Kwahiyo hii misaada yote inayotolewa na serikali ya Marekani duniani kila mwaka inayozidi mabilioni ya Dola za Marekani kila mwaka, mbona usiiseme serikali ya US ambayo ndiyo yenye jukumu la kusaidia raia wake badala yake unamsema mtu binafsi ambaye hawajibiki kisheria?.
Serikali ya Marekani ndiyo yenye kukusanya Kodi za wamarekani ili kuwahudumia raia wake, huyo Bill Gate pia analipa Kodi kubwa kwa mwaka, lakini serikali hiyo hiyo ya Marekani ndiyo inayo ongoza kuchangia WHO na UN bodies zote duniani, Hilo unadhani ni sahihi, Marekani ndiyo inayo ongoza kutoa misaada Dunia nzima, mbona husemi "charity begins at home", ila mtu binafsi akifanya vile apendavyo kwako sio sawa.