hiyo inaitwa Name Calling Propaganda.Kuhusu propaganda, mimi siko interested na hayo, nipo hapa kutoa maoni yangu binafsi tuu.
Kuhusu watu wa Tanganyika Law society (TLS), Maria Sarungi na hata Tundu lissu, mimi huwa siwaoni kama wana uzalendo wa kweli (labda kama kazi yao ni kupeleka watu maboya) ila kusema CCM mtandao ni wazalendo, hapo ndipo tutatofautiana.
Magufuli kweli alikuwa mzalendo, ukiondoa mapungufu aliyokuwa nayo, alileta positive impact kwa nchi yetu, ndiyo maana wakamuua, sasa unajiuliza, walimuua mzalendo kwa faida ya nani?
Sasa hivi tunaona mpasuko, watu wanaanza kuchochea udini, hii ni kwa faida ya nani? Ikichafuka Tanzania, utafurahi?
Hiyo propaganda inatumika sana, na ukiulizwa utoa ufafanuzi kunakuwa hakuna ufafanuzi. Propaganda kazi yake ni kuamsha hisia na siyo logical issues. Mifano ya Name Calling "Nduli Idd Amin", Bashite, Ponjoro, Nyanga'u, Makaburu nk.
Sasa na wewe either ni msambaza propaganda pasipo kujijua au wewe ni sehemu ya mpango wa propaganda hizo.
Hebu tueleze CCM mtandao ni akina nani na wamefanya nini? Weka ushahidi wa kitu walichokifanya.