Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Yani kuhusu Samia hata bila kufanya mauaji, mi bado naona utendaji kazi wa serikali yake ni mdogo sana. Naona nchi yetu inaendelea taratibu mno ndo maana namuuliza huyu Venus Star anitajie mega projects mpya za Samia maana sidhani kama zipo, sijawahi hata kusikia. Ila sijui ngoja tuone hii miaka 5 kama kuna kitu kikubwa atafanya 🙂
Huwezi kuchafu kitu kitakatifu. Tanzania inaendelea kusonga mbele. Wengine wanatumika kuichafua.

Tanzania imepiga hatua kwenye kilimo Bank ya Maendeleo ya Kilimo inatoa fedha kwaajili ya kufanikisha miradi ya kilimo. Pesa zipo andika andiko lako waone TADB upate pesa.

We jamaa mbona una tabia za kike kike?

Eti wivu na kura mmejipigia
Kaka hayo siyo yangu. Kazi yangu ni kuonesha mazuri yaliyofanywa na yanayofanywa na Tanzania. Hiyo ya kuichafua na kuiongelea mabaya Tanzania siyo kazi yangu.

Unaifahamu Banki ya maendeleo ya Kilimo (TADB)? Wamepatiwa fedha zaidi ya Tsh 10 trillion kwaajili ya kuwapatia watu kwenye miradi ya kilimo. Changamkia fursa hii kaka.

Maeneo yanayopatiwa fedha:

Pembejeo​

Usambazaji wa mbegu bora, mbolea, na rasilimali nyingine kwa ajili ya uzalishaji.

Uzalishaji​

Kuwawezesha wakulima kupata vifaa, ujuzi, na huduma za fedha ili kuleta tija katika uzalishaji.

Uhifadhi​

Kuwezesha upatikanaji wa maghala, vihenga vya kisasa na vyumba vya barafu ili kutatua tatizo la upotevu wa mazao baada ya kuvuna na kuhakikisha ubora wa bidhaa.

Uchakataji​

Kuongeza thamani ya mazao ghafi ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuboresha bidhaa.

Usambazaji​

Kuongeza ufanisi katika usambazaji wa bidhaa kwenye masoko kupitia njia mbali mbali za usafirishaji.

Masoko​

Kuwezesha upatikanaji wa masoko mapya ya bidhaa za kilimo ili kumuongezea mkulima mapato.

Pitia hapa ujifunze zaidi

Huwezi kuchafu kitu kitakatifu. Tanzania inaendelea kusonga mbele. Wengine wanatumika kuichafua.

Tanzania imepiga hatua kwenye kilimo Bank ya Maendeleo ya Kilimo inatoa fedha kwaajili ya kufanikisha miradi ya kilimo. Pesa zipo andika andiko lako waone TADB upate pesa.

View attachment 3498272
Yani niichafue Tanzania nifaidike nini wakati mimi ni Mtanzania? Na si a nchi nyingine tofauti na hii
Hizi project zipo lakini sio nyingi kama enzi za Magufuli, halafu nyingi sikuhizi hata sio megaprojects kubwa kihivyo ni za kawaida tu.
Kwa jinsi awamu ya 6 ilivyokopa, na hizi tozo zote, na serikali inadai uchu.mi wetu unakua projects kubwa kubwa zilipaswa kuwa nyingi kuliko awamu ya 5
 
I mean hii miradi ilishaanzishwa sasahivi inaendelezwa, hivi vinapaswa viendelee huku miradi mipya inazidi kuongezwa, si kila siku tunaambiwa uchumi wetu unakua kwa kasi

Just imagine uanzilishi wa Megaprojects kama
1. Mradi wa SGR
2. Mwalimu Nyerere HEP Project
3. Ujenzi wa mji wa kiserikali Dodoma
4. Ujenzi wa Flyovers Tanzania
5. BRT
6. Madaraja makubwa Dar na Mwanza

Hizi zilikuwa project chache lakini ni kubwa sana ukifananisha na project za sasahivi na zilianzishwa ndani ya awamu ya 5 pekee lakini uanzilishi wa project hizi ulikuwa unaenda sambamba na project nyingine za kati mfano bus stations kubwa kila kona ya Tanzania, ujenzi wa modern hospital kubwa ya Mloganzila, hospitali mbili mbili kila wilaya, usambazaji umeme kwa kasi vijijini, maeneo mengi yalijengeka kipindi hiki, mtandao mkubwa wa lami, upanuzi wa Airport ya Mwl Nyerere, shule za kutosha. Yani kipindi hicho hadi ofisini watu walikuwa wanapiga kazi kuhofia kutumbuliwa. Rushwa ilipungua sana. Na kumbuka Magufuli hakutuwekea tozo za ajabu ajabu, na bado tukaingia uchumi wa kati

Sasa hii awamu ya 6 si tunaambiwa uchymi wetu ni mkubwa zaidi na unakua kwa kasi, pia kipindi hiki cha tozo, na ukizingatia tunakopa sana kwa hiyo hela zipo nyingi zaidi kipindi hiki. Niwe tu mkweli nilitarajia tuwe na even more projects kushinda enzi za Magufuli kwa sababu sasahivi hela ipo ya kutosha. Lakini karibia kila mradi sikuhizi naona ni hiihii ya level ya kati ambayo hata enzi za Magufuli ilikuwepo tena mingi zaidi. Ila zile strong hakuna
Kwanza correnction.
BRT ilianzishwa wakati wa Kikwete.
Mradi wa SGR Fesibility study ilianza wakati wa Kikwete, lilikuwa adhimio la East Africa kujenga SGR.

2. Wakati Magufuli akiwa president mshauri wake wa kwanza na wa karibu alikuwa Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassani Mwanamke wa Shoka, wanaume wakimuona wanatetemeka.
 
Yani niichafue Tanzania nifaidike nini wakati mimi ni Mtanzania? Na si a nchi nyingine tofauti na hii
Hizi project zipo lakini sio nyingi kama enzi za Magufuli, halafu nyingi sikuhizi hata sio megaprojects kubwa kihivyo ni za kawaida tu.
Kwa jinsi awamu ya 6 ilivyokopa, na hizi tozo zote, na serikali inadai uchu.mi wetu unakua projects kubwa kubwa zilipaswa kuwa nyingi kuliko awamu ya 5
Ndio utueleze sasa wale waliochoma vituo vya mwendo kasi ni watanzania au siyo watanzania?
 
Watu wapo kazini kwaajili ya maendeleo. Wengine wapo kupiga domo na Mange.

TADB - Kilimo kinabenkika

Kwanza correnction.
BRT ilianzishwa wakati wa Kikwete.
Mradi wa SGR Fesibility study ilianza wakati wa Kikwete, lilikuwa adhimio la East Africa kujenga SGR.

2. Wakati Magufuli akiwa president mshauri wake wa kwanza na wa karibu alikuwa Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassani Mwanamke wa Shoka, wanaume wakimuona wanatetemeka.
Feasibility study ni easy issue ni utekelezaji, kama Samia ni mshauri mzuri sana mbona sasa awamu yake anashindwa kujenga sana kama Magufuli
 
Umeamua kupuuzia miradi ninayokuonesha Kwikwikwikwikwi

Miradi uliyoonesha ni ya kawaida sana. Sio mibaya ila sio mikubwa ukilinganisha na pesa ambazo serikali inakusanya sasa
Halafu hiyo Kwikwikwikwi... ndio nini
 
Miradi uliyoonesha ni ya kawaida sana. Sio mibaya ila sio mikubwa ukilinganisha na pesa ambazo serikali inakusanya sasa
Halafu hiyo Kwikwikwikwi... ndio nini
Sasa unataka miradi gani mdogo wangu. Kwikwikwikwikwi umeshiwa points. Kinachokusumbua bro ni chuki tu hakuna kingine.

Pole
 
Kwa hiyo hapa ndio nini sijaelewa. Kwamba watalii wameletwa na Mama Samia au Samia ndo kaleta vivutio vya utalii. Hiyo Kazi na Utu inahusikaje hapa, maana ni slogan ya Samia, sio ya utalii 😂😂
Good Question. Unaikumbuka Royal Tour Film? Hii imeleta mabadiliko makubwa sana kwenye Sector ya Utalii. Huu ubunifu haujawahi kutokea tangu dunia iumbwe. Hii Film ilioneshwa kwenye maeneo mengi sana Duniani. Imechechemua utalii Tanzania, hadi sasa wakenya wanaugulia maumivu. Hawana hamu Na Dkt.

View: https://youtu.be/WyHKO9DB4dQ?si=s9eC_SOBNcQ9jJzN
 
Sasa unataka miradi gani mdogo wangu. Kwikwikwikwikwi umeshiwa points. Kinachokusumbua bro ni chuki tu hakuna kingine.

Pole
Ni kweli, nachukia kuona nchi yetu inaendelea taratibu kuliko inavyotakiwa. Na hii chuki ni kweli inanisumbua
 
Ni kweli, nachukia kuona nchi yetu inaendelea taratibu kuliko inavyotakiwa. Na hii chuki ni kweli inanisumbua
Mimi kaka nakugonga kwa facts tu. Tanzania ni kati ya nchi 10 zinazokua kwa haraka Afrika.

Hii nayo unalo la kusema?

1762449437517.png
 
Back
Top Bottom