chongchung
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 14,316
- 45,124
Kaka umesema uchumi wa maghorofa ukanikumbusha hiki kiwanda kikubwa sana Africa cha ngozi, magu mtu wa Chato aliwaambia NSSF waache kuwekeza kwenye artificial economy wa skyscrapers wawekeze kwenye viwanda kama hivi, halafu matako mmoja anasema magu hakujua biashara seriously?Mtoto (fetus) anapokuwa tumboni mwa mama yake, organ ya kwanza kabisa kujengwa katika kile kipindi cha rapid cell division (Mitosis) ni moyo. Kazi kubwa ya moyo ni usafirishaji wa damu ambayo inabeba virutubisho, taka na hewa. Bila ya kuwa na mfumo bora wa usafirishaji, mifumo mingine yote haiwezi kufanya kazi.
Ufanisi (maendeleo, ujenzi, uchumi, sayansi n.k) kwenye maisha ya mwanadamu ni kugeza yale yaliyokwisha fanywa kwenye asili (nature) na Muumba.
Mawazo ya kibiashara ya Magu yalikuwa ya kiwango cha juu sana, yeye aliangalia misingi ya kujenga uchumi imara. Sio uchumi "artificial" wa kina Dr. Dau wa kujenga maghorofa wakati hakuna watu wakupangisha majengo hayo.
Magu alisisitiza kwenye usafirishaji (barabara, ndege, meli, reli na bandari). Baada ya hapo akaja kwenye nishati (Bwawa la Nyerere) ili kupunguza gharama za umeme kwa viwanda, kuchochea uwekezaji. Yaani unakuta kiwanda cha saruji cha Tanga na bandari vinakosa wateja kwasababu reli iliyotegemewa imekufa, hamna anayejali. Anakuja mtu anaifufua reli hiyo halafu kuna watu kama Geza Ulole wanasema Magu hakuwa na mawazo ya kuichumi/biashara, kweli?
Hiki kiwanda kinapeleka bidhaa zake East Africa yote, kupata kiatu hapa ni mbinde aisee hii pesa wangeweka kwenye majengo tenants wangekuwa wanagombania spaces kama bidhaa za hiki kiwanda saivi?
. Kama unataka kuonyesha miradi ya mama onyesha, hakuna haja ya kumtaja au ku linganisha na JPM. Hii siyo sehemu yake. Kafanye hivyo kwenye majukwaa husika. Yamejaa tele. 