Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Mimi mwenyewe nipo humu since 2019 ninazo id mbili humu.

Kwanini unapenda kutia chumvi vitu .? Nini lengo lako.? Wewe ni Chadomo.?
Shida haipo kwako tuu wajinga wengi kama wewe hawaupendi ukweli. Nikuulize wewe k kibuyu unauhakika Gani kuwa naongeza chumvi? Mara ya mwisho umepanda mwendokasi ni lini?
 
Hapa kwenye kukawia buses kufika kwasababu ya uchache wake siwezi kukupinga, pia inategemeana na route. Kwa mfano, umeona pale kimara mwisho.? Pale changamoto ya kukaa ndio unaweza kui experience zaidi kwasababu buses ni chache na routes zimeongezwa, sahii buses zinaenda hadi kibaha (sidhani kama wakati wananunua buses kwa awamu ya kwanza walinunua zinazotoshakufika huko) zingine zinaenda muhimbili, zingine zinapita sinza (barabara ya bamaga-Shekilango) zingine zinapita bagamoyo road, pia inatakiwa tukubaliane na ukweli kwamba watumiaji wa huduma wameendelea kuongezeka siku hadi siku, na ndio sababu demand imekua kubwa while supply ni ilele ya hitaji letu la awali.. sasa lazima kasoro zitokee.

Hapa nitakuunga mkono kuipigia kelele serikali inunue buses za kuzudi ili kukidhi mahitaji ya watumiaji. Na kimsingi tumeshuhudia jamaa wamenunua buses mingi labda tupige kelele waongeze ziwe walau buses 5000 hivi kwaajili ya phases zote 6 zikikamilika. Walau kila phase iwe na at least buses 700+.
 
Nayo Serikali imealika private sector.Bongo hapa Mali ya Umma Huwa ni shamba la Bibi so Bora waendeshe private sector kuliko zife na tuwe tunaziendesha Kwa ruzuku ni upuuzi
Uwajibikaji ndio tatizo wala sekta binafsi Tanzania hazijashindwa kuendesha huo mradi na hii yote ni kwa sababu ya kulindana na uchawa, yani tushindwe kuendesha brt ndio tutaweza Atcl na sgr
 
Umeeleza vizuri ila mwishoni tunarudi pale pale kwenye uwajibikaji ili suala halipo kabisa kwenye mashirika yetu ya serikali japo usafiri wa umma ufai kuendshwa kwa faida kwa sababu utakua gharama sana ila inabidi kuwepo na uwajibikaji kwa kiwango cha juu kwenye matengenezo na customer care , trc wanajitahidi kwenye upande wa sgr mpaka sasa ila bado mapema sana kusema wana afadhali
 
Uwajibikaji ndio tatizo wala sekta binafsi Tanzania hazijashindwa kuendesha huo mradi na hii yote ni kwa sababu ya kulindana na uchawa, yani tushindwe kuendesha brt ndio tutaweza Atcl na sgr

Kwa namna mchakato wa kupata fedha unavyokuwa mrefu serikalini ni ngumu sana kuendesha huu mradi kwa ufanisi. Ni Bora serikali iendelee na ujenzi wa miundombinu ila upande wa waendeshaji wa mabasi waweke kampuni tofauti tofauti.

Serikalini Hela kuingia ni rahisi ila kutoka ni ngumu, pili watu wa kupiga kwa pet cash... Kwa biashara ya usafirishaji unatakiwa uwe na balance cash muda wowote kwa ajili ya dharura... Huwezi kuandika pet cash kila siku sijui bolts, oils, rangi, break pads,fluids etc... utachoka..

Halafu bado upigaji upo sana maana uwajibikaji ni zero....wahasibu wanadhani wakitoa Hela ni kama wanakupa ya kutumia,sio ya kufanyia kazi... Zile gari zingekuwa zinajichanganya mtaani wangekuwa wananyonya mafuta kila siku...ila wanaiba sana engine oils na lubricant... Wananunua ila hawaweki kwenye magari...yanakufa tu yenyewe hakuna anaejali...

Kampuni binafsi wanakuwa na uchungu na gari zao, service watazingatia, uendeshaji wa tahadhari watazingatia na mambo mengine.... Ile maintenance team pale ukienda kuwakagua sidhani kama wanajua kazi yao...kila siku wana outsource mafundi nje na bado wako na kitengo Cha Ufundi... Ni upigaji tu wa kifala...

Gari ni matunzo na service kulingana na ratiba, hizo za kwao hawatunzi kabisa na ni kwa sababu usimamizi hakuna... management Haina wataalam wa mambo ya magari na usafirishaji... Kiburi na fair of insubordination inapelekea kuua mradi..
Wabinafsishe tu...wanakie kutoza Hela ya njia.
 
Tumerudi kule kule, "sisi hatuwezi, sijui sisi ni masikini".

Yaani tufanye upembuzi yakinifu, tutafute pesa wenyewe, halafu eti tushindwe kuendesha, akili za wapi hizi? Haya ndo matatizo ya kubebana na kuchekeana.
Na hatuwezi kupiga hatua hata kidogo tukiendelea hvi na mawazo yale yale eti mtu akikosea unamwamisha kitengo badala ya kumwajibishaa , kutegemea wawekezaji wa njee waje watukomboe kutoka kwenye umaskini wetu.
 
Uchumi huria sawa ila kuna sekta kama izi haifai kupewa mwekezaji wa njee ingekuwa atcl hapa sawa ila sio usafiri wa umma
 
Kama hiyo ndio sababu, mbona hata sasa kuna kampuni local imepewa sehemunya mradi??

View attachment 3354580
Mwanzoni ilitakiwa iwe hivyo lakini sasa anybody can operate sababu hii concept ya BRT imeshazoeleka huku kwetu na changamoto tumeshazijua na zimefanyiwa utatuzi hususan kwenye eneo la ticketing na display ya muda wa mabasi kuwasili vituoni hii kazi walipewa kampuni toka Spain kama sikosei.
 
Is yours based on statistics? I was there and I know Eastleigh. You just threw words around. Can you even tell how tall the tallest building under construction in Kariakoo is?
kama huwezi kuleta stat but una argue on what you saw in KKO tufunge mjadala maana hakutakuwa na informing conclusion.
 
Uchumi huria sawa ila kuna sekta kama izi haifai kupewa mwekezaji wa njee ingekuwa atcl hapa sawa ila sio usafiri wa umma
kama kampuni zetu ama serikali hazina ufanisi katika uendeshaji wake tufanyaje mkuu? Tuangalie miradi ya gharama ikifa polepole ama tufanye maamuzi magumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…