Hizo ni insecurities zenu. Mbona Uganda wasilalamike?
1. EAC ilivunjwa kisa hakukuwa na maelewano. Huwezi laumu Kenya wakati kutoelewana kulitokea pande zote. Hatukuiba ndege, tulichukua ndege kulingana na shares tulizokuwa nazo. Kwa East African Airways, Kenya ilikuwa na 67.7% shares Tanganyika ikawa na 9% Uganda 22.6% na Zanzibar 0.7%. Ulitegemea tugawane visawa wakati sisi tuna shares nyingi? Cha kushangaza, Waganda ambao walikua na shares nyingi kumshinda hawalalamiki ni nyinyi tu kisa mmeaminishwa na wanasiasa wenu na chuki zenu.
2. Maandamano ya EACOP hayakufanywa na Wakenya, yalifanywa na watetezi wa mazingira. Yalifanyika UK na France. Tena wanasiasa wenu wamemuaminisha ni Kenya. Shida yenu hamuelewi jinsi ulimwengu unavyosonga. Kwa nchi zilizo na uhuru wa kujieleza huwezi jenga mradi wa kiwango hicho na kusikuwa na maandamano ya watetezi wa Mazingira - hapa Kenya kabla SGR ijengwa kulikuwa na maandamano - same na Thika road, EXpressway n.k.
3. Sijui unamaanisha nini na kupotosha ukweli. Shida yenu huwa hampendi kukubali ukweli alafu kila kitu mtalaumu Wakenya, sijui mna akili za kitoto ama vipi. World Bank ikitoa ripoti isema Tanzania ni bora kuliko Kenya kwa sector fulani, mtashangilia kila mahali hadi kwa socia media ndio kitu mtaongelea. The same World Bank ikitoa repoti eti Kenya ni bora kwa Tanzania kwa lingine mnaanza eti ooh Wakenya wanapotosha ukweli, ooh wanacook figures waonekane bora kutushinda. Yani huwa mnatia huruma sana.
Wee mwenyewe ukichunguza vizuri kwenye huu uzi walio na chuki ni kina nani? Saa hii tunabanter ni nchi gani itakuwa more prepared for AFCON ila wakati zetu ni banter tu, kwenu ni full chuki hadi mnaomba tukuwe banned ama tusiwe na uwezo wa kuandaa.