Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Unaumwa mavi wewe!


View: https://youtu.be/HrTNg9ppdZM?si=u2BiVuRJQ8P1piZj
 
Hayati Magufuli amefanya makubwa katika hii nchi toka akiwa waziri sifa yake kubwa ilikuwa ni uchapakazi mtu aliyeamini katika matokeo yawe mazuri yawe mabaya, kuna miradi mingi sana CCM ilikuwa ikiisogeza mbele kwenye maandiko yao kwa mgongo wa β€œNo Fund” ijapokuwa kwenye makaratasi ipo, Mwamba alivyoingia madarakani akaestablish almost full swing, inaishaje hakuna aliyekuwa na idea, mara ghafla katukota,
Kutokana na kanuni na taratibu za nchi Makamu wa Rais inamlazimu kushika nchi kwa kipindi cha muhula kilichosalia,kilichofuata
Mama Samia anaingia Madarakani, Miradi mingi ikiwa kwenye hatua ya awali ama katikati ama mingine haijaanza kabisa, Amejitahidi sana huyu Mama kwenye utekelezaji na ndicho Watanzania tunachotaka.
Kufanya stori yangu fupi ni hivi,
Hayati Magufuli ametuaminisha Watanzania Tunaweza Kufanya Makubwa kwa kwa kuanzisha miradi mikubwa mikubwa
Mama Samia ametudhihirishia kwa vitendo ni kweli Watanzania Tunaweza.
 
Naona mkuu unaanza kutokwa na kumbukumbu ama na akili
Na ukumbuke Magufuli amefariki mwaka wa kwanza tu alipoanza muhula wake wa pili.
Na kwa asilimia zilizobaki angemaliza na kuzindua mwenyewe.
Ange ange!
 
Alifungua nani na baada ya nani kukamilisha ujenzi?

Usitusumbue,hakuna kitu Mwendazake alikamilisha Kwa miaka yake 5.5

View: https://x.com/TanzaniaYaMama/status/1817558841568932110?t=0_swK51VCsAbVlVGGLi2qQ&s=19View attachment 3144923
kukamilisha ilikua ni lazima hata mwenye mradi angekuwepo angekamilisha sometimes unakua kama vile huna akili πŸ˜‚πŸ˜‚

kwan angekuwepo yeye asingekamilisha hayo madaraja aliyoyaanzisha mwenyewe au unafkiri kuanzisha ni rahisi sana, yataka moyo sana
 
Mradi wa Tabora wa Bilioni 700? Unaota wewe,uweke hapa na Mimi nisome kama wewe ulivyosoma πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kwa hiyo viwanja vya ndege 2 basi ndio vinatosha miaka 5.5? πŸ˜‚πŸ˜‚

Kigamboni ya wapi hiyo? Daraja la Kigamboni amejenga JK,the same to Kilombelo ambalo lina jina La Magufuli

Wewe Bado unaokoteza miradi ambayo hata haikufanyika awamu ya 5 πŸ˜‚πŸ˜‚

Weka hapa mradi wa Maji wa Bilioni 700 😁😁,Bora hata ungesema mradi wa Maji wa Arusha ambao haukumaliza kama kawaida yake πŸ˜‚πŸ˜‚

Mwisho Mwendazake alikuwa na miradi ya kuokoteza Kwa sababu hata pesa hakuwa nazo maana hajui kuzitafuta, biashara zilianguka, investors wakakimbia,Kilimo kilianguka nk nk
 
kaka whatever the case huu mradi jamaa aliupigania sana na fitna nyingi sana zilitembea na musianze kuleta ujinga sasa hao mawaziri waliokua wanatumwa kwenda uganda mara yeye magi akutane na museven tanga munafkiri ilikuja kwa bahat mbaya

toeni credit kwa jamaa japo ukweli ni mchungu infact he was a real fighter, kutoa mradi kuuleta tanzania sio jambo dogo kabisa wakenya wanasifika duniani kwa uongo na drama, haikua kazi rahisi kama munavofikiri kabisaaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Flyover ya tazara ulikamilisha wewe?
Interchange ya ubungo nani alikamilisha?
JNIA je nani alikamilisha? Acha utoto.
yani hata mm hua nashangaa huu utoto hawa wakenya ukiwauliza leo alieleta maendeleo tanzania watakujibu magufuli tena straight bila kupepesa machoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
nimecheka sana tena nimecheka kwa nguvu sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…