Bado wanafanya mpaka leo. Lipa kwa Mpesa haikupaswa kuwa na makato hivyo. Tungekuwa tunalipa kwa simu kila mahali. Juzi nilibook bus nikalipa kwa simu walichukua 2000 kabisa kama makato. Yaan wanadiscourage kabisa lipa kwa mpesa. Mtu akiangalia hiyo 2000 si bora abook kituoni na apate hata supu ya book jero
Kusingekuwa na makato hata Daladala zote tungelipa kwa simu kama fuliza, pochi nk kama baadhi ya route za Matatu kule Nairobi .
Hapa akina
NairobiWalker nawapongeza, matatu zao nyingi hasa za thika road unaweza lipa kwa simu. Japo Bado tunawapita kwa kuwa na City Mobile application ya Mwendokasi na Dar city NCARD ambazo nazo ni cashless