Mm nakuelewa.but what do.you think needs to be done...?
My view
1. Kutafuta makazi mapya ..na serikali kujengea watu nyumba nzuri standard na watu kulipa kidogo kidogo bila riba...
Lakini ili hyo ifanyike kwanza we have to deal with other pressing issues ..then tukishajikwamua kwenye issue kama kila wilaya kuunganishwa na lami, kuwa na hospital nzuri na mifumo mizuri ya elimu ..serikali inaweza ikaangalia swala la kubomoa informal houses na kisha ku relocate watu..
2.Inaweza ikafanyika kwa pamoja ..ni kutenga kiasi kidogo cha fedha kama billion 50 to bil 100 kila budget kuhamisha watu na kupanga mji vizuri
Umeongea vizuri kaka, ngoja niongezee na mimi kidogo.
Tukiendelea na huu utaratibu wa watu wajenge nyumba hatutafika, mashirika ya serikali kama watumishi housing, nhc jeshi, tba nk yana uwezo wa kujenga nyumba ila saa nyingine inakuwa ngumu kupata wateja sababu watu wanajijengea.
Ili kuondoa makazi holela serikali izuie kwa sasa watu kujenga then iweze she makampuni kama nhc nk yajenge nyumba kwa Kuanzia serikali ikubali hasara au nusu hasara, kwa mfano itoe bilioni 100 kila mwaka kwa tba, nhc nk wajenge nyumba kwa sharti la kuvunja sehemu zilizo hovyo kama wslivyofanya magomeni kisha wananchi walioathirika wa napata nyumba zinazobaki wanauza au kupangisha.
Tujenge maghorofa, ujenzi wa nyumba za chini sio mzuri unafanya miji inakuwa mikubwa na Hatuwezi kupeleka barabara maji na umeme.
Mfano ukijenga maghorofa 10 ya floor 10 kila moja na kila floor inachukua familia 2 maana yake jengo moja litakuwa na familia 20,majengo 10 familia 200.
Ukijenga nyumba za chini 200 utachukua eneo kubwa sana na utahitaji mitandao ya maji barabara na umeme nk.
Watu wansobomolewa nyumba kupisha miradi wasilipwe fidia ila serikali ijengwe nyumba wahamishiwe kwenye hizo nyumba, fidia ilipwe tu kama kilichohusika kwenye mradi sio nyumba ya kuishi.
Sheria za miji ziheshimiwe, si kila nyumba ilio pembeni ya barabara basi iwe na frame(s)
Kuwe na maeneo maalumu ya biashara.
Nyumba kama za wamasai handeni zinatosha kwa watu wa hali ya chini, zikijengwa kama zile 1000 kila mwaka kureplace makazi holela nazo pia zitasaidia.
Haya ni mawazo yangu, hii sehemu ya makazi Magu hskuigusa, ni Wakati Wa mama kujichukulia ujiko eneo hili.