Ni neema kubwa mno, kwanza ile amani ya moyo tuliyo nayo sisi Watanzania na furaha ni jambo la kumshukuru Mungu sana.Ebu fikiria unaweza kutoka Mtwara hadi Bukoba hujaulizwa kitambulisho chako, unafika huko unageuza unakwenda hadi Mbeya hujaulizwa umetokea wapi, bado unaelekea Arusha hakuna mtu anakuuliza wewe ni kabila gani.
Kote huko kuna watu unakutana nao mnapeana namba mnawasiliana vizuri, siku ukiondoka unaulizwa vipi ulifika salama ndugu yangu/yetu.Tayari ni ndugu maana umeshafahamika.
Watu wakiuliza wewe ni wapi au kabila gani wanapenda kujua asili yako ili kama ukipatwa na tatizo wajue ni jinsi gani watakusaidia au kuwasiliana na ndg zako, wengine utakuta ni watani wako mnaanza kutaniana lakini si kwa ajili ya kukubagua.
Hata humu kuna wakati tunaitana ndg yangu, mkuu, boss,rafiki yangu,bro ,but it is quite different from Kenyans.