Angejiuliza why I chose the lowest ranked towns in Kenya to compare with Mbeya and not Kisii, Kericho Thika, Kakamega.
To be frank, Kisii, Thika and Kakamega are well developed more than Mbeya yet they are not regarded cities in Kenya.
Okay let me just address this kwa sababu sitaki kuwa naingia humu kubishana na nyinyi kila siku.
Tanzania sio Kenya, sawa? Huku Tanzania ili place iwe city kuna standard zetu wenyewe tumejiwekea, hatutumii Kenyan standards, tunazo zetu wenyewe
Mbeya imepewa hadhi ya jiji kwa sababu inatimiza vigezo ambavyo serikali ya Tanzania hutumia kutangaza eneo kuwa jiji.
1. Makao makuu ya Mkoa
Mbeya ni makao makuu ya Mkoa wa Mbeya.
Makao makuu ya mkoa huwa na uzito mkubwa kiutawala, jambo ambalo linaipa hadhi ya jiji.
2. Idadi kubwa ya watu
Mbeya ina idadi kubwa ya wakazi wa mijini ukilinganisha na miji mingine mingi Tanzania.
Hata kama hakuna majengo marefu, jiji linaenea eneo kubwa na lina mitaa mingi yenye watu wengi.
Jiji la Mbeya lina takribani watu laki 6, hata money circulation ni kubwa
3. Umuhimu wa kiuchumi
Mbeya ni kitovu muhimu cha biashara na usafirishaji kwa Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na nchi jirani kama Zambia, Malawi na DRC. Ina:
- Kituo kikuu cha reli ya TAZARA
- Barabara kuu zinazounganisha mikoa na nchi jirani
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe
- Masoko makubwa ya kilimo (Uyole, Soko Matola, Igawilo n.k.)
- Bandari kavu ambayo ipo busy, Dry port
4. Miundombinu ya Mjini
Hadhi ya jiji pia kwa hapa Tanzania hutokana na huduma za mijini. Mbeya ina:
- Hospitali nyingi
- Universities nyingi
- Benki nyingi
- Viwanda vingi
- Ofisi nyingi za serikali ya mkoa na halmashauri
5. Maendeleo ya kihistoria
Mbeya imekua makazi makubwa tangu enzi za ukoloni kutokana na uchimbaji madini, kilimo na usafirishaji. Ukuaji huu wa muda mrefu uliisaidia kupata hadhi ya jiji.
Kwa kifupi:
Mbeya ni jiji kwa sababu ya umuhimu wake kiutawala, idadi ya watu, uchumi, na miundombinu na sio mwonekano wa skyline au majengo marefu.
Mbeya haina skyscrapers, majengo mengi Mbeya ni floor 5 hadi 7 kushuka. Hata tallest buildings hapa zina around 10 floors only. Na hii ni kwa sababu soil ya Mbeya hairuhusu skyscrapers
Hata sasahivi mji umeanza kukua tena baada ya kulala kwa muda mrefu, majengo yote mapya yanayojengwa 99% ni less than 7 floors. Na mji huu utaendelea kuwa hivi na majengo mafupi
Mbeya ni sehemu nzuri yenye milima mingi, maisha ni very cheap, kuna chakula kingi sana, hali ya hewa nzuri ya ubaridi mwaka mzima, mvua nyingi na ardhi yenye rutuba
Pia maeneo yote ya slums ya Mbeya ni kwamba nyumba hizo zilijengwa miaka ya zamani, sikuhizi watu wanaojenga nyumba Mbeya wanajenga nyumba nzuri na za kisasa
Mwenzako Nicxie anasema natetea Mbeya eti kwa kuwa ni my home town, Mbeya sio hometown yangu, ila huu ni mwaka wa 3 nipo Mbeya. Nilikuwepo high school miaka 2 na November nimekuja pia kwa ajili ya masomo yangu ya ngazi ya juu, niko more than 850km from home
So nakuambia tu hizo Bondo na Siaya hata zingekuwa hapa Tanzania zisingekuwa cities, kwa sababu hazijafikia viwango vya kuwa city Tanzania. Mbeya imekidhi vigezo na huku kwetu skyscrapers sio kigezo cha sehemu kuwa city.