Mkuu sawa basi tuangalie kwa upande mwingine elimu. Kikwete aliweza ongeza idadi ya shule za sekondari zaid ya mara kumi na vyuo vikuu almost nusu , mkuu unarecord yoyote ya ujenzi wa shule mpya au chuo chochote kipya kipindi Cha magu?
View attachment 3133203
Hilo la elimu lote mimi nalifidia kwa sera ya Magufuli ya elimu bure.
Utambue kuwa unapoweka huduma fulani bure serikalini kunatakiwa kuwe na fungu la uendeshaji hiyo huduma.
Kikwete alianzisha ujenzi wa hospitali kama Benjamin mkapa, mlonganzila,JKCI NA Maboresho kadha wa kadha kwenye afya mkuu una data za maboresho yoyote yanayomgusa Moja kwa Moja mwananchi kipindi Cha magu.
Kuna vituo vya afya hususan maeneo ya vijijini vingi tu vilijengwa kipindi cha Magufuli na hata mimi nimeshuhudia.
Morogoro mkoa naotembea sana kuna vituo vya afya vitatu vilijengwa kwa wakati mmoja katika vijiji vitatu vinavyofuatana mnamo 2017 kama sijakosea.
Pia kuna vifaa tiba muhimu kama CT-Scan nahisi vilianza kuingizwa ama kuagizwa kwa wingi kipindi cha Magufuli.
Sera ya kubobeza madaktari ili wabaki katika vituo vyao badala ya kuandika rufaa lukuki kwa wagonjwa hili lilianza kipindi cha Marehemu Magufuli.
2005 mwalimu au mtumishi ngazi ya degree alipokea mshahara wa 140,000 na Kila mwaka kukiwa Kuna ongezeko yaan annual increment, mpaka mwaka 2011 tgs d akawa amepandishiwa mpaka 449,000 ongezeko la zaid asilimia 200 na Kila mwaka kulikuwa na ajira.
Je una habari toka kikwete ametoka madarakani mshahara wa tgsd umekuwa ni 710,000 mpaka magu anatoka madarakani hakuwahi kuongeza hata Senti huku akizuia upandaji wa madaraja na akaondoa mpaka Ile annual increment.
Hapa sasa ndio patamu zaidi mkuu.
Hivi umeshajiuliza pesa za kulipa hao watumishi wa umma na kuajiri zaidi zinatoka wapi!?
Mnafurahia mishahara mikubwa pasi na kujua wapi inatoka.
Kwa pato gani la taifa kila awamu uongeze mishahara!?
Mwishowe mnakopa na nchi inazidi kuwa na madeni baadae kupelekea devaluation ya shilingi yako.
Magufuli alishasema wazi,serikali ya Tanzania haina hizo pesa kiuhalisia za kuongeza mishahara kila wakati na kuajiri kila wakati.
Ila usisahau kuwa aliwapa kipaumbele wajasiriamali wadogo wadogo na vijana na kina mama kwa kuwapa fedha za mikopo kutoka Halmashauri.Hili jambo halikuanzia kwa Samia lilianzia kwa Magufuli.
Alitengeneza mazingira wezeshi ya hadi wa mtu wa chini kupata pesa.
Ila uliza sasa hivi hali ikoje mtaani.
Miradi hiyo michache ya sgr ,bwawa, umeme kwa sababu ya ukubwa inatupofusha na kusahau kuwa Kuna mahitaji mengi zaid ya ujenzi tu.
Leo hii ukiienda Kila ofisi Kuna uhaba wa watumishi huku tuna vijana kibao tu mtaan na hii inatokana na gap la kutoajiri alilolitengeneza magu.
Hata ukiangalia miradi tukiachana na hiyo tajwa hivi kujenga geita, sumbawanga,rukwa na chato airports kulikuwa na umuhimu kuliko barabara. Leo hii rukwa huko na chato ndege zinatua mara chache huku Hela ikiwa imelala
Mimi kila leo naingia ofisi za utumishi wa umma.
Sijaona huo uhaba unaousemea zaidi ya kurudi kwa uzembe na kutokujituma kwa watumishi wa umma na kukosa nidhamu ya utumishi wa umma.
Usiseme miradi midogo unakosea hilo.
*Ufufuaji wa reli ya Kaskazini Arusha.
-Uboreshaji wa reli kuwa continuos welded kutoka kuwa jointed rail.
Maana hii reli Kikwete aliirudisha toka kwa wahindi ikiwa mufrisi.
*Uboreshaji wa bandari.
*Uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati.
*Uboreshaji wa sekta ya madini kwa kuweka mashine ya usafishaji dhahabu kuwa 99.99% pure na uozeshaji wa makinikia.
-Kuwapa fursa wachimbaji wadogo wadogo wa kufanya biashara ya madini na kupata mikopo wezeshi ya kuwezesha shughuli zao.
Hii unasema ni miradi midogo mkuu!??
Aya endeleeni kufurahia serikali za danganya toto kukopa ili iwaongezee mishahara na ajira ilhali nchi inaoza.