Hapana Tony, haya Mambo yanahusiana kwa karibu na kwa ujumla ni kitu kimoja. Wakenya mnahisi ninyi mpo sahihi kwa Kila jambo, katika kusema na kutenda.
Kawaida mtu yeyote anayejiona kwamba wakati wote yeye yupo sahihi, basi hataki kuona watu wengine wanaofanya tofauti na vile anavyopenda au anavyotaka yeye.
Kenya Kama nchi au Kama wakenya mnalo Hilo tatizo Sana, na ndio sababu Kenya inakwaruzana na majirani wake wote, mara utasikia Kenya na Uganda wanagombania Mambo ya maziwa ya lato, mara sukari, mara ushuru wa magari, ukija Kenya na Tanzania ndio kabisaa migogoro haikatiki.
Tanzania tukichoma vifaranga ni makosa, lakini Kenya mkizuia mahindi yetu kwa kisingizio cha "aflotoxin" hiyo ni sawa.
Anachokifanya "Nairobiwalker" hapa kukuchagulia nini la kusema, ndicho mlichomfanyia
Geza Ulole huko Skyscraper city mwisho alizuiliwa na mkampiga ban. Jambo la kushangaza, wewe unasifia kwamba Geza ni miongoni mwa watanzania hapa JF ambaye yupo independent, lakini huko Skyscraper city, hiyo indepence yake hamuhitaki
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app