Chamoto
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 9,856
- 22,191
Mbona wananchi hawakupewa nafasi ya kumachagua Saitoti?Wewe huelewi maana ya neno demokrasia unataka ufundishwe kama mtoto mdogo. Demokrasia ni pale ambapo wananchi wenyewe wanapatiwa fursa ya kumchagua kiongozi wanaomtaka. Hata kama viongozi wote wanatokea kabila moja hakuna shida. Tofauti ya Egypt na Kenya ni kwamba Kenya raia wanapatiwa fursa ya kumchagua rais wao ilhali huko Egypt raia hawapati fursa ya kumchagua rais wao, wanatawaliwa kimabavu.
Kwani ni lazima rais awe mwanamke au LGBTQIA ndiyo kuwe na demokrasia?Marekani bado haijapata rais mwanamke ila sijasikia ukipinga kwamba Marekani ina demokrasia ya kweli.
FYI, 2016 ndani ya democrat, kuna wafuasi wengi wa Bernie hawakumpigia kura Hillary, ndiyo maana akakosa kura muhimu kwenye zile swing states. Hata hivyo, chaguzi za rais zinatumia mfumo wa electoral college ambao siyo demokrasia unayoiongelea wewe.

