Nimehama Chama? Unadhani mimi ni zezeta wa CCM? CCM Ndio chanzo cha matatizo yote ya Tanzania na Ndio sababu hadi leo tupo kwenye hali ya chini ya kiuchumi.
Of course kuna vitu vizuri vinvavyofanywa na viongozi wa nchi ambao pia ni viongozi wa CCM, lakini ideology ya CCM na historian yake ni uchafu mtupu.
Halafu, nilishaongea kabla na nitarudia tena. Kuzuia mtoto kurudi shule ni kumsukuma kwenye shimo la umasikini. Especially mtoto wa kike. Watoto wengi wanaopata ujauzito Sio kwamba wanataka kupata ujauzito, ni kwasababu hawapati elimu ya uzazi shule na kutoka kwa wazazi wao. Pili, wengi wao wanarubuniwa na watu wazima! Kwa hiyo umasikini pia unachangia! Unafikiri kwanini zamani kulikuwa na matangazo yanayoonyesha watoto wa kike wakirubuniwa kwa Chipsi? Halafu pia kuna ubakaji! Tuna Hizi kesi za ubakaji Mara kwa Mara zinaishia chini chini bila kuripotiwa kwenye vyombo husika.
Hapa tunaongelea kuhusu watoto wenye umri chini ya Miaka 21! Ukimzuia mtoto mdogo namna hii kusoma, unampeleka wapi? Kujiuza? Kuwa house girl? Unamnyima fursa ya kumi endelea za kimaisha! Na huu ni upuuzi namba 1.