Kuna mahali hapo kati tulipotea njia. Inasikitisha sana.
Kuna nchi zilichukua somo wakalifanyia kazi (Jeshi) kipindi cha Nyerere JWTZ ilikua ni jeshi imara na lilikua linaombwa kusaidia nchi nyingi kuzima mapinduzi, kutoa uhuru, kuzuia waasi. Kama falsafa ingeendelea si tungekua na jeshi hatari zaidi (Rwanda alichukua somo vizuri mnaona alivyo).
Viwanda vya Kijeshi (Nyumbu, Kiwanda cha Mizinga na risasi, ila walikiua) Uganda kabeba somo vizuri.
Naweza sema hakuna viwanda vinavyoniuma kama hivi.
1. General Tyres hadi leo kina potential ya kua revenue generator wa serikali ila hawakioni wanaona kuongeza tozo ndio kupata pesa.
2. Viwanda vya Nguo (Urafiki, Mwatex, Musoma Textile) dah yaani hakuna mwendeleo sisi wa kuexport mafamba hivyo?.
3. Viwanda vya Baisikeli ya Swala (NABISCO) Naamini sasa bajaji isingekua tabu.
4. Kiwanda cha chuma (chenye kuunda kila aina ya pembejeo au chuma) mashine aliuziwa Mchungaji Rwakatare like Seriously?
Na now vinavyouma zaidi nina wasiwasi zaidi ni hii miradi ambayo gov in full control nayo SGR, JNHP, MERERANI, MCHUCHUMA & LINGAGA, TWIGA MINERALS (BULYANHULU 50% NORTH MARA 16%), TEMBO NICKEL.
Wameanza na PORT sijui kinachofata asee.
Ikiwa kipindi cha Sakata la Dp World walitaka sheria ya Magufuli ya Permanent Sovereignty on Natural resources ibadilishwe itakuaje hivyo. Maana walishindwa kupitisha.
Hiyo sheria ya 2017 ina ipa Nchi Permanent Sovereignty, inamaanisha mkataba wa milele hauwezekani, na ikiwa muwekezaji haifaidishi nchi inaweza kuvunjwa akarudi kwao, na kushtaki ni kushitakia hapa hapa sio nje.
Sheria kama hiyo unaenda ibadili ili iweje?