Lazima tuanze kuyajenga kwa watoto wadogo wakiwa shule hadi university yaani haya yanakuwa ni masomo mtambuka...
Hili likifanyika ndio itajenga sense ya kuheshimu Katiba na sheria na kuwajibika vinginevyo kuweka tuu hizo Katiba bila maadili tutazipuuza tunatengeneza mazingira ya upigaji vilevile..
Binafsi kwangu kitu cha muhimu kwenye Katiba nataka mamlaka za serikali za mitaa zipewe nguvu za kujisimamia Ili tutumie rasilimali za maeneo yetu kujijenga kuliko ilivyo sasa unaletewa DED,DC,RC na mambo kama hayo na huna cha kuwafanya..
Naongezea pia somo la Uzalendo ni muhimu kwa watoto lifundishwe kuanzia ngazi za chini hadi juu.
Kufundishwa utunzaji wa mazingira na rasilimali zake ni muhimu sana.Sisi tukiwa wadogo tulikuwa tunaona machapisho mbalimbali kwenye kuta za umma, ofisini, mbao za matangazo na kalenda zinatoa maonyo mbali mbali.
Mfano; Maji ni uhai, Kata mti Panda mti, Miti chanzo cha mvua, Afya ni mali, Tunza mazingira ili yakutunze. N.K.
Hivi vilitujenga sana kisaikolojia kutambua na kuthamani utunzaji wa mazingira, mfano unaona picha ya mti inalia huku ikisema "Usinikate, mimi ninakuletea mvua, kuni, mbao na kivuli,kitotototo unaona ni kweli ukiukata utalia [emoji16][emoji16].
Hii mentality unakua nayo huwezi kukata mti bila sababu ya msingi. Saikolojia pia inatakiw kuwajenga watoto wakiwa bado wadogo ili tupate kizazi chenye maadili.
Hivi matangazo ya sasa hivi tunamsaidiaje mtoto mdogo, Jiunge Freemason uwe Tajiri, badala "Fanya kazi kwa bidii ",Utajiri wa majini, badala waseme Utajiri upo katika "Kilimo bora na Ufugaji"
Dawa za nguvu za kiume:Kwanini isiwe ili uwe na nguvu za kiume zingatia mlo bora na mazoezi?.
Zamani mtoto alivyokuwa akimaliza elimu ya msingi alikuwa na uwezo wa kufanya kazi za mikono baada ya stadi na maarifa aliyoyapata darasani na kuweza kujiajiri, sasa hivi muulize mtoto mboji ni nini na inatumikaje kama ataweza kukwambia. Kwanza ni mdogo kiumri halafu kujua maisha ni nini siyo rahisi kung'amua kutokana na maarifa aliyoyapata na umri wake.
Wazee wetu walikuwa na akili sana walitutunzia rasilimali zetu nyingi pamoja na kutokuwa na elimu ya darasani lakini mazingira waliyajua ipasavyo, leo hii tunajiita wasomi tunakwapua rasilimali za Taifa utadhani tutaenda nazo kaburini, hii ni kwasababu ya umasikini wa fikra, ubinafsi na uchoyo kwamba mwingine asipate.
Tusipowafundisha watoto wetu kujitambua,kujitathimini, kujua umuhimu wa rasilimali zetu na kuzitunza kama si kizazi hiki au vijavyo vitarudi utumwani na kutawaliwa kama ilivyokuwa zamani.
Mababu zetu walikufa kwa ajili yetu ili tuweze kujitawala, akina Mkwawa, Isike, Milambo, Mangi, Kimweri, walipinga kutawaliwa mpaka wengine wakasalitiwa.Hawakuwa wajinga walikataa kuwa vibaraka ili walinde rasilimali kwa ajili ya Fahari ya Mtanzania, leo hii hatuwaoni wa maana tunautukuza uzungu kwa kujua kuongea lugha yao tunajiona tumestaarabika, kumbe tunaelekea utumwani na kwenye ukoloni tena.
Hapa naongelea Afrika nzima,tusipojitambua tutapoteza vizazi vyetu. Sijasema tujitenge na watu lakini tutunze asili yetu kama Waafrika.
Misingi ya Taifa ikiwa mibovu huwezi kujenga Taifa lililo Imara. Turudi kwenye misingi yetu kwa kuwa na elimu yenye kutambua asili yetu. Tuboreshe mitaala ya elimu yetu.
Ahsanteni sana.